Social Icons

Tuesday, September 17, 2013

KISA NGONO, DENTI AMCHOMA KISU BABA YAKE

Stori: Richard Konga, Arusha
DENTI wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo (jina  tunalo) iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha, anadaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba yake mzazi Daudi Msemo baada ya kuonywa kuachana na tabia ya kuchanganya ngono na masomo, Uwazi limeambiwa.
Denti wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo anayedaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba yake mzazi Daudi Msemo.
Hayo yamesemwa na Fatuma Daudi ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi huyo mara baada kutokea tukio hilo la kusikitisha hivi karibuni nyumbani kwao Monduli ambapo denti alipofikishwa polisi alisema alifanya kitendo hicho kwa sababu baba yake alitaka kumbaka.
“Binti yetu huyu amekuwa akibadilika tabia na mara nyingi tumekuwa tukimuonya aache vitendo vya umalaya akiwa mwanafunzi lakini bado amekuwa akiendeleza tabia yake hiyo ambayo sisi wazazi tumeona ni kudharau maagizo yetu,” alisema Fatuna alipozungumza na gazeti hili.
Aliongeza kuwa, tabia hiyo ilikuwa ikimfanya mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kutorudi kabisa.
Mama huyo alisema, kutokana na tabia hiyo  waliamua kumdhibiti ili aache lakini matokeo yake alimchoma kisu baba yake na akamsingizia alitaka kumbaka hali iliyowalazimisha polisi kuwaweka ndani wote.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
Fatuma alikwenda mbali zaidi kwa kuwaomba baadhi ya wanajeshi ambao wana uhusiano wa kimapenzi na binti huyo waache kwa kuwa ni kinyume cha maadili na mwanaye bado ni mwanafunzi wa kidato cha nne.
Maelezo ya denti huyo yalimfanya baba mzazi kuahidi kujiua baada ya kutoka kituoni hapo akidai amedhalilishwa sana, hali iliyowafanya polisi kuamua kuendelea kumshikilia licha ya kwamba walishamruhusu kutoka baada ya mkewe kumtetea.
Afisa mmoja wa jeshi la polisi ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tunaendelea na uchunguzi na wote wawili, baba na mwanaye tunawashikilia ili kubaini chanzo cha kutokea kwa tukio hilo, baada ya uchunguzi maelezo zaidi utapewa na kamanda wa mkoa afande Liberatus Sabas, kwani ndiye msemaji wa jeshi mkoani hapa,” alisema afisa huyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

KIJIJI CHA UNGA CHAFUMULIWA...

