Social Icons

Tuesday, October 15, 2013

UFOO SARO; KUMBE CHANZO NI NYUMBA

Stori:  Brighton Masalu
KITENDO cha kudaiwa kugoma kuhama nyumba anayoishi mtangazaji wa Independent Television (ITV) na Radio One, Ufoo Peter Saro iliyopo Mbezi, Dar kinadaiwa ndiyo chanzo cha kupigwa risasi na kujeruhiwa na mchumba’ake, Anther Mushi ambaye naye alijiua.
Ufoo Peter Saro akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza na Uwazi, juzi nyumbani kwao Kibamba Dar, mdogo wa Ufoo aitwaye Goodluck Saro alisema ugomvi anaoujua yeye ni kitendo cha dada yake huyo kukataa kuhamia kwenye nyumba ya Kimara, Dar ambayo Anther aliipanga.
Alisema hajui kwa undani ni kwa nini dada yake alikuwa akigoma kuhamia makazi hayo mapya lakini kitendo hicho kilikuwa kikimfanya shemeji yake kubadilika.
“Siku za hivi karibuni shemeji alibadilika hata tabia. Zamani alikuwa akija anatuchangamkia sana, siku za hivi karibuni alikuwa akija, baada ya salamu haongei,” alisema Goodluck.
Baadhi ya wananchi na wanahabari waliofika hospitalini kumjua hali ya Ufoo juzi.
Wakizungumza na gazeti hili juzi, saa chache baada ya tukio hilo, baadhi ya majirani wa nyumbani kwa akina Ufoo walisema walishtushwa na milio ya risasi kutoka kwenye nyumba ya mama Ufoo, Anastazia Peter Saro wakidhani amevamiwa na majambazi.
“Ilikuwa saa kumi na moja alfajiri, mimi nilikuwa nimeshtuka kutoka usingizini lakini sijatoka kitandani, nilisikia milio ya risasi, nilijua mama Ufoo amevamiwa na majambazi.
“Lakini nikiwa najipanga jinsi ya kutoka nikasikia sauti ya mama Ufoo akisema jamani nakufa huku Ufoo akipiga kelele za kuomba msaada, nikashangaa maana najua haishi hapo, kwenda nikamuona Ufoo yupo nje akikimbia hovyo na damu chapachapa maeneo ya kifuani na mgongoni.
“Nilimuuliza kuna nini, kabla hajanijibu nikamwona mwanaume wake anatoka nje akiwa peku. Akasimama na kupiga risasi nyingine hewani kisha akaingia ndani.
“Muda huohuo nikasikia mlio mwingine wa risasi, nikajua kuna mauaji makubwa sana,” alisema jirani huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Jirani mwingine alisema alishtushwa sana na milio ya risasi, akaminya ndani akijua ni majambazi mpaka baadaye aliposikia watu wakilia huku wakisema mama Ufoo ameuawa kwa risasi na mkwe wake.
Habari nyingine zinadai kuwa Anther kabla ya kujiua, alikaa kwenye kochi kwanza na kujiandaa ambapo alisema: “Nimezaliwa siku moja nitakufa siku moja.” Akajilipua!
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura, marehemu Anther alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini Sudan.
Habari za ndani zinadai kuwa usiku wa kuamkia siku ya tukio, mwanaume huyo akiwa nyumbani kwa Ufoo, Mbezi, Dar  hawakulala kwa ugomvi ambapo marehemu alisikika akimshutumu mchumba wake huyo mambo ambayo hakuyaweka wazi.
Ikadaiwa kuwa ili kumaliza mgogoro, saa kumi na nusu alfajiri waliondoka kwenda Kibamba kwa mama wa Ufoo ili akasaidie kurejesha amani.
Katika kurudisha amani, mama Ufoo alikuwa mstari wa katikati, akiwa hapendelei lakini marehemu Anther alimshutumu mama mkwe wake huyo kwamba anampendelea mwanaye.
Ndipo alipotoa bastola na kuielekeza kwa mama Ufoo na kumpiga risasi ya kifuani. Mama huyo alianguka na kukata roho papo hapo.
Aliielekeza bastola kwa Ufoo na kumfyatulia risasi nne, mbili kifuani, moja begani na nyingine tumboni ambapo damu zilimtoka kwa wingi.
Ufoo alikimbizwa katika Hospitali Teule ya Tumbi (Kibaha) na baadaye kukimbizwa Muhimbili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MBUNGE ASAKWA KWA WIZI WA GARI

