Social Icons

Wednesday, May 30, 2012

Usafi wa nywele zako

 IKIWA utaosha nywele zako kama kawaida na baadaye kutumia chanuo ama brash katika kuzibana, wakati mwingine unaweza kusababisha kukatika au hata kuathiri ukuaji wa nywele zako.

 Hata hivyo, kwa kufuata ushauri unaweza kuepukana na tatizo hilo na hivyo kusababisha nywele zako kujaa na kukua vyema.  Fuata hizi dondoo rahisi ambazo ili kuhakikisha unasaidia sio kuua nywele zako bali kuzikuza na kuzifanya zinawiri. Ikiwa unatumia mafuta ya jeli, umakini unahitajika katika kuziosha nywele zako. Kama unatumia jeli ya nywele katika mtindo wako, hakikisha unaosha vizuri na kuondoa jeli yote kabla ya  kulala. Unapolala na jeli au urembo mwingine unaofanana nayo, unasababisha kuziba kwa tundu za nywele katika ngozi ya kichwa.

 Kitendo hicho mbali na kuzuia kupumua kwa ngozi ya kichwa pia huchangia kuzuia nywele chipukizi kuota katika ngozi ya kichwa. Kuwa makini na shampoo za madukani Mara nyingi baadhi ya watengenezaji wa vipodozi huweka maslahi mbele bila kuangalia athari zinazoweza kuwapata watumiaji wa bidhaa zao. Kwani kuna baadhi ya shampoo huwa na kemikali hatari kwa ngozi. Hivyo ni vyema zaidi ikiwa utakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na aina hiyo ya kipodozi. Pendelea zaidi kutumia herbal shampoo.

 Si hivyo tu wakati mwingine vipodozi vya bei rahisi huwa na kasoro, hivyo ni vyema kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa nywele kujua ni aina gani ya shampoo ni sahihi kwa nywele zako. Kinyume cha hapo unaweza kuishia kuathiri nywele na ngozi yako bila ya mwenyewe kufahamu. Epuka kubana nywele mara kwa mara Ubanaji wa nywele hasa kuelekea mgongoni mara nyingi huhatarisha maisha ya nywele zako hasa za usoni. Kwani kiteno cha kuzibana husababisha kuvutwa kwa nywele na hivyo kusabisha kukatika hasa kwa zile zilizo hafifu.

 Usichane nywele zikiwa mbichi Zinapokuwa mbichi nywele huwa na uwezekano mkubwa wa kukatika hasa pale zinapochanwa au kufutwa kwa taulo gumu. Ni vyema ukaacha zikauke kwa upepo na baada ya hapo unaweza kuzichana. Katika hili kama utakuwa unatumia ‘conditioner’hakikisha husugui katika nywele na badala yake tumia kwa kupaka. Ikiwa kama nywele zako zimekatika na hazilingani, ni vyema ukakata ncha ili kuzisawazisha. Hii husaidia kuzifanya zikue vizuri na pia kuondoa uwezekano wa kukatika mara zinapoingia maji.

Hasa kwa zile zenye ‘relaxer’.   Chochea ukuaji wa nywele zako kwa kuzichana Unapochana nywele zako hakikisha unatumia shanuo la mbao au kitana chenye meno yaliyoachana. Hakikisha nywele zako zinakuwa kavu. Usizivute sana kwani pamoja kusababisha maumivu pia huleta uwezekano wa kukatika.

 Jambo la muhimu katika uchanaji wa nywele, husaidia kuchochea mzunguko wa damu katika ngozi ya kichwa na pia husaidia kukua kwa nywele. Imarisha umaridadi wa nywele zako IKIWA utaosha nywele zako kama kawaida na baadaye kutumia chanuo ama brash katika kuzibana, wakati mwingine unaweza kusababisha kukatika au hata kuathiri ukuaji wa nywele zako

. Hata hivyo, kwa kufuata ushauri unaweza kuepukana na tatizo hilo na hivyo kusababisha nywele zako kujaa na kukua vyema.  Fuata hizi dondoo rahisi ambazo ili kuhakikisha unasaidia sio kuua nywele zako bali kuzikuza na kuzifanya zinawiri. Ikiwa unatumia mafuta ya jeli, umakini unahitajika katika kuziosha nywele zako. Kama unatumia jeli ya nywele katika mtindo wako, hakikisha unaosha vizuri na kuondoa jeli yote kabla ya  kulala. Unapolala na jeli au urembo mwingine unaofanana nayo, unasababisha kuziba kwa tundu za nywele katika ngozi ya kichwa.

 Kitendo hicho mbali na kuzuia kupumua kwa ngozi ya kichwa pia huchangia kuzuia nywele chipukizi kuota katika ngozi ya kichwa. Kuwa makini na shampoo za madukani Mara nyingi baadhi ya watengenezaji wa vipodozi huweka maslahi mbele bila kuangalia athari zinazoweza kuwapata watumiaji wa bidhaa zao. Kwani kuna baadhi ya shampoo huwa na kemikali hatari kwa ngozi. Hivyo ni vyema zaidi ikiwa utakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na aina hiyo ya kipodozi. Pendelea zaidi kutumia herbal shampoo. Si hivyo tu wakati mwingine vipodozi vya bei rahisi huwa na kasoro, hivyo ni vyema kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa nywele kujua ni aina gani ya shampoo ni sahihi kwa nywele zako. Kinyume cha hapo unaweza kuishia kuathiri nywele na ngozi yako bila ya mwenyewe kufahamu. Epuka kubana nywele mara kwa mara Ubanaji wa nywele hasa kuelekea mgongoni mara nyingi huhatarisha maisha ya nywele zako hasa za usoni.

 Kwani kiteno cha kuzibana husababisha kuvutwa kwa nywele na hivyo kusabisha kukatika hasa kwa zile zilizo hafifu. Usichane nywele zikiwa mbichi Zinapokuwa mbichi nywele huwa na uwezekano mkubwa wa kukatika hasa pale zinapochanwa au kufutwa kwa taulo gumu. Ni vyema ukaacha zikauke kwa upepo na baada ya hapo unaweza kuzichana. Katika hili kama utakuwa unatumia ‘conditioner’hakikisha husugui katika nywele na badala yake tumia kwa kupaka. Ikiwa kama nywele zako zimekatika na hazilingani, ni vyema ukakata ncha ili kuzisawazisha. Hii husaidia kuzifanya zikue vizuri na pia kuondoa uwezekano wa kukatika mara zinapoingia maji. Hasa kwa zile zenye ‘relaxer’.   Chochea ukuaji wa nywele zako kwa kuzichana Unapochana nywele zako hakikisha unatumia shanuo la mbao au kitana chenye meno yaliyoachana.

 Hakikisha nywele zako zinakuwa kavu. Usizivute sana kwani pamoja kusababisha maumivu pia huleta uwezekano wa kukatika.  Jambo la muhimu katika uchanaji wa nywele, husaidia kuchochea mzunguko wa damu katika ngozi ya kichwa na pia husaidia kukua kwa nywele
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."