Social Icons

Featured Posts

Friday, September 2, 2016

MTN yawatema mastaa wa Nigeria kuwa mabalozi wa mtandao huo

Mtandao wa simu wa MTN umewamwaga wasanii wakubwa wa Nigeria akiwemo Don Jazzy, Tiwa Savage, Davido kuwa mabalozi wa mtandao huo na kutangaza majina ya wasanii wengine watakaoshika nafasi hizo.
mtn_building
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao huo kwa vyombo vya habari imetangaza majina ya wasanii wapya ambao watakuwa mabalozi wa mtandao huo kwa mwaka 2016/17.
“Music ambassadors for 2016-2017 are: Praiz (Praise Adejo), Iyanya (Iyanya Mbuk), Chidinma(Chidinma Ekile), Falz (Folarin Falana), Tekno Miles (Augustine Kelechi), Skales (Raoul Njeng-Njeng), Saka, (Hafiz Oyetoro), Nedu (Steve Onu), Osuofia (NkemOwoh),” imesema taarifa hiyo.
Naye Mkurugenzi wa mtandao huo nchini humo, Amina Oyagbola amesema, “MTN remains proud to be associated with the growth and development of the careers of all our ambassadors, past and present.”
“We specially thank all our former ambassadors for their immense contributions to building our brand and also making us the network of choice in Nigeria,” ameongeza.
“We will definitely continue to maintain the strong and mutually beneficial relationship with them through the monetisation of their content on all our digital platforms – MTN Music+, CRBT and VAS.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Kanye West atoa viatu vya Yeezy kwaajili ya watoto

Kanye West ameonyesha bidhaa yake mpya ya viatu vyake vya Yeezy kwa watoto kupitia kwa mwanae Saint West.

Saint West
Mtoto wa Kanye West, Saint West akiwa amevaa viatu vya brand ya Yeezy
Viatu hivyo vinapatikana kwa watoto kuanzia miezi 8 na kuendelea kwa kiasi cha $130 kwa pea moja.
Siku chache zilizopita rapper huyo alifungua maduka 21 ya muda kwenye nchi tofauti ambayo yaliuza bidhaa zake huku moja kati ya maduka hayo lilikuwa nchini Afrika Kusini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

FOUNDER WA FACEBOOK MARK ZUCKERBERG AENDA KENYA KUJIFUNZA KUHUSU MOBILE MONEY.

Founder/CEO was Facebook, Mark Zuckerberg anasafiri kimya kimya na sass yup Kenya kwa ajilI ya kujifunza kuhusu mobile money.
I dado kubwa sana ya watu Kenya wanatumia Internet kupitia simuzap na anampango wa kuwa-connect zaidi watu.
Mark Zuckerberg ::“Just landed in Nairobi! I’m here to meet withentrepreneurs and developers, and to learn about mobile money – where Kenya is the world leader,” 
 Mark Zuckerberg akila ugali na Samaki akiwa na serikali ya Kenya.


Mark Zuckerberg akitalii akiwa Kenya.


Kwa information zaidi soma Forbes Africa 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Sunday, March 20, 2016

New audio: Lady Jaydee - Ndi Ndi Ndi

Download Hapa wimbo Mpya wa Lady jaydee http://bit.ly/NdiNdiNdi

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

HIVI NDIVYO MWANAMKE MJASILIAMALI KUTOKA TANZANIA SANDRA BENARD ALIVYOSHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KIAINA YAKE.

Sandra bernard (sondy bernard kalumanga) kama wengi wanavyomfahamu ni kati ya wanawake wajasiliamali na wanaojituma tanzania.

