Stori: Makongoro Oging’
AHADI ya Mchungaji Anthony Lusekelo au Mzee wa Upako katika msiba wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) Dk. Moses Kulola ya rambirambi ya shilingi milioni 15 imezua utata baada ya kiongozi huyo kutoitimiza, Uwazi limeambiwa.
Hata hivyo, utata unakuja kwani Mzee wa Upako mpaka Jumapili iliyopita fedha zake zilikuwa hazijafika kwa kamati husika inayoratibu rambirambi hizo.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba wachungaji na maaskofu walioahidi wameshatimiza ahadi zao ndani ya siku nne baada ya kuuaga mwili lakini kwa upande wa Mzee wa Upako bado hajatimiza ahadi yake.
Mzee wa Upako ndiye mchungaji pekee aliyewashinda wenzake kwa kutangaza dau kubwa la rambirambi kiasi cha shilingi 15,000,000.
Mweka Hazina wa Kanisa la EAGT kanda ya Dar es Salaam, Mchungaji Praygod Zawadi Mgonja ndiye aliteuliwa na uongozi wa kanisa hilo kuratibu, kupokea rambirambi na ndiye alikuwa akisimamia matumizi.
Gazeti hili liliwasiliana kwa njia ya simu ya kiganjani na Mchungaji Mgonja na kumuuliza kama ameshapokea mchango huo toka kwa mtumishi huyo wa Mungu ambapo alisema kwamba hajapokea na kudai kwamba huenda ameshapeleka mwenyewe kwa familia ya marehemu.
“Pamoja na kwamba ahadi hiyo kutonifikia huenda aliamua kupeleka kwa wana familia, jaribu kuwasiliana nao,”alisema Mchungaji Mgonja.
Mwandishi alimtafuta mtoto wa marehemu aitwaye Willy Kulola na alipoulizwa kama amepokea mchango wa rambirambi kutoka kwa Mzee wa Upako alisema familia haijapokea fedha hizo.
“Hatujapokea labda mumuulize Mchungaji Mgonja kwani ndiye aliteuliwa kuratibu mambo hayo,” alisema.
Mzee wa Upako alipoulizwa alikiri kuwa fedha hizo hajaziwasilisha kwa wahusika kwa madai kwamba hapendi kumpa Mchungaji Mgonja wala mtoto wa marehemu bali anataka kumkabidhi mke wa Askofu Kulola.
“Napenda taarifa hizi zimfikie
mke wa Mzee Kulola ili anifuate na nitampa rambirambi hiyo hata kama ni kesho akija nitamuandikia cheki,” alisema.
Alipoulizwa endapo anaweza kutoa fedha hizo kwa mtoto wa marehemu, alisema hawezi kumpa labda kama atakuwa amemsindikiza mama yake.
Gazeti hili lilimtafuta tena Willy na kumweleza kuhusu majibu ya Mzee wa Upako, lakini kijana huyo wa marehemu alisema hataweza kumpeleka mama yake kwa mchungaji huyo kwa sababu bado anapokea wageni wanaokuja kuhani msiba.
“Itakuwa jambo la ajabu kwa mfiwa kuanza kuzunguka huku na kule kufuatilia rambirambi, hiyo siyo kawaida kwa mjane kukusanya rambirambi kwani kanisa liliweka utaratibu,” alisema Willy.
Katika kuaga mwili wa marehemu, Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God Mikocheni B, Dk.Getrude Rwakatare alitangaza rambirambi zake kuwa angetoa shilingi milioni moja, akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Mchungaji Josephat Gwajima aliyeahidi kutoa shilingi milioni 10. Wote wametimiza ahadi zao.
Baadaye alikabidhiwa kipasa sauti Mzee wa Upako ambaye alitangaza kwamba hawezi kuzidiwa na Mchungaji Gwajima, hivyo aliahidi kutoa shilingi milioni 15.
Hata hivyo, baadhi ya wachungaji na maaskofu waliamua kufanya siri ahadi zao.
AHADI ya Mchungaji Anthony Lusekelo au Mzee wa Upako katika msiba wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) Dk. Moses Kulola ya rambirambi ya shilingi milioni 15 imezua utata baada ya kiongozi huyo kutoitimiza, Uwazi limeambiwa.
Mchungaji Anthony Lusekelo ' Mzee wa Upako'.