Stori: Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
JIJI la Dar es Salaam lina mambo mengi lakini moja ambalo linatisha ni kugundulika kwa kijiji cha madawa ya kulevya ambacho kipo kando ya Bahari ya Hindi.
Mwili ulioshonewa madawa ya kulevya.
Kijiji hicho ni Kunduchi, nje kidogo ya jiji na uchunguzi wa gazeti hili umeonesha kuwa, madawa ya kulevya yenye thamani ya mabilioni ya shilingi yamekuwa yakikamatwa katika eneo hilo.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Uwazi kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walisema matajiri wengi wa ‘unga’ wamekuwa wakitumia eneo hilo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni salama kwa shughuli hiyo.
Kijiji cha dawa za kulevya kilichopo Kunduchi jijini Dar.
“Hapa Kunduchi ni kando ya bahari, wengi wanatumia majahazi au boti za uvuvi kuingiza mihadarati hiyo. Wanapoleta madawa yao wanaonekana kama wanatoa samaki au mizigo mingine ya kawaida lakini kumbe ni madawa ya kulevya,” alisema kijana mmoja.
Mzee wa siku nyingi wa kijiji hicho alisema anasikitishwa kuona kuwa kitongoji chao kimekuwa makao makuu ya biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya na yanauzwa wakati serikali ipo.
“Kuna wakati tulitaka sana kijengwe kituo cha polisi lakini tukaambiwa kuna matajiri hawataki hilo, hivyo ajenda hiyo ikaisha na wengi tunaamini matajiri kwa kutumia fedha hawaruhusu kituo cha polisi kuwepo eneo hilo ndiyo maana hakijengwi,” alisema mzee huyo na kuongeza kuwa Kituo cha Polisi cha Silver Sands kiko mbali sana.
Dawa za kulevya.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa watuhumiwa wengi wa madawa hayo haramu wanakamatiwa katika kijiji hicho.
Kwa mfano, Fred William Chande na wenzake wanane waliwahi kukamatwa kwa madai ya kuwa na madawa hayo aina ya heroin yenye thamani ya shilingi bilioni 6.4 Februari 21, 2011 na tayari wamefunguliwa kesi namba 1/ 2012 Mahakama Kuu ya Tanzania.
Chanzo kingine cha habari kilidai kuwa hata madawa aina ya Crystal Methamphetamine kilo 150 yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8 walizokamatwa nazo Agness Jerald ‘Masogange’ na Melisa Edward nchini Afrika Kusini chimbuko lake ni Kunduchi.
Naye Mwanaidi Ramadhan na wenzake wanane wanadaiwa kukamatwa na madawa aina ya heroin yenye gramu 2,083.3 ambayo thamani yake ni mamilioni ya shilingi, eneo la Mbezi Beach Kata ya Kunduchi, Dar na tayari polisi wamewafungulia kesi mahakama kuu ambapo jalada lao ni namba 10/2012. Walikamatwa Juni 1, 2011.
Naye Ally Murzai Pirbakshy ‘Haji’ na wenzake watatu walikamatwa wakidaiwa kuwa na  madawa aina ya heroin yenye thamani ya mamilioni ya shilingi na uzito wa gramu 3,053.5 Septemba 7, 2011. Nao wamefikishwa mahakama kuu na kufunguliwa kesi namba 10/2012.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamishna Godfrey Nzowa alipoulizwa juu ya kijiji hicho alisema polisi wamekuwa wakifanya kazi kubwa  kwa kushirikiana na wananchi na matokeo yake yamekuwa mazuri.
“Yeyote ambaye ana habari juu ya wanaofanya biashara hiyo aje kuniona na njia ya bahari tunaidhibiti, wasijidanyanye kuitumia kwani kuna wenzao walifanya hivyo Lindi tukawakamata, ”alisema Nzowa.
 CREDIT:Global Publishers
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

HUYU NDIYE JAMAA ALIENASWA KWA WIZI WA MAGARI..!! AKUTWA NA LUNDO LA MAGARI YA THAMANI...!!



Kigogo wa magari ya wizi, Benovilla Luhanga baada ya kunaswa.
Jengo ambalo linadaiwa ndiyo kiwanda hatari cha kubadilisha magari ya wizi, kimefumuliwa na mmiliki wake sasa hivi yupo nyuma ya nondo akingoja kufikishwa mahakamani. Benovilla Luhanga, 43, ametajwa kuwa ndiye mmiliki wa kiwanda hicho na siku ananaswa, alikutwa na magari ya kihafari matano ambayo yote inadaiwa ni ya wizi.
Vilevile, Luhanga alikutwa na Bajaj moja ambayo imedaiwa nayo ni ya wizi na kwamba alikuwa tayari ameshaibadili rangi.
Luhanga alikamatwa akiwa na mkewe ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

 
Moja ya gari alilokutwa nalo mtuhumiwa.
Kigogo huyo na mkewe, wanaishi ndani ya nyumba hiyo iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, kwa nje huonekana kama gereji lakini ndani ni makazi ya watu na shughuli za ubadilishaji magari, Bajaj na pikipiki hufanyika humo.
Luhanga na mkewe walikamatwa baada ya polisi kuvamia kiwanda hicho, saa 5 asubuhi lakini mchakato wa ukamataji ulikamilika saa 10 alasiri.
Mchakato wa kuwakamata uliwagharimu polisi jumla ya saa 5 kukamilika kwa sababu ilibidi kufanya upekuzi wa hali ya juu kwenye kiwanda hicho ili kubeba kila kitu kilichoonekana ni cha wizi.
Magari yote yaliyokutwa kwenye kiwanda hicho pamoja na Bajaj moja, ilidaiwa ni mali za wizi huku tayari yakiwa yameshabadilishwa rangi na kufungwa namba feki za usajili, isipokuwa gari moja.

