Social Icons

Tuesday, September 17, 2013

KISA NGONO, DENTI AMCHOMA KISU BABA YAKE

Stori: Richard Konga, Arusha
DENTI wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo (jina  tunalo) iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha, anadaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba yake mzazi Daudi Msemo baada ya kuonywa kuachana na tabia ya kuchanganya ngono na masomo, Uwazi limeambiwa.
Denti wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo anayedaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba yake mzazi Daudi Msemo.
Hayo yamesemwa na Fatuma Daudi ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi huyo mara baada kutokea tukio hilo la kusikitisha hivi karibuni nyumbani kwao Monduli ambapo denti alipofikishwa polisi alisema alifanya kitendo hicho kwa sababu baba yake alitaka kumbaka.
“Binti yetu huyu amekuwa akibadilika tabia na mara nyingi tumekuwa tukimuonya aache vitendo vya umalaya akiwa mwanafunzi lakini bado amekuwa akiendeleza tabia yake hiyo ambayo sisi wazazi tumeona ni kudharau maagizo yetu,” alisema Fatuna alipozungumza na gazeti hili.
Aliongeza kuwa, tabia hiyo ilikuwa ikimfanya mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kutorudi kabisa.
Mama huyo alisema, kutokana na tabia hiyo  waliamua kumdhibiti ili aache lakini matokeo yake alimchoma kisu baba yake na akamsingizia alitaka kumbaka hali iliyowalazimisha polisi kuwaweka ndani wote.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
Fatuma alikwenda mbali zaidi kwa kuwaomba baadhi ya wanajeshi ambao wana uhusiano wa kimapenzi na binti huyo waache kwa kuwa ni kinyume cha maadili na mwanaye bado ni mwanafunzi wa kidato cha nne.
Maelezo ya denti huyo yalimfanya baba mzazi kuahidi kujiua baada ya kutoka kituoni hapo akidai amedhalilishwa sana, hali iliyowafanya polisi kuamua kuendelea kumshikilia licha ya kwamba walishamruhusu kutoka baada ya mkewe kumtetea.
Afisa mmoja wa jeshi la polisi ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tunaendelea na uchunguzi na wote wawili, baba na mwanaye tunawashikilia ili kubaini chanzo cha kutokea kwa tukio hilo, baada ya uchunguzi maelezo zaidi utapewa na kamanda wa mkoa afande Liberatus Sabas, kwani ndiye msemaji wa jeshi mkoani hapa,” alisema afisa huyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."