Stori:  Mwandishi Wetu
Bifu zito lipo hivi sasa kati ya Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani.
Gari la Amos Makalla aina ya BMW X5 ambalo linadaiwa kuchukuliwa na Profesa Maji Marefu.
Makalla anamtuhumu Ngonyani a.k.a Profesa Maji Marefu kuwa alichukua gari lake aina ya BMW X5 kisha akatokomea nalo kisha akawa anampigia simu hapokei na hata akimtumia SMS hajibu.
Kutokana na malalamiko hayo, hivi sasa Maji Marefu anasakwa na polisi wa Kituo cha Kati (Central), Dar es Salaam, tuhuma zikiwa ni wizi wa kuaminiwa, shauri lipo kwenye kitabu cha ripoti za polisi (Report Book ‘RB’) kwa namba CD/RB/13336/2013.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
NYEUPE NA NYEUSI YA TUHUMA ZENYEWE
Nyeupe na nyeusi (black and white) ya tuhuma hizo, inawekwa wazi na ‘sosi’ wetu ambaye aliliibia siri gazeti hili kwamba sakata kati ya Maji Marefu na Makalla lilianza tangu Julai, mwaka huu wakati waheshimiwa hao walipokuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam.
“Maji Marefu aliomba gari la Makalla ili alitumie kwa mizunguko ya siku moja tu lakini hakurudisha,” kilisema chanzo chetu. “Mgogoro mkubwa ulianza kuibuka kuanzia hapo na mpaka leo waheshimiwa hao hawazungumzi kwa salamu wala kutakiana heri.”
Chanzo chetu kiliendelea kusema: “Siku ya kwanza tu ilipopita, Makalla alimpigia simu Maji Marefu akawa hapokei, akimtumia SMS hajibu. Kwa kifupi Makalla alipoteza mawasiliano na Maji Marefu lakini aliendelea kusubiri kwa sababu anajua ni mtu wake.”
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani.
Habari zaidi zinasema kuwa kilipita kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja bila ya Makalla kumpata Maji Marefu kwenye simu lakini walikutana katika Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioketi kati ya Agosti 27 hadi Septemba 13, mwaka huu, Dodoma.
“Walipokutana Makalla alimuuliza Maji Marefu gari lake lipo wapi? Maji Marefu alimjibu alilikabidhi Lamada Hotel, Dar es Salaam,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza: “Unajua makabidhiano ya lile gari yalifanyika Lamada Hotel, kwamba angelirudisha baadaye lakini ikawa kimya.
“Hata hivyo, Makalla aliona siyo kesi kubwa, akafuatilia Lamada Hotel, menejimenti ya hoteli hiyo ilijibu kuwa gari hilo halijapelekwa pale. Vilevile baada ya kuzungumza siku hiyo, Maji Marefu alitoweka na bungeni hakuonekana tena.
“Baada ya kupata majibu hayo kutoka kwa Profesa Maji Marefu na Lamada, Makalla alifungua mashitaka Central, akidai kuibiwa gari lake na Maji Marefu.”
MAKALLA AFUNGUKA
Makalla ambaye ni Mbunge wa Mvomero (CCM) alipozungumza na mwandishi wetu alikubali kila kitu kisha akafunguka: “Niliomba polisi wanisaidie maana kwa hali iliyokuwepo ni kama nilikuwa nimeshatapeliwa. Vilevile niliripoti kwa Kamanda Mohamed Mpinga (mkuu wa kikosi cha usalama  barabarani) ili naye awaambie vijana wake wanisaidie kunitafutia gari langu.
“Nilimpa alama zote, rangi na namba za usajili. Oktoba Mosi, mwaka huu, ikiwa ni karibu miezi mitatu imepita tangu nimpe gari, polisi Tanga waliliona gari langu likiwa linaendeshwa na mheshimiwa Ngonyani (Maji Marefu) kwenye msafara wa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
“Nilimtumia SMS kumwambia kuwa gari langu ameonekana nalo katika msafara wa makamu wa rais. Polisi Tanga walitaka kumkamata lakini nikaomba aachwe kwanza, kukamatwa katika msafara wa makamu wa rais angeona amedhalilishwa.
“Nilimuomba baada ya msafara akalikabidhi gari kwa RPC Tanga kwa sababu linatafutwa na polisi. Akaniambia hawezi kulipeleka polisi kwa sababu tulikabidhiana vizuri. Nikamwambia sitaki kwa sababu alikuwa ananizungusha sana kunirudishia gari langu, mara aseme amelipeleka Lamada kumbe bado analo na wakati huohuo hapokei simu wala hajibu SMS zangu.”
USHAHIDI WA SMS
