PICHA zilizosambaa mtandaoni zikimuonesha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipaka wanja na ‘mapouda’ zimewashanganza wengi huku baadhi wakisema anakoelekea siko.Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipaka wanja. Wakizungumza na Ijumaa, baadhi ya watu waliyoziona picha hizo walisema kuwa, ni kweli kuna suala la kujiweka ‘sopsop’ kwa staa ili aonekane nadhifu lakini hilo la kufikia kupaka wanja na ‘mapouda’ kama mademu halileti picha nzuri.
“Unajua watu wanaweza kufikiria tofauti kwa picha hizi, mwanaume na poda au wanja wapi na wapi?
Ni sawa, yeye ni rais wa masharobaro lakini sidhani kama usharobaro ni lazima upake wanja, mimi hizi picha zimenishtua sana,” alisema Halima wa Kinondoni jijini Dar.
Naye Juma Salum wa Mwenge jijini Dar alisema ukiona watu wanafikia hatua ya kuitwa wanaume kama mabinti ni kwa matukio kama haya kwani imezoeleka wanaojiremba hivyo ni wanawake na si wanaume.
Katika kufuatilia zaidi, mwandishi wetu alibaini kuwa picha hizo Diamond alizipiga alipokuwa akishuti video ya wimbo alioshirikishwa na mwanadada Keisha. Diamond alipotafutwa ili kuzungumzia ishu hiyo, hakuweza kupatikana mara moja.
No comments:
Post a Comment