Social Icons

Tuesday, November 27, 2012

Taarifa Kamili Baada ya Ajali aliyopata Marehemu Sharo Millionea

Usiku wa jana ni ulikuwa usiku wa majonzi kwa watanzania wote hasa kwa waliokuwa mashabiki wakubwa wa msanii na mchekeshaji maarufu nchini Sharo Milionea,ambae amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kueleka wilayani Muheza, Tanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe Hussein Ramadhani (Sharo Milionea) alikuwa akiendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier. Alipofika maeneo ya Segera gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa, likagonga mti na kusababisha kifo chake na yeye kutokea mbele ya kioo cha gari na kutupwa mbali.
Alisema Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza. Aliongeza kuwa hakuna kona kali wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali. Gari lake imehifadhiwa mahali salama kwakuwa limeharibika vibaya na kwamba kwenye gari alikuwa mwenyewe.


Habari kuhusu kuthibitika kwa kifo chake zilianza kuenea jana usiku ambapo kwa upande wa rafiki yake wa karibu Kitale amesema alikuwa akiipiga simu ya Sharo Milionea iliyokuwa ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa na kisha kupigiwa simu na Tundaman, Mzee Majuto na Mjomba wake Sharo kumtaarifu juu ya kifo hicho.
Naye Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Bwana Simon Mwakifwamba alisema kwamba  “Sisi binadamu tunaweza kuwaza hivi na Mungu naye akawaza lake kwahiyo sisi tunaziombea familia hizi Mungu azipe faraja ya kweli na nadhani inatoka kwa Mungu,” alisema hayo kwenye kituo cha televisheni ya TBC.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wamesema kuwa  kifo cha Sharo Milionea kimetokea wakati ambao alikuwa ameanza kufanikiwa. “Sharo umri wake na mambo aliyoanza kuyafanya ni makubwa. “Sharo alishaanza kupata matumaini yaani ni sawasawa unatupa mbegu halafu uitegemee inaanza kuchepua. Sharo alishaanza kuchepua, anachepua ile mbegu yake, ameanza kujisaidia yeye kama yeye sababu katika maisha lazima kwanza uanze kujisaidia wewe kama wewe halafu pili uingalie jamii inahitaji nini kwako. Amejipatia usafiri maskini ya Mungu, pa kulala, na maisha yote ya kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga kuwaona wazazi kutumia gharama yake.”Maneno hayo yalisemwa na Bwana Steve Nyerere,na pia aliongeza na kusema kuwa Jmbo la msingi ni Kumwachia Mungu na kuondoa mawazo kuhusiana na kifo chake.
Umoja wa wasanii wa filamu nchini umesema umepata pigo kubwa sana hasa kwakuwa bado wana msiba wa msanii mwingine wa filamu, Marehemu John Stephano ambaye anatarajia kuzikwa leo. Wamesema baada ya mazishi hayo kesho wanatarajia kusafiri na mabasi mawili kuelekea wilayani Muheza kwaajili ya mazishi ya marehemu Hussein Ramandhani(Sharo Millionea).
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Friday, November 23, 2012

‘MAPOUDA’, WANJA WA DIAMOND MH!

Na Imelda Mtema
PICHA zilizosambaa mtandaoni zikimuonesha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipaka wanja na ‘mapouda’ zimewashanganza wengi huku baadhi wakisema anakoelekea siko.Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipaka wanja. Wakizungumza na Ijumaa, baadhi ya watu waliyoziona picha hizo walisema kuwa, ni kweli kuna suala la kujiweka ‘sopsop’ kwa staa ili aonekane nadhifu lakini hilo la kufikia kupaka wanja na ‘mapouda’ kama mademu halileti picha nzuri.
“Unajua watu wanaweza kufikiria tofauti kwa picha hizi, mwanaume na poda au wanja wapi na wapi?
Ni sawa, yeye ni rais wa masharobaro lakini sidhani kama usharobaro ni lazima upake wanja, mimi hizi picha zimenishtua sana,” alisema Halima wa Kinondoni jijini Dar.
Diamond Platnumz akipaka poda.
Naye Juma Salum wa Mwenge jijini Dar alisema ukiona watu wanafikia hatua ya kuitwa wanaume kama mabinti ni kwa matukio kama haya kwani imezoeleka wanaojiremba hivyo ni wanawake na si wanaume.
Katika kufuatilia zaidi, mwandishi wetu alibaini kuwa picha hizo Diamond alizipiga alipokuwa akishuti video ya wimbo alioshirikishwa na mwanadada Keisha. Diamond alipotafutwa ili kuzungumzia ishu hiyo, hakuweza kupatikana mara moja.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."