MAKALLA: “Mhe. pamoja na kutopokea simu na kutojibu meseji zangu, nakujulisha leo Oktoba Mosi, umeonekana na gari langu kwenye msafara wa makamu wa rais. Polisi walitaka wakukamate nikashauri wasubiri umalize mkutano. Kwa meseji hii naomba kesho asubuhi ukakabidhi gari langu kwa RPC Tanga, bila kukosa. Utamkuta ndugu Rajabu alipokee gari hilo baada ya ukaguzi mbele ya RPC.”
MAJI MAREFU: “Sawa nimekuelewa, yote ni makosa yangu na hii ni mali yako ila gari hatukupeana polisi, ungeniambia ulipo nikuletee.”
MAKALLA: “Sitaki umenizungusha sana, nilikukabidhi kwa heshima lakini umegeuka adui, hupokei simu huu ni mwezi wa tatu.”
MAJI MAREFU: “Ok nitafanya hivyo.”
MAKALLA ANAENDELEA
“Hakupeleka gari kwa RPC Tanga kama nilivyomtaka. Zilipita kama siku tatu, ndipo mtu mmoja akaenda kulitelekeza gari langu Lamada Hotel usiku. Walinzi walimuuliza yule mtu aliyetekeleza lile gari kwa nini anaacha gari na anakimbia? Hakujibu, akarukia kwenye pikipiki ambayo ilikuwa inalifuata lile gari kwa nyuma kisha akatoweka.
“Uongozi wa Lamada baada ya kuliona gari langu walinipigia simu, wakanijulisha nami nikapiga simu polisi, wakaenda kulichukua. Mpaka sasa gari lipo polisi central, wanasubiri kumkamata Mhe. Ngonyani ili kesi iendelee mbele.”
KAZI YA UWAZI
Gazeti hili baada ya kuzungumza na Makalla, lilikwenda kufanya upekuzi wake central na kubaini kwamba kesi hiyi ipo na madai yapo kama yalivyoelezwa.
Baada ya hapo, mwandishi wetu alimpigia simu Maji Marefu ambaye alipokea akiwa Nairobi, Kenya, na aliposomewa tuhuma dhidi yake, alijibu: “Subiri nirudi Dar, nitaeleza kila kitu.” Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;
MWANDISHI: Kuna madai kwamba ulichukua gari la Mheshimiwa Makalla, umekaa nalo miezi mitatu, kipindi chote hicho simu ulikuwa hupokei wala hujibu SMS zake.
MAJI MAREFU: Siyo kweli.
MWANDISHI: Labda ukweli ni upi.
MAJI MAREFU: Labda kwa sababu sipo Dar, nisubiri nirudi tutakaa tuzungumze.
MWANDISHI: Ungeniambia kwa kifupi tu ni kwa nini Makalla akushitaki, maana hii kesi ipo polisi, RB ipo na unatafutwa kwa tuhuma za wizi wa kuaminiwa.
MAJI MAREFU: Polisi wananitafuta mimi?
MWANDISHI: Ndiyo wanakutafuta wewe.
MAJI MAREFU: Kwa vile nipo Nairobi na wewe upo Dar, naomba usubiri tukutane kwanza ndipo nitaweza kueleza ukweli halafu ndipo mtaamua kuendelea mbele.
MWANDISHI: Sawa mheshimiwa, swali lingine wewe una ugomvi na Mheshimiwa Makalla?
MAJI MAREFU: Aah, ndiyo nikasema tukikutana ndiyo italeta picha nzuri. Kama natafutwa au kuna tukio lolote nitaeleza.
MWANDISHI: Sawa mheshimiwa, basi nijibu swali hili, wewe una ugomvi na Makalla?
MAJI MAREFU: Sina ugomvi naye.
MWANDISHI: Sasa kwa nini akushtaki kwa wizi wa gari lake?
MAREFU: Naomba tukutane nikirudi nitaongea tu.
MWANDISHI: Inasemekana hilo gari uliwahi kumwambia Makalla kwamba uliliacha Lamada Hotel lakini baadaye ukaonekana nalo kwenye msafara wa makamu wa rais Tanga. Hili limekaaje?
MAJI MAREFU: Mimi nina magari zaidi ya 15, nitakupeleka uone kama mimi nina shida ya gari. Nyumbani kwangu kuna magari ya kila aina.
MWANDISHI: Ni kweli Makalla alikukabidhi gari?
MAJI MAREFU: Subiri nirudi Dar nitaongelea hilo.
MWANDISHI: Nijibu tu hilo moja tu, alikupa au hakukupa?
MAJI MAREFU: Kwani yeye anasema nilimnyang’anya au alinipa?
MWANDISHI: Anasema alikupa.
MAJI MAREFU: Sasa subiri nirudi nitaeleza ukweli wangu.
MWANDISHI: Kwani mheshimiwa inashindikana nini kunijibu swali hili moja tu? Alikupa au hakukupa?
MAJI MAREFU: Ukweli mtaupata nikisharudi Dar.
POLISI NAKO
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alipoulizwa kuhusu kesi hiyo, kwanza alisema hajapata taarifa yoyote kuhusu sakata hilo mpaka afuatilie.
Siku iliyofuata, Kova alipigiwa tena simu akaulizwa kuhusu sakata hilo, akajibu: “Kuna mtu wa Uwazi alinipigia simu jana kuhusu hii kesi, unajua mimi ni kamishna, hii kesi ni ndogo na siyo kila kesi lazima nijibu mimi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Saturday, October 12, 2013