Siku yake ya kuzaliwa tarehe 10 March  aliamua kuisherekea kipekee kbs pamoja na rafiki zake kwa kuwakumbuka watoto hawa kwenye kituo chao wanacholelewa,

Kiukweli ameonesha mfano mkubwa sana maana licha ya kuwa na majukumu mengi ila siku hii aliifanya ya kipekee kushirikiana na watoto hawa

Mungu azidi kumbariki

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Tuesday, September 2, 2014

HIVI NDIVYO MUUNGANO ‘UNAVYOZITESA’ SERIKALI

NIanze kwa kumuomba Mungu atuzidishie maarifa ili tuwe na afya na upendo miongoni mwa Watanzania ili taifa letu lizidi kustawi na kila mtu apate neema na ustawi wa Mungu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Baada ya kusema hayo niseme wazi tu kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni suala ambalo limekuwa likiitesa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar (SMZ) kwa miaka mingi na kuzisababishia kuingia hasara kwa kuunda kamati au tume mbalimbali kushughulikia kero za muungano huo kwa gharama kubwa.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejikuta ikiingia katika mkondo wa kuunda tume na kamati nyingi zaidi kuliko Serikali ya Muungano kushughulikia jambo hilo. Serikali zote zinapounda kamati au tume juu ya mambo mbalimbali ya kiserikali, suala la muungano ‘huchomekwa’ viongozi wake wanapokutana na wananchi.
Suala hilo limekuwa likiibuka katika mijadala mikubwa ya kikatiba na kisiasa nchini, kwa upande mwingine katika uendeshaji wa shughuli za serikali za kila siku na matatizo na vikwazo kadhaa ya kiutawala na kiutendaji, vimekuwa vikiripotiwa kila mara kwamba vinakwamisha uimarishaji wa Muungano.
Tume na kamati kadhaa zimeundwa kuainisha matatizo ya Muungano na kupendekeza njia za kuyatatua. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda tume na kamati ambazo pamoja na mambo mengine, zilijikita pia kuzungumzia na kuandika ripoti kuhusu suala la muungano.
Baadhi ya kamati hizo ni Kamati ya Mtei, Tume ya Jaji Francis Nyalali  mwaka 1991, Kamati ya William Shellukindo ya mwaka 1994, Kamati ya Shellukindo ya pili ya kuandaa muafaka juu ya Mambo ya Muungano baina ya SMZ na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Jaji Mark Bomani ya mwaka 1995, Kamati ya Jaji Robert Kisanga ya mwaka 1998 na kadhalika.
Nayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ‘imeteseka’ zaidi kwani imetia fora kwa kuunda kamati ambazo zimejadili kero za muungano bila mafanikio.
Kamati ilizounda ni  Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) (1992), Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamati ya Shamuhuna) (1997), Kamati ya Rais Kuchambua Ripoti ya Jaji Kisanga (Kamati ya Salim Juma Othman), Kamati ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Juu ya Kero za Muungano (Kamati ya Ramia) (2000).
SMZ iliunda pia  Kamati ya Baraza la Mapinduzi Juu ya Sera ya Mambo ya Nje, Kamati ya Rais ya Wataalamu Juu ya Kero za Muungano (2001), Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kamati ya Mafuta, Kamati ya Madeni Baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ), Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu, Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu (1996 –1999), Kamati ya Baraza la Mapinduzi Juu ya Matatizo na Kero za Muungano na Taratibu za Kuyaondoa (2004).
Ukiacha tume, kamati na ripoti hizo, kuanzia mwaka 1985 kulianzishwa utaratibu wa Kamati ya Pamoja ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi wa Zanzibar pamoja na Mawaziri wa Serikali zote mbili ambayo ilitarajiwa iwe ndiyo jukwaa la kuzungumzia matatizo kutoka kwa washiriki wakuu wa muungano huu na kuyapatia ufumbuzi unaofaa, lakini nayo iligonga mwamba.
Utaratibu huu uliachwa kwa muda mrefu lakini sasa umerejeshwa upya kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa katika mkutano na mawaziri na watendaji wakuu wa serikali yake huko Ngurdoto, Arusha Februari, 2006.
Mikutano hiyo sasa imebadilishwa utaratibu wake na inaongozwa na kusimamiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na timu za pande mbili zikiongozwa na Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mikutano, makongamano, semina zimefanywa kujadili masuala ya muungano na kupendekeza hatua za kuchukuliwa lakini bado kuna malalamiko na ndiyo maana nasema serikali hizo zimeteseka sana na suala la muungano wa nchi zetu mbili hizi.
Ndugu zangu siyo siri, wasomi mbalimbali wameona kuna kasoro katika muungano wetu na kupendekeza kuboreshwa lakini jambo hili limekuwa kama donda ndugu maana hata Bunge Maalum la Katiba limevurugika kwa baadhi ya wajumbe kususa na wengine wamo ndani lakini suala la Muungano likiibuka kutoka nje ya vikao.
Hii maana yake ni kwamba bila kuwa na mikakati inayokubalika na watu wa pande zote mbili za muungano, suala hili litakuwa kama jini ambaye hakamatiki, viongozi wa serikali walione hili.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MJANE ALIPULIWA KWA PETROLI