Gari aina ya Nissan Navara lenye thamani ya shilingi milioni 45 alilokutwa nalo mtuhumiwa.
ZA MWIZI ZILIVYOTIMIA
Habari zinaeleza kuwa kuwa kiwanda hicho kiligundulika kutokana na kijana mmoja ambaye aliwahi kuibiwa gari aina ya Toyota Canter, Goba, Dar, hivi karibuni.
Imebainika kuwa kijana huyo baada ya kuporwa gari hilo ambalo yeye alikuwa ameajiriwa kama dereva, maisha yalimwendea kombo kabla ya kwenda kwa Luhanga kuomba kazi, akidhani ni gereji.
Chanzo chetu kilitamka kuwa akiwa ndani ya kiwanda hicho, kijana huyo aliliona hilo Toyota Canter ndani ya uzio wa kiwanda hicho, hivyo kutoa taarifa Kituo cha Polisi Kawe, Kinondoni, Dar.
“Baada ya kuripoti, askari walifuatilia na kukuta kweli kuna gari aliloibiwa kijana huyo na walipofanya upekuzi wakayakuta magari mengine matano yaliyoripotiwa kuibwa,” kilisema chanzo hicho.
Habari zinasema, polisi waliweza kubaini kuwa magari hayo baadhi yake yalibadilishwa rangi na kupakwa nyeusi huku namba za usajili nazo zikiwa zimebadilishwa.

Nyumba anayoishi kigogo huyo.
KAMATAKAMATA IKAANZA
Polisi baada ya kugundua wizi huo, kamanda aliyeendesha oparesheni hiyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, aliamuru Luhanga na mkewe wakamatwe na magari yaliyokuwa na uwezo wa kutembea yaliendeshwa, mengine yalikokotwa kwa ‘breakdown’ hadi Kituo cha Polisi Kawe.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa watuhumiwa hao tayari wamefunguliwa jalada katika kituo hicho kwa namba KW/RB/8194/2013 WIZI WA MAGARI.
Waandishi wetu walipofika kituoni Kawe Jumapili iliyopita, walikuta ndugu sita wa Luhanga wakihaha kutaka kuwawekea dhamana.

MAGARI YALIYOIBWA
Magari yaliyoibwa ni aina ya Nissan Navara lenye thamani ya shilingi milioni 45, lililokutwa na kibao cha usajili namba T519 BNP.
Lingine ni Toyota Harrier, ambalo thamani yake ni shilingi milioni 30. Hili lilikutwa na namba za usajili T 924 AXB, wakati kuna Toyota Rav4 new model, lenye thamani ya shilingi milioni 40 ambalo lilikutwa na namba T 581 BBL.
Gari lingine ni Toyota Canter, vilevile kulikuwa na Rav4 new model nyingine lenye rangi ya kijivu, hili lilikuwa limeng’olewa namba zake halisi bila kuwekewa nyingine.
Rav4 hilo ambayo halikufungwa namba, imeelezwa lilikuwa halijabadilishwa rangi, kwani kwa kawaida yale yanayoporwa na kuingizwa kiwandani humo, hupakwa rangi nyeusi.

OFISINI KWA KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, ACP Camillius Wambura, hakuweza kupatikana licha ya waandishi kufika ofisini kwake. Hata hivyo, ofisa mmoja mwandamizi wa jeshi hilo, alithibitisha kutokea kwa tukio.
“Tukio hilo lipo na tunaendelea na uchunguzi,” alisema ofisa huyo huku akiomba asiandikwe jina lake gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Monday, September 16, 2013

KWA NINI WASIUZE UNGA?