MFAHAMU JACKLINE WOLPER FEKI ANAEWATAPELI WATU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

kumekuwa na wimbi kubwa la matapeli kwenye mitandao ya kijamii hususan FACEBOOK, TWITTER, BBM na mingine mingi. Jana katika pita pita zangu kwenye mtanfao wa Facebook nilipokea ujumbe ukionesha Jackline Wolper anaomba urafiki nami bila kusita nika confirm obi lake. Leo nilipoingia inbox yangu ya facebook nilikuta ujumbe huu.


  • Conversation started today
  • Jackline Wolper
    Jackline Wolper

    Hello, sorry naweza kukusumbua kitu nw?
  • Jackline Wolper
    Jackline Wolper

    Naomba nisaidie, niko nyumban and sijatoka bado kuna kaz naifanya kwenye computer, kazi ya ofisini. Umeme Umeniishia naomba niazime 20,000 ninunue then baadae nikitoka nakurudishia.
  • Pablo Junior Calter I
    Pablo Junior Calter I

    ohky haina tatizo sasa hizo pesa nitakupatiaje ama una tigopesa?
  • Jackline Wolper
    Jackline Wolper

    0712394346, Jina litokee jackline massawe
  • Pablo Junior Calter I
    Pablo Junior Calter I

    sawa wng so utanirudishia lini
  • Jackline Wolper
    Jackline Wolper

    Baadae nakutumia, kuna kazi nikiimaliza ndo ntatoka, naomba nitumie bas sasa ivi Pablo
  • Pablo Junior Calter I
    Pablo Junior Calter I


    poa nakutumia

    na hii ni picha ya chat tuliyofanya

    chat yangu na jackline wolper feki
     
    Facebook wapo watu wengi sana wenye hii tabia ambayo sio nzuri kwakweli wasanii wetu kila siku wana lalamika kuwa majina yao yanatumiwa vibaya jambo ambalo sio jema guys kwa wewe mwenye huu mchezo nakushauri uache maana iko siku utagundulika tu "ZA MWIZI NI AROBAINI".


    fungua hapa kuangalia hio account fake ya Jackline Wolper

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

HAUSIGELI AMNYONGA MTOTO

Gladness Mallya na Hamida Hassan
NI ukatili uliopitiliza! Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu, Risasi Jumamosi limekamata tukio zima.
Mtoto Arafat Allan enzi za uhai wake.
Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.
AONDOKA NA MTOTO
Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
“Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la kesi KB/RB/1154/2013 TAARIFA.
HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume  imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
Baba wa marehemu akiwa hospitali.
“Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,” alisema huku machozi yakimtoka.
MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.
Mama wa marehemu akiwa hospitali baada ya kuzimia.
MAUAJI YAHUSISHWA NA USHIRIKINA
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita akiwemo mama wa marehemu, walisema kwa siku mbili hizo alizofanya kazi hausigeli huyo alionekana kuwa na mambo ya kishirikina kwani asubuhi ya siku ya tukio aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja.
“Siku hiyo ya Jumapili huyo mdada wa kazi aliamka akiwa amenyolewa nywele upande mmoja, alipoambiwa amalizie zote alikataa akisema atanyoa baada ya kutoka sokoni ambapo hakurudi tena,” alisema mama wa marehemu.
HAUSIGELI AKAMATWA
Jumatatu iliyopita, siku moja baada ya tukio, hausigeli huyo alikutwa akirandaranda stendi akiomba fedha za nauli ili arudi kwao Mbeya lakini alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo kidogo cha polisi.
Habari zinasema hali kwenye kituo hicho ilikuwa mbaya kufuatia baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujaribu kukivamia ili wamuue mtuhumiwa huyo. Ilibidi mtuhumiwa ahamishiwe Kituo cha Polisi cha Tumbi, Kibaha.
MANENO YA WATU WA KARIBU
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia hiyo, msichana huyo aliokotwa na ndugu wa baba wa marehemu baada ya kumkuta barabarani akiomba msaada akidai anateswa na ndugu zake, wakampeleka kwa baba wa marehemu ili wamsaidie ambapo walimpa shughuli ya kazi za ndani.
Baba wa marehemu, Allan hakuweza kuzungumza kutokana na kuwa kwenye hali mbaya katika Zahanati ya Kellen alikolazwa baada ya mwanaye kuzikwa katika Makaburi ya Mailimoja, Jumatano iliyopita.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MAPENZI YAMPOTEZA SKAINA

