Social Icons

Thursday, July 26, 2012

JACK PATRICK ADAIWA KUMTOSA MUMEWE

                                                                Jacqueline Patrick.


Abdullatif Fundikira.
Mwanamitindo Jacqueline Patrick ambaye pia ni Miss Ilala no.3, 2005 anadaiwa kumtelekeza mumewe Abdullatif Fundikira aliyepo mahabusu katika Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam kwa madai ya kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Akizungumza na Amani, rafiki wa karibu na mwanamitindo huyo alisema kuwa wenzake wanamshangaa Jack kwa kitendo cha kumtosa mumewe wakati anafahamu yupo katika matatizo makubwa.
“Kiukweli anachofanya Jack si uungwana kabisa, we fikiria tangu mumewe akamatwe (Mei mwaka huu), hajawahi kwenda mahabusu kumtembelea au hata siku ya mahakamani kuhudhuria kusikiliza kesi yake inavyoendelea, yeye na starehe, starehe na yeye,” alisema shostito huyo akiomba kuhifadhiwa kwa jina lake.
Akiendelea kuzungumza, rafiki huyo alisema kuwa kitu kingine ambacho anaamini kuwa ndoa ya Jack ni ndoano ni kitendo cha kuondoka nyumbani kwake na kutimkia nje ya nchi bila mumewe kuwa na taarifa.
“Yaani huyu mwanamke ni wa ajabu sana, hivi ninavyokwambia yupo nje ya nchi huku mumewe akiwa anateseka mahabusu, mbaya zaidi mume hajui,” alisema.
Baada ya kusikia kauli hiyo, Amani lilianza kumsaka Jack kupitia simu yake ya mkononi ambapo muda wote ilionekana haipo hewani lakini kupitia udodosi wa paparazi wetu, lilimnasa staa huyo juu kwa juu kupitia mtandao wa What’s Up ambapo mahojiano yalikuwa hivi:
Shakoor: Jack ningependa kufahamu upo wapi kwa sasa maana nakutafuta kwenye simu yako ya mkononi sikupati?
Jack: Shida yako nini? Sihitaji stori wala promo ya aina yoyote kutoka kwenu.
Shakoor: Mbona umefika mbali? Hata ninachotaka kukwambia hujakisikia unaanza kuwa mkali.
Jack: Hapa hatuchezi drama hicho ndicho ninachoongea, nipo bize na mambo yangu, naomba niache.
Hata hivyo, Jumatatu iliyopita, paparazi wetu mmoja alifunga safari hadi nyumbani kwa nyota huyo, Mbezi, Dar es Salaam ambapo watu waliokutwa ndani walisema Jack amesafiri kwenda ughaibuni bila kutaja jina la nchi aliyoenda.
Mtu wa karibu na Jack alipopatikana na kuulizwa alipo mwanandoa huyo, aliweka wazi kuwa yupo nchini Finland lakini hakusema amefuata nini huko.
“Mimi ninavyojua Jack yuko Finland, sasa lini atarudi au amefuata nini huko, sijui,” alisema.
Imeandikwa na: Shakoor Jongo na Musa Mateja.
 
 

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Saturday, July 14, 2012

Baada ya wezi kumvamia Wema Sepetu sasa aamua kumuiga mpenzi wake wa zamani Diamond kwa hili


                                                                       WEMA SEPETU
Pamoja na wajanja kuvamia nyumbani kwake kwa nia ya kumwibia vitu vyake vya thamani juzi kati na baadaye kushindwa kutimiza adhma yao, Wema Sepetu is here once again kuwa-prove wrong.
Kwa taarifa yako Diva huyu toka Bongo movies aitwaye Wema Abraham Sepetu baada ya ku-launch movie yake ya superstar kwa kumdondosha Omotola toka Nollywood industry ya Nigeria at Kempinski na baadaye kufanya family party pale Girafe Hotel, yuko tayari kuvunja bank kwa ajili ya kuagiza mkoko mpya aina ya Toyota Prado.
Gari hiyo aina ya Prado itakayo gharimu kiasi cha hela ya Tanzania million sitini mpaka kufika hapa na mambo mengine yote kama usafirishaji na gharama za ushuru wote husika, hiyo itakuwa inakamilisha gari yake ya tatu baada ya ile Mark X na Harrier.Ndiga hii anayotaka kununua Wema Sepetu ni kama ile ambayo mpenzi wake wa zamani,Diamond amenunua hivi karibuni.

 HII NDO PRADO YA DIAMOND AMBAYO WEMA ANATAKA KUNUNUA KAMA HIYO
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

NEW HIT:New video by Gosby July 2012 Named Erday

new video called ''EVERYDAY'', directed by Adam Juma, track produced by Maxi & Erasto Machine(Authentic studio's)
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

NEW HIT:(Official Music Video) Cindy Rulz ft. A.V.I.D song named "Redio". Enjoy...

Cindy comes with a single featuring A.v.i.d, Redio, produced by Lamar and the video was directed by Karabani
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."