Alisema… “Nitafanya tamasha la kuwashukuru Watanzania kote nchini, Kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimeanza kutembea mwenyewe sasa hivi nina miezi mitano, nilipofika India kama baada ya wiki mbili nilianza kutembea mwenyewe lakini ile kuwa na nguvu ni miezi kama mitatu au minne”
Aliugua kwa muda mrefu sana, watanzania wanajua aliugua kwa miezi kumi tu ila ukweli ni kwamba ameugua kwa miaka miwili kasoro, sio kwamba alikua anaficha ila alijaribu kujitibu mwenyewe na familia yake lakini mambo yalipokua magumu ndio akaamua kushirikisha watanzania wamchangie na kutoa msaada kumpeleka India.
Alifikia kipindi akakata tamaa ya maisha hasa kipindi cha mwisho alipokaribia kwenda India, namkariri akisema “nilikua nakata tamaa lakini vilevile nilimshukuru Mungu kwa sababu kuumwa kwetu sisi ni ibada kwa hiyo nilijiona kama niko kwenye ibada tu kwa sababu matatizo yapo kwa ajili ya sisi binadamu”
“Hali yangu bado haijakaa vizuri sana na nilipotoka India ndio kidogo hali yangu ilikua haiwi nzuri na tatizo kubwa lilikua ni damu inapungua sana na ndio ilikua inanisababishia matatizo”
Mwigizaji Sajuki amefariki dunia leo january 2 2012 katika Hospitali ya Muhimbili Dar es salaam huku tatizo kubwa likiwa ni upungufu wa damu, Mungu ampumzishe kwa amani.
No comments:
Post a Comment