Stori: Brighton Masalu
STAA wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ amepotea kwenye gemu chanzo kikidaiwa kuwa ni mapenzi kwani kila mwanaume anayeanzisha naye uhusiano wa kimapenzi, humzuia kuendelea kufanya kazi za sanaa.
‘Akibadilishana sentensi’ na mwandishi wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema kitendo cha wanaume wengi wanaoanzisha uhusiano na Skaina kumzuia kuendelea na kazi ya uigizaji, kimechangia kumpoteza.
Mwandishi wetu ‘alipomvutia waya’ Skaina, aliambulia majibu ya ‘sintofahamu’ huku akisisitiza kutosumbuliwa.
“Sasa kama umeambiwa hivyo mnachoniuliza hapo ni nini? Kwani lazima niigize mara kwa mara? Mimi naipenda kazi yangu, sitaki maswali zaidi,” alisema Skaina.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

JACK DUSTAN AZURURA NUSU UTUPU DUBAI

Stori: Imelda Mtema
MREMBO aliyefahamika kupitia Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dustan, amenaswa akizururura mitaani na kibukta kifupi mithili ya nguo ya ndani.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni pande za Dubai ambapo baada ya paparazi wetu kuzinyaka picha hizo, iliibuka minong’ono ya kulikoni avae hivyo wakati raia wengi wa huko wanavaa mavazi ya heshima.
Akichonga  na Weekly Star Exclusive, rafiki mkubwa wa Jacqueline ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini ambaye ndiye aliyevujisha picha hizo,  alisema hata yeye alimshangaa sana shosti wake kwa kumtumia picha hizo.
“Sikuamiani kabisa kama ni yeye kwa maana sijawahi kumuona akivaa hivi huku Bongo japokuwa anavaa nguo fupi lakini siyo kama hicho kibukta alichokivaa na kukatiza mitaani bila wasiwasi wowote,” alisema rafiki huyo na kuongeza:
“Nilipojaribu kumuuliza kulikoni avae kikaptula hicho tena katika nchi za watu wanaojiheshimu, akadai kwake siyo ishu na zaidi ni Wabongo ndiyo wanaopenda kufuatilia maisha ya watu.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

WASTARA ASEMA KUOLEWA NI LAZIMA

Stori: Brighton Masalu
MWIGIZAJI mahiri Bongo, Wastara Juma Issa Abeid ‘Wastara’ amesema suala la kuolewa tena halikwepeki licha ya kutokuwa na mawazo juu ya suala hilo kwa sasa.
Akizungumza na paparazi wetu, Wastara ambaye ni nadra sana kukosea awapo mbele ya kamera, alisema yeye kama mwanamke aliyekamilika hadhani kama atakaa bila mwanaume lazima ataolewa tena.
“Mimi ni mwanamke niliyekamilika, suala la kuolewa ni lazima, japo kwa sasa sifikirii kufanya hivyo, lakini sidhani kama nitaweza kukaa bila mwanaume, lakini pia usumbufu kutoka kwao unaendelea,” alisema Wastara
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MIMBA ROSE NDAUKA YAWA KIVUTIO...

