Wema aliyasema hayo kwa paparazi wetu juzi baada ya kubanwa kuhusu madai kuwa ameolewa ambapo alisema hayupo katika ndoa na mwanaume yeyote yule kama watu wengine wanavyoamini.
Wema Sepetu.
Mahojiano kati ya Wema na paparazi wetu kwa njia ya simu yalikuwa kama ifuatavyo:Paparazi: Mambo vipi Wema?
Wema: (Kwa sauti ya ukali kidogo) Poa, nani wewe mwenzangu?
Paparazi: Mimi ni mwandishi wa Global Publishers hapa…
Wema: (Anashusha sauti) Ooo, unasemaje?
Paparazi: Nataka kujua kuhusu ndoa, maana nimesikia umeolewa, ni kweli?
Wema: (Kicheko) Jamani, watu wengine bwana. Mimi sijaolewa jamani, hayo maneno nimeyapuuza lakini ukweli sijaolewa, nipo singo.
Paparazi: Sasa unaposema hivyo kama mtu akijitokeza sasa hivi na kutaka kukuoa je?
Wema: (Anaacha kucheka) Sasa mimi si mwanamke jamani, lazima nitaolewa tu lakini kwa sasa sijaolewa na nataka watu wajue hivyo.
Hata hivyo, mlimbwende huyo hakuweza kusema ni kwa nini kumekuwepo na madai ya yeye kuolewa bali aliendelea kusisitiza kuwa amepuuza habari kwamba ameolewa na anaendelea kudunda ‘kitaani’ kama zamani.
Mbali na kuwepo kwa madai hayo, Wema amekuwa akidaiwa kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mmoja ambaye mpaka sasa hajawahi kuthubutu kufungua kinywa kumtaja kwa jina hata moja, achilia mbali kuelekeza mahali anakopatikana.
No comments:
Post a Comment