Hina ya bibi harusi Michoro ya hina ya bibi harusi huwa na maua makubwa na yaliyojaa tofauti na mingine. Si hivyo tu michoro hiyo huchukua sehemu kubwa ya maungo. Kwa mfano ikiwa ni mikononi, basi hupakwa hadi kwenye viwiko au kuanzia chini hadi juu kabisa. Kwa upande wa miguu huanzia kwenye unyayo hadi karibu na magoti. Wengine huchora hadi kifuani na sehemu ya juu ya mgongo karibu na shingo. Ili kuleta ladha zaidi, hina ya bibi harusi huongezwa nakshi zaidi kwa kunakshiwa na piko hasa kwa wale wenye ngozi nyeusi.
Kwani kwa wenye ngosi nyeupe inatosha kuchora kwa kutumia hina yenyewe. Hina kwa wanaume Wanaume huchora hina kama tattoo. Mara nyingi huchora sehemu ya juu kabisa ya mkono. Hina kwa wasichana Wasichana wengi wamekuwa wakichora hina katika mtindo tofauti na ule uliozoeleka. Wao wamekuwa wakichora katika eneo la kiuno kwa upande wa mbele au nyuma. Mara nyingi hupenda ionekane pindi wanapovaa top fupi. Kwa watoto Hina hutumiwa na watoto hususan wa kike katika sikukuu hasa za Kiislamu kama vile Eid, Maulid na nyingine.
Wao huchora maua mbalimbali ya kitoto na hivyo kuwafanya wapendeze zaidi. Watalaam wa urembo wanashauri watu wengi kutumia hina kwani ni njia ya asilia ambayo haina madhara kwa ngozi
No comments:
Post a Comment