Na Imelda Mtema
MUONEKANO mpya wa ‘kubugia kijusi’ wa msanii wa filamu za Kibongo, Rose Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ umezua miguno, minong’ono huku ikionekana kivutio kwa wengi na kubaki wakihoji maswali yasiyojibika haraka, Risasi Jumamosi linaifunua.
Hayo yalichukua nafasi hivi karibuni wakati staa huyo alipofanya sherehe ya kutimiza miaka kadhaa tangu ‘anuse hewa ya Oksijeni’ iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Club Escape Beach Kigamboni jijini Dar na kuacha historia ya aina yake.
Baadhi ya wahudhuriaji wa sherehe hiyo, walionekana kuwa na viulizo vingi juu ya mimba yake, huku gauni fupi alilovaa siku hiyo likiionesha kwa ufasaha mimba hiyo na kufanya baadhi yao kubaki wasiamini kama kweli msanii huyo amechukua uamuzi wa kuzaa kabla ya ndoa.
“Mh! hivi kweli Rose ana mimba?, siamini kama ameamua kuzaa kabla ya ndoa si alikuwa akikataa huyu? Sasa imekuwaje” alisikika mama mmoja katika sherehe hiyo.
“Ila kapendeza jamani, sasa kaonekana mwanamke kweli,  muone anavyotembea kwa madaha, mimba hiyo imemuongezea mvuto!” alisema msanii mwingine wa kike mwenye ‘taito’ kubwa bongo.
Mwandishi wetu alipomuuliza Rose juu ya minong’ono hiyo, alijibu kwa kifupi huku akionekana kufurahia.
“Jamani sina jibu la kuwapa, kama watu wanashangaa ni wao niseme nini tena?” alisema Rose na kisha kufunga ‘faili’ la mazungumzo na mwandishi wetu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

SNURA: SIKATI MAUNO ILI NIIBE WANAUME

Stori: Mayasa Mariwata
STAA wa Majanga, Snura Antony Mushi ‘Snura’ amesema kamwe wanaume za watu wasimmendee katika shoo zake kwani hakati mauno ili kuwapata hasa wenye wake.
Akipiga stori na paparazi wetu, Snura alisema kukata mauno kwenye shoo ndiyo silaha yake ya kuwateka mashabiki lakini anashangaa kuona wanaume za watu ndiyo wanaongoza kwa kutuma maombi ya kutongoza.
“Sipendi kabisa kusikia masuala ya wanaume za watu, siko tayari kuvunja ndoa za watu. Pesa za kuhongwa sioni raha nazo hata kidogo napenda za kujitafutia za kwangu,” alisema Snura.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Friday, October 11, 2013

UMEIONA TATOO MPYA YA LULU? KAMA BADO ICHEKI HAPA IMEANDIKWA "ONLY GOD CAN JUDGE ME"




O yes "ONLY GOD CAN JUDGE ME."
 
credits :jestina george
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

KUHONGWA KWA LINAH KWAIBUA MAMBO

Na Mwandishi Wetu
MAELEZO ya hivi karibuni aliyodaiwa kuyatoa mwanamuziki Estelina Sanga ‘Linah’ mtandaoni kuwa mtaji wake katika kazi za ujasiriamali ameupata kwa kuhongwa na mpenzi wake na kuchanganya na pesa zake yameibua mambo.
Wakionesha kushangazwa kwao na maelezo hayo, baadhi ya mashabiki wake walisema kitendo cha yeye kukiri kuwa anahongwa kinawashawishi wasichana wengine wahisi nao bila kuhongwa hawawezi kufanikiwa.
“Huyu anasema mtaji wake ameupata kwa kuhongwa na mpenzi wake, ina maana asingehongwa asingefika hapo alipo? Na sisi tutafute wa kutuhonga ili tufanikiwe? Lakini kwani mpenzi wako akikupa pesa anakuhonga? Linah asitupotoshe,” alisema Neema Kiza.
Mdau mwingine ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema: “Eti anasema amehongwa na mpenzi wake, sasa anatuambia ili iweje? Hata hivyo, mpenzi wako anapokupa pesa hakuhongi, anakusaidia, alijue hilo.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MUHIMBILI YATIKISIKA!