Stori: Haruni Sanchawa  na Makongoro Oging’
MAMA mmoja mjane, Mwajuma Hamisi Lissu (42) ameteketea kwa moto baada ya nyumba aliyokuwa amelala eneo la Kibamba Hondogo A maarufu Miti Mirefu jijini Dar es Salaam, kulipuliwa kwa petroli usiku wa  Agosti 24, mwaka  huu.
Marehemu Mwajuma Hamisi Lissu Enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kusikitisha inadaiwa linahusishwa  na ugomvi baada ya mama  huyo kuachana na ulokole na  kujiunga tena katika dini yake ya zamani ya Kiislamu.Akisimulia mazingira ya tukio hilo, mtoto wa pili wa mama huyo ambaye hivi sasa ni marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Charity Jikole alikuwa na haya ya kusema:
Picha ikionyesha sehemu ya ndani ya nyumba ilivyoteketea kwa moto.
“Mama amelipuliwa na petroli. Baada ya moto huo kulipuka chumbani tulikuta nyavu za kwenye dirisha la chumba alicholala zimekatwa, tunaamini mlipuaji ndiye aliyekata nyavu hizo na kupitishia petroli.
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.
Mtoto wa Marehemu, Charity Jikole.
“Mkasa huu unatokana na ukweli kuwa mama yangu awali alikuwa Muislamu lakini kutokana na matatizo yake ya kiafya alishauriwa na baadhi ya watu kujiunga na maombi katika makanisa ya kilokole ili awe anaombewa tatizo la presha.
“Baada ya kushauriwa aliamua kujiunga na makanisa hayo ya kilokole akiamini kuwa angeweza kupona.Waombolezaji wakishusha mwili wa marehemu kwenye gari kwa ajili ya mazishi.
“Mama alikuwa ni mjane mwenye watoto watatu na baada ya kujiunga na walokole amekuwa akisali katika makanisa manne tofauti.“Sisi kama familia tunawatuhumu walokole kwa  sababu hata baada ya moto  huo, baadhi yao hawakuja kusaidia kuuzima wala kutoa maji.
Nyumba ya marehemu inayodaiwa kuteketea kwa moto eneo la Kibamba Hondogo
“Kwa kweli tulishangazwa na kitendo hicho na kuwaona ni watu wabaya sana kwetu.”
Hata hivyo, mtoto huyo alisema kifo cha mama yake kimekuja siku moja baada ya kufanyiwa sherehe ya kutoka katika dini ya kilokole na kurudi kwenye Uislamu.
Mchungaji aliyetajwa kwa jina la George Said ambaye anawaongoza walokole wa eneo hilo, alipohojiwa na waandishi wetu alikiri kusikia tuhuma hizo.“Hata mimi nimesikia tuhuma hizo lakini si za kweli hata kidogo na mpaka sasa sijahojiwa na mtu yeyote au hata polisi kuhusiana na tatizo hilo,” alisema  mchungaji huyo.
Uwazi lilipompigia simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP, Camillus Wambura na kumuuliza juu ya tukio hilo, alikiri kutokea na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo chake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

best videos

Loading...
 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."