Na Gladness Mallya
IMEBAINIKA kwamba ukifuatilia ratiba za maisha ya anasa ya kila siku ya mastaa wa Kibongo, lazima utajiuliza kwa nini wasiuze au kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’? Ijumaa Wikienda lina ripoti ya kushangaza.
Masogange.
Uchunguzi wa gazeti hili uliopewa sapoti na baadhi ya mastaa hao, ulibaini kwamba suala la kupenda kujirusha kuliko kazi ndiyo chanzo cha kufanywa ‘punda’ wa kusafirisha unga na matokeo yake kunaswa na kuingia kwenye matatizo makubwa.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa kuna baadhi ya mastaa hao, ratiba zao za kujirusha na kula bata ndefu zimewabana kiasi cha kushindwa kuendeleza vipaji vyao katika sanaa.
Ratiba za baadhi ya mastaa hao za kujirusha ni kama ifuatavyo;
Odama.
JUMATANO
Ilibainika kuwa Jumatano, baadhi ya mastaa hao hupenda kwenda kujirusha kwenye kumbi za starehe hasa katika Klabu ya Bilicanas, Posta ambako mara nyingi kunakuwa na bendi inayomwaga burudani huku wakishushia na pombe.
Ilibainika kuwa mastaa hao huondoka kwenye kumbi hizo za starehe karibia kunakucha (majogoo) huku wakiwa ‘tilalila’ na kwenda kulala.
Aunt Lulu.
ALHAMISI
Data zilizopatika kwa kumsoma msanii mmoja baada ya mwingine zilibaini kwamba, kwa kuwa huchelewa kulala Jumatano huku wakiwa na uchovu, Alhamisi huamka saa 10:00 jioni kisha kuchati kidogo na marafiki kabla ya usiku kwenda kujirusha hasa New Maisha Club kunakokuwa na burudani ya bendi.
Ilibainika kwamba wakiwa humo hujiachia kwa ‘masebene’ na kugonga pombe kama ilivyokuwa jana yake hadi majogoo.
Baby Madaha.
IJUMAA
Uchunguzi ulibaini kuwa siku ya Ijumaa, baadhi ya mastaa hao huamka tena saa 10:00 jioni na kinachoonekana ni kati ya siku ‘bize’ kwa mambo ya starehe hivyo wanakuwa na mialiko mingi.
Ilibainika kuwa baadhi yao huhudhuria mialiko ya sherehe za harusi, send-off, kitchen party, birthday na nyinginezo kabla ya baadaye kumalizia kwa kwenda kwenye ‘live’ bendi.
Mara nyingi hupenda kuhudhuria kwenye shoo kama hizo katika Kumbi za Thai Village, Masaki, Nyumbani Lounge, Ada Estate, Kinondoni au Club 24, Mikocheni ambako huko nako hukesha hadi majogoo.
Melisa.
JUMAMOSI
Uchunguzi wetu ulibaini kwamba Jumamosi, baadhi ya mastaa hao huamka saa 10:00 jioni kama kawa kisha kunyoosha miguu hadi baa ambapo giza likiingia huzama tena kwenye burudani ya bendi.
Wengi hupatikana katika kumbi zinazoungurumisha muziki wa bendi za dansi. Huko nako huwa wanakula bata ndefu hadi majogoo kisha kurejea nyumbani kulala.
Jack Patrick.
JUMAPILI
Kama kawaida, baadhi ya mastaa hao huamka saa 10:00 jioni kisha kwenda kujipumzisha ufukweni hasa Coco na kuendelea kujirusha. Usiku mnene ‘hujimuvuzisha’ kwenye klabu za starehe ambapo ama msanii wa Bongo Fleva anazindua wimbo au kunakuwa na shoo ya kawaida ya muziki.
Kumbi za starehe zinazokuwa ‘bize’ na mastaa huku kukiwa na shoo usiku wa Jumapili ni pamoja na Bilicanas na New Maisha Club ambako huko nako huondoka majogoo kwenda kulala.

JUMATATU
Ilifahamika kuwa siku ya Jumatatu baadhi ya mastaa hao huamka saa 7:00 mchana kisha kwenda saluni na baadaye kufanya ‘window shopping’ katika maduka ya nguo, supermarket na sehemu nyingine.
Baada ya hapo muda wa jioni, baadhi ya mastaa hao hupendelea kwenda kuogelea (swimming) kisha kuibuka Coco Beach kupata mihogo ya kuchoma, mishikaki, ‘shisha’, pombe na starehe nyingine za kiutu uzima.