Stori: Waandishi Wetu
WIKI moja baada ya gazeti hili kuibua skendo nzito ya uozo ndani yake, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imetikisika huku viongozi wake wakiweweseka na kutapatapa kujinasua katika kashfa hiyo.
Daktari feki akimwangalia mgonjwa wodini.
RIPOTI YA UOZO
Habari za uhakika zilieleza kuwa patashika imejitokeza baada ya mwandishi wa Global Publishers kujigeuza daktari kisha kufanya kazi kwenye hospitali hiyo kwa siku tatu mfululizo bila kushtukiwa na uongozi wala walinzi na kuibua uozo huo.
Tukio hilo liliripotiwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti hili toleo Namba 847 la Oktoba 4-10,2013 iliyopewa kichwa cha habari; KIOJA MUHIMBILI, MWANDISHI GLOBAL AJIFANYA DOKTA MUHIMBILI, AFANYA KAZI ZA UDAKTARI KWA SIKU TATU BILA KUSHTUKIWA.
Katika habari hiyo, mwandishi wetu alisimulia jinsi usalama wa wagonjwa kwenye hospitali hiyo ulivyo mdogo kiasi cha kumuwezesha mtu yeyote ambaye si daktari kuingia wodini akiwa na mavazi ya kidaktari, kuona wagonjwa, kusoma mafaili yao, kuingia chumba cha upasuaji hadi katika ofisi za utawala bila kushtukiwa.
...Akiongea na wagonjwa.
LENGO LILIKUWA KUTOA TAHADHARI
Hata hivyo, lengo la habari hiyo lilikuwa kutoa tahadhari juu ya usalama wa wagonjwa na hospitali nzima ili kusije tokea hatari ya aina yoyote hivyo kuwafanya viongozi wa hospitali hiyo kuchukua hatua kwa kuboresha ulinzi na umakini.
Mara baada ya habari hiyo kuingia mtaani Ijumaa iliyopita na kuibua mshtuko mkubwa, siku mbili baadaye uongozi wa Muhimbili ulituma barua kwenye gazeti hili ukitaka maelezo ya kile kilichoandikwa huku ukihitaji majibu ndani ya siku mbili.
Wakati barua yao ikijibiwa, uongozi huo ulitoa taarifa kwa umma kupitia magazeti mbalimbali ukidai kuwa habari hiyo haikuwa na ukweli na kwamba mwandishi huyo hakufanya kazi za udaktari hivyo gazeti hili linalazimika kuthibitisha ukweli wa kilichoandikwa.
Matukio yote aliyoyafanya mwandishi huyo aliyejifanya dokta yalikuwa yakirekodiwa kwa picha za mnato na video hivyo ushahidi wa habari hiyo mahakamani upo wa kutosha.
...Akiwa ndani ya hospitali.
MASWALI
Taarifa kwa umma iliyotolewa na hospitali hiyo ilieleza kuwa katika habari ya gazeti hili hakuna mahali palipoonesha kuwa mwandishi huyo alifanya kazi ya udaktari jambo lililoibua maswali kwa walioisoma taarifa hiyo ukilinganisha na habari ya kwenye gazeti.
Taarifa ya hospitali hiyo imehoji mambo kadhaa iliyodai kuwa ndiyo majukumu ya daktari ambayo mwandishi wetu hakuweza kuyafanya.
USHAHIDI WA KUMWAGA
‘Daktari’ wetu alifanya mambo kadhaa yanayofanywa na madaktari wa hospitali hiyo ambayo pia yamerekodiwa kama ifuatavyo:
Kwanza, alifanikiwa kuingia katika wodi za Mwaisela na Kibasila na kukagua wagonjwa. Akiwa huko aliuliza maendeleo yao sanjari na kusikiliza matatizo.
..Akikagua vyeti vya wagonjwa.
Pia, akiwa katika mavazi hayo ya kidaktari, aliaminiwa na wagonjwa kiasi cha kupewa kusoma mafaili yao kwenye vyeti vya X-Ray. Tena mgonjwa aliyekuwa na cheti cha X-Ray ni mfungwa.
Pia, ‘dokta’ wa Global Publishers aliweza kushirikiana na wahudumu wengine wa hospitali hiyo kujua ratiba za siku za madaktari na kuingia hadi chumba cha upasuaji.
Ijumaa linaamini kuwa uongozi wa hospitali hiyo ya umma umekurupuka kutoa taarifa kwa kutumia fedha za walipa kodi bila kusoma habari yetu mstari kwa mstari kwani ilifafanua kila kitu.
Mwandishi wetu alifanya vitu hivyo vyote huku akipishana na kusalimiana na madaktari wengine ndani ya hospitali hiyo na kumalizia kwenye Ofisi ya Ofisa Habari, Aminieli Aligaesha ambaye pia alizungumza naye bila kushtukiwa.
WAGONJWA WANASEMAJE?
Wakati hayo yakiendelea huku uongozi ukitaka kujinasua katika kashfa hiyo nzito, gazeti hili liliendelea na uchunguzi wiki hii ndani ya hospitali hiyo ambapo lilizungumza na wagonjwa waliosoma habari hiyo wiki iliyopita kisha wakamwaga maoni yao.
Katika Wodi ya Mwaisela, mmoja wa wagonjwa waliolazwa mwanzoni mwa wiki hii alilieleza gazeti hili kwamba kwa habari hiyo ni dhahiri kuwa kuna uzembe mkubwa ndani ya hospitali hiyo hasa juu ya usalama wa wagonjwa na taasisi kwa jumla.
“Kama hali ndiyo hii, inawezekana mtu hatari akaingia wodini na kujifanya daktari kisha akawachoma sindano ya sumu wagonjwa wote wakafa. Litakuwa ni janga kubwa. Afadhali gazeti limetoa angalizo ili yakitokea ya kutokea watu waseme Gazeti la Ijumaa lilitahadharisha juu ya suala hilo,” alisema.
MKURUGENZI ANG’OLEWE
“Lakini kwa nini tufike huko wakati kuna uwezekano wa kuzuia yasitokee? Kwa kashfa hii, Mkurugenzi wa Muhimbili (Dkt. Marina Njelekela) ang’olewe ili tuokoe hatari hii kwani ameshindwa kazi,” alipendekeza mgonjwa mwingine.
Juu ya habari hiyo, baadhi ya wagonjwa kwenye Wodi ya Kibasila hospitalini hapo walisema kuwa kuna kila sababu ya kuongeza umakini hasa suala la kutambuana ili kuziba mwanya kwa mtu mwingine mwenye nia mbaya na asiye daktari kufanya hujuma yoyote.
“Hapa kuna tatizo la umakini hasa suala la vitambulisho vya kutambuana. Kwa hali ilivyokuwa ilikuwa rahisi kwa mtu yeyote kuvaa koti jeupe na kubeba kipimo kisha kuingia wodini kwa heshima zote bila kuzuiliwa popote.
“Uongozi ulipaswa kulishughulikia suala hilo badala ya kuanza kutumia nguvu kubwa kukanusha habari wakati ukweli ni kwamba hali ya usalama Muhimbili ni tete,” alisema mmoja wa wagonjwa wodini hapo na kuongeza:
“Unajua taasisi nyingi za serikali hawapendi kukosolewa au kuambiwa ukweli, wanapenda kusifiwa tu jambo ambalo haliwezekani kwani hata siku hazifanani. Hapa lazima Waziri wa Afya (na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi) achukue hatua mara moja ili hii ishu isipite hivihivi.
“Penye hatari lazima pawe na tahadhari, watu wajipange, wawe makini zaidi, siyo kwamba hawapo makini lakini ni vema umakini ukaongezeka hasa kwa kipindi tulichonacho cha tishio la ugaidi.”
MSISITIZO
Dawati la Gazeti la Ijumaa linasisitiza kuwa lengo la habari ile halikuwa baya bali ni kupima ulinzi na umakini wa hospitali yetu, kwa vile ndiyo kubwa na inayotegemewa na umma. Hii ni hospitali ya Watanzania, ni jukumu letu kusaidia kuwakumbusha waliopewa dhamana kuwa makini.
Tunawaomba viongozi wa Muhimbili kuchukua habari yetu kama changamoto, kama walivyofanya watu wa Mlimani City na Uwanja wa Taifa ambao baada ya sisi kuandika habari za kueleza upungufu wa ulinzi katika maeneo hayo, mara moja walichukua hatua.
IJUMAA KUPELEKA RIPOTI KWA JK
Endapo uongozi wa Muhimbili utaendelea kutumia fedha za walipa kodi kukanusha ukweli huu kwa kusambaza ripoti kwenye vyombo vya habari,  gazeti hili lipo tayari kupeleka video yenye tukio zima kwa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa hatua muafaka.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MSANII BONGO MOVIE AVULIWA NGUO CHINA