Ahadi hiyo alitolewa na Mzee wa Upako siku ya kuuaga mwili wa
kiongozi huyo Agosti 31, mwaka huu katika kiwanja cha Kanisa la EAGT,
Temeke ambapo viongozi kadhaa wa makanisa akiwemo Mchungaji Lusekelo
walitoa ahadi zao za rambirambi.Hata hivyo, utata unakuja kwani Mzee wa Upako mpaka Jumapili iliyopita fedha zake zilikuwa hazijafika kwa kamati husika inayoratibu rambirambi hizo.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba wachungaji na maaskofu walioahidi wameshatimiza ahadi zao ndani ya siku nne baada ya kuuaga mwili lakini kwa upande wa Mzee wa Upako bado hajatimiza ahadi yake.
Mzee wa Upako ndiye mchungaji pekee aliyewashinda wenzake kwa kutangaza dau kubwa la rambirambi kiasi cha shilingi 15,000,000.
Marehemu Dk. Moses Kulola enzi za uhai wake.
Askofu Kulola alifariki dunia Agosti 29, mwaka huu ambapo sasa ni zaidi ya mwezi mmoja na siku kadhaa.Mweka Hazina wa Kanisa la EAGT kanda ya Dar es Salaam, Mchungaji Praygod Zawadi Mgonja ndiye aliteuliwa na uongozi wa kanisa hilo kuratibu, kupokea rambirambi na ndiye alikuwa akisimamia matumizi.
Gazeti hili liliwasiliana kwa njia ya simu ya kiganjani na Mchungaji Mgonja na kumuuliza kama ameshapokea mchango huo toka kwa mtumishi huyo wa Mungu ambapo alisema kwamba hajapokea na kudai kwamba huenda ameshapeleka mwenyewe kwa familia ya marehemu.
“Pamoja na kwamba ahadi hiyo kutonifikia huenda aliamua kupeleka kwa wana familia, jaribu kuwasiliana nao,”alisema Mchungaji Mgonja.
Mwandishi alimtafuta mtoto wa marehemu aitwaye Willy Kulola na alipoulizwa kama amepokea mchango wa rambirambi kutoka kwa Mzee wa Upako alisema familia haijapokea fedha hizo.
“Hatujapokea labda mumuulize Mchungaji Mgonja kwani ndiye aliteuliwa kuratibu mambo hayo,” alisema.
Mzee wa Upako alipoulizwa alikiri kuwa fedha hizo hajaziwasilisha kwa wahusika kwa madai kwamba hapendi kumpa Mchungaji Mgonja wala mtoto wa marehemu bali anataka kumkabidhi mke wa Askofu Kulola.
“Napenda taarifa hizi zimfikie
mke wa Mzee Kulola ili anifuate na nitampa rambirambi hiyo hata kama ni kesho akija nitamuandikia cheki,” alisema.
Alipoulizwa endapo anaweza kutoa fedha hizo kwa mtoto wa marehemu, alisema hawezi kumpa labda kama atakuwa amemsindikiza mama yake.
Gazeti hili lilimtafuta tena Willy na kumweleza kuhusu majibu ya Mzee wa Upako, lakini kijana huyo wa marehemu alisema hataweza kumpeleka mama yake kwa mchungaji huyo kwa sababu bado anapokea wageni wanaokuja kuhani msiba.
“Itakuwa jambo la ajabu kwa mfiwa kuanza kuzunguka huku na kule kufuatilia rambirambi, hiyo siyo kawaida kwa mjane kukusanya rambirambi kwani kanisa liliweka utaratibu,” alisema Willy.
Katika kuaga mwili wa marehemu, Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God Mikocheni B, Dk.Getrude Rwakatare alitangaza rambirambi zake kuwa angetoa shilingi milioni moja, akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Mchungaji Josephat Gwajima aliyeahidi kutoa shilingi milioni 10. Wote wametimiza ahadi zao.
Baadaye alikabidhiwa kipasa sauti Mzee wa Upako ambaye alitangaza kwamba hawezi kuzidiwa na Mchungaji Gwajima, hivyo aliahidi kutoa shilingi milioni 15.
Hata hivyo, baadhi ya wachungaji na maaskofu waliamua kufanya siri ahadi zao.
No comments:
Post a Comment