JUMANNE
Mara nyingi uchunguzi wetu ulibaini kuwa siku ya Jumanne hutumiwa na wasanii hao kupumzika kutokana na uchovu wa wiki nzima kabla ya ratiba kujirudiana tena kuanzia Jumatano.

WENYEWE WANASEMAJE?
Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya mastaa wachache wa kike kuhusu suala la kujirusha ambapo kila mmoja alifungukia ratiba yake.

BABY MADAHA
“Mimi naweza kujiachia kila siku lakini mara nyingi natoka siku tano na ratiba zinaendelea kama kawa maana huwa nalala mchana na nikitoka narudi saa 9:00 usiku.”

MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
“Siku hizi natoka mara mojamoja siyo kama zamani lakini nikiwa na kampani huwa narudi kulala saa 10:00 usiku.”

TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
“Mimi huwa natoka kwenye ishu maalum tu.”
JACQUELINE PATRIC
“Naweza nisitoke wiki nzima lakini nikijisikia pia naweza kutoka wiki nzima na mambo mengine yanaendelea.”

WATOTO WA MBWA (TIKO, MARY & THEKLA)
“Siku hizi huwa tunatoka siku maalum, siyo kama zamani.”

YOBNESH YUSUF ‘BATULI’
“Inategemea, kama nimealikwa sehemu narudi saa 10:00 usiku au asubuhi maana kazi zetu siyo za kila siku.”

LULU MATHIAS  ‘AUNTY LULU’
“Huwa natoka siku ya Ijumaa narudi saa 8:00 usiku naamka 4:00 asubuhi. Pia natoka Jumapili kwa sababu Jumatatu nakuwa off.”

KWA NINI WASIUZE UNGA?
Uchambuzi wa kina ulibaini kuwa mbali na starehe hizo, pia kuna masuala ya mapenzi ambayo nayo huwa ni gharama na pia hutumia muda wao mwingi.
Ilibumburuka kuwa kwa staili hiyo ya maisha ya anasa huku baadhi wakisahau kwenda studio kurekodi na mazoezi ya shoo (kwa wanamuziki) na kutoonekana lokesheni wakishuti filamu.
Ilifahamika kwamba kwa ratiba hizo, anapotokea kigogo (mfanyabiashara wa madawa ya kulevya) na ‘kumsomesha’ msanii kuwa kuna dili la unga lazima akubali kuwa punda ili apate fedha za harakaharaka za kutanulia asiachwe na watoto wa mjini.
Listi inazidi kuongezeka kila kukicha ya mastaa mbalimbali ambao wanadaiwa kunaswa na unga wakiwemo Agness Gelard ‘Masogange’ na shosti yake, Mellisa Edward, Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’, Saadah Ally, Aisha Bui, Mkwanda na Mbwana Matumla, Joseph Kaniki na wengineo.

CREDIT:Global Publishers
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Friday, September 13, 2013

MZEE GURUMO AKIRI KUFUMANIWA NA MKE WA MTU

Stori: Brighton Masalu
SIKU chache baada ya kustaafu muziki, mwanamuziki mkongwe nchini, Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo’ amekiri kupitia maisha mabaya ujanani ikiwemo kufumaniwa na mke wa mtu pamoja na uvutaji wa ‘sigara kubwa’ Ijumaa linaanika.
Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo’.
Akizungumza katika mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Runinga ya East Africa chini ya Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa mambo mabaya ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.
KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo, Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye aligoma kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ‘wakiponda kirauli’ ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia kuwa anayegonga mlango ni mumewe.
“Niliogopa sana, ikabidi nijibanze nyuma ya mlango, alipoingia tu nikatimua mbio kali sana, lakini hakujua kama ni mimi,” alisema Gurumo.
Kuhusu uvutaji wa bangi, Gurumo alikiri kuwahi kuonja kilevi hicho ujanani mwake ambapo alibainisha kuwa alishawishiwa na mwimbaji mwenzake maarufu sana kwa wakati huo.
Alisema siku ambayo alivuta sigara kubwa, alipofika nyumbani baada ya kutengewa chakula, alimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa akidhani ni mchuzi.
“Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu, nilivuta kutokana na ushawishi, baada ya kufika nyumbani, wakati wa chakula nilimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa, nikasema mbona mchuzi hauna ladha nzuri, lakini baadaye nilijutia sana,” alisema Gurumo na kuongeza:
“Nimepitia maisha ambayo si mazuri sana ujanani, lakini yote hayo ni mapito na imebaki kama historia tu kwangu, namuomba Mungu anisamehe kwa hayo,” alisema Gurumo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