Na Imelda Mtema
MSANII wa Bongo Movie, Devota Mbaga hivi karibuni alipatwa na kisanga cha mwaka baada ya kuvuliwa nguo na maofisa wa uhamiaji alipoenda Hong Kong, nchini China kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara.
Devota Mbaga.
Kwa mujibu wa staa huyo, alifanyiwa kitendo hicho cha kuvuliwa nguo zote na maofisa wa uhamiaji mara alipotua Uwanja wa Ndege wa Hong Kong na kumsachi kwa kuhofiwa kuwa amebeba ‘unga’.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Devota alisema baada ya kuvuliwa, alishikwa sehemu zake za siri kitendo alichokiita ni cha kidhalilishaji.
“Ilikuwa ni baada ya kugongewa pasipoti yangu nikaingizwa kwenye kitengo cha polisi wa madawa ya kulevya ambao walinitaka nivue nguo zote ili nikaguliwe,” alisema kwa masikitiko.
Msanii huyo alisema mbaya zaidi siku hiyo alikuwa katika mzunguko wake wa mwezi lakini maofisa hao hawakujali.
Kama vile haitoshi, Devota alisema kuwa, baada ya kumalizika kwa zoezi hilo maofisa hao walimchezea sehemu za kifuani huku wakimwambia kama hakutaka kufanyiwa hivyo angerudishwa alikotoka.
 “Kwa kweli nimeumia sana kwa kitendo nilichofanyiwa, nimeshinda nikilia kutwa nzima na kila nikikumbuka naumia,” alisema Devota.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."