Social Icons

Saturday, April 7, 2012

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEPHEN CHARLES KANUMBA 'THE GREAT'

HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
 
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na  sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
 
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
 
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
 
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
 
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
 
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
 
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.



TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MORE PICS ZA HUKO MSIBANI KWA MAREHEMU STEVE KANUMBA

 
Ni alfajiri kabisa kama saa 12 hivi watu wengine wakiwa ndio wanaamka na wengine wakienda kulala na kupata mshtuko wa kuondokewa na kipenzi chao kwenye tasnia ya filamu hapa bongo Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatcan. Chazo kinasema Kanumba alitoka kuoga na kumkuta Lulu ambaye inasemekana ni wapenzi akiongea na simu ndipo hapo ugomvi ulipoanzia mpaka kanumba kujikuta akidondokea kisogo na kutokwa na damu nyingi. Kwa sasa msanii wa kike Lulu anashikiliwana police kwa maelezo zaidi
Watu wakiwa hawaamini kilichotokea 
  
Msanii Shilole akiwa hajielewi kabisa akiingia nyumbani kwa Marehemu
 Rafiki mkubwa wa marehemu anaitwa Tito yeye ndio alikuwa na mwili wa marehemu hadi hosp ya Mwimbili 




Msanii Johari akiwa kwenye huzuni kabisa akifanya mahojiano ya TV
Kijana huyu yeye alipopata habari pale pale alianguka chini
H.Baba akiwasili nyumbani kwa Marehe Steven Kanumba
 Steve Nyerere akiwasili nyumbani kwa marehemu akiwa kwenye majonzi mengi
Swahiba mkubwa wa Kanumba Ray akiwa mwenye huzuni nyingi 







 



 




TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

BREAKING NEWS LULU AKAMATWA AKIWA UCHI NI KIWEWE KIMEMSHIKA i





sasa Lulu(hot Lulu)yupo kituoni police
na mahututi kwani anamaumivu na majeraha mengi sana usoni,lulu kapasuliwa pia na Kanumba,hawa watu walikuwa wapenzi wa muda mrefu,chanzo ni simu jamani,kanumba aliona lulu anapigiwa simu za kuitwa sana kwenye madili,sasa jamaa(marehemu Kanumba)akashikwa wivu,duuu mapenzi ni hatarii
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

CHANZO CHA KIFO CHA STEPHEN CHARLES KANUMBA CHAFAAMIKA

KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU STEVE KANUMBA, ALISEMA KUWA ELIZABETH MICHAEL  MAARUFU KAMA LULU ALIKUJA NYUMBANI KUKAWA NA KAUGOMVI AMBAPO WAKAINGIA CHUMMBANI WAKIWA HUKO BAADA YA MUDA,LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE  KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA, YE ALIPOENDA AKAMKUTA KAANGUKA NDIO AKAENDA MUITA DAKTARI WA KANUMBA AMBAPO ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU, LAKINI  HADI TUNAVYOONGEA LULU YUKO POLISI OSTERBAY KWA AJILI YA MAHOJIANO NA POLISI

Inasemekana Lulu aligombana na marehemu Kanumba ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wake baada ya kukutwa akiongea na mwanaume mwingine kitendo ambacho kilimuudhi marehemu.. Lulu anasemekana kumsukuma marehemu na ndipo alianguka na umauti kumfikia jana usiku...
 R.I.P Steven Kanumba
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."