FALLING IN LOVE NDIO HABARI YA MUJINI KWA SASA GET UR COPY NOW

HATIMAYE:Kile Kitabu kilichokuwa kinasubiriwa na wengi,SASA KIKO MTAANI...
Falling In Love....YOU CANT MISS THIS BOOK
PATA NAKALA YAKO Kwa Shilingi 10,000 tu kwa kuingia Hapa,
www.sethuniversity.com


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MMH CHOZI LA STEVE NYERERE LINA...

Stori: Shakoor Jongo
KIFO cha aliyekuwa msanii wa Bongo Movies, Zuhura Maftah ‘Malisa’ kimeacha simanzi kwa wengi lakini kwa mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ni zaidi kwani alimwaga chozi lililoibua minong’ono kuwa lina kitu cha ziada nyuma yake, Ijumaa lina tukio kamili.
Malisa alifariki dunia katika Hospitali ya Hindu Mandal, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kulazwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye ubongo ambapo Jumanne iliyopita aliagwa nyumbani kwao Mikocheni kisha kwenda kupumzishwa katika nyumba ya milele kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.
Katika msiba huo, mwili wa Malisa ulipowasili  Steve ambaye ana mke wake alianza kumwaga machozi huku akijitenga na wenzake.
Haukupita muda mrefu ambapo mwili wa Malisa ulipoanza kuagwa lakini Steve hakuonekana hadi alipotokea akiwa wa mwisho akisaidiwa na baunsa ili asidondoke.
Kadiri Steve alipolikaribia jeneza ndivyo alivyoongeza spidi ya kilio  na akalikumbatia jeneza lililobeba mwili wa marehemu.
Baadaye aliingiza mikono kwenye jeneza kisha akashika mwili wa Malisa akakiinua kichwa na kumbusu marehemu mdomoni kwa dakika kadhaa.

Steve aliendelea kuling’ang’ania jeneza hilo huku akilia, jambo lililoibua minong’ono mingi kuwa machozi yake yalikuwa na kitu cha ziada nyuma yake kwa sababu ilikuwa ni zaidi ya kilio.
“Maskini Steve, anaonekana ameuamia kuliko mtu yeyote. Ukweli ni kwamba alimpenda sana marehemu. Kwa vyovyote machozi yake yana kitu cha ziada, siyo bure. Labda aamini kama Malisa hatunaye,” alisema mmoja wa wasanii wa Bongo Movies.Baada ya mwili kuagwa, safari ya kuelekea Makaburi ya Kinondoni ilianza ambapo Steve alishindwa kuendesha gari, hivyo akasaidiwa na rafiki yake.
Alipofikishwa makaburini, wakati wa zoezi la kurudishia udongo kaburini, Steve alishindwa tena kujizuia, aliendelea kumwaga machozi huku akizungumza vitu visivyoeleweka zaidi ya kusikika maneno ‘wasanii wa Bongo Movie’.Hata hivyo, gazeti hili lilipotaka kujua kulikoni akamwaga chozi kiasi hicho, Steven hakuwa na ‘mudi’ ya kuzungumza chochote.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Steve na Malisa walikuwa watu wa karibu, hivyo inawezekana ndiyo sababu ya mwigizaji huyo kumwaga machozi kuliko wengine na kufuatiwa na Yvone-Chery Ngatwika ‘Monalisa’ na waigizaji wengine.
Kwa upande wa filamu, kabla ya mauti, Malisa alionekana kwenye Filamu ya Big Dady ya marehemu Steven Kanumba ambaye naye alizikwa kwenye makaburi hayo ya Kinondoni.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."