Kutokana na habari zilizotufikia jana kwamba mwanalibeneke mwenzetu
kakamatwa na Polisi kufuatika sakata la ndugu Absalom Kibanda, leo hii
ndugu Mjengwa ameamua kufunguka na kuelezea mkasa mzima juu ya habari
hiyo kwa maeneno yake mwenyewe kama nilivyo nukuu hapa chini:
"Yaliyonikuta Jana Jumamosi" - Maggid Mjengwa
Ndugu zangu,
Kwanza
kabisa niwashukuru kwa dhati kabisa nyote mlionitumia salaam za
kunifariji kwa njia za simu, email, facebook, majukwaa ya Mabadiliko,
Wanabidii na JF.
Nimefarijika sana kutambua kuwa kuna wengi wenye kunifuatilia na kunijali.
Ndugu zangu,
Kama
alivyowataarifu kaka yangu Nyaroonyo Kichehere, ni kuwa, jana Jumamosi
nilikuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa tano asubuhi ya jana
mpaka saa tatu usiku. Ilihusu mahojiano ya Polisi na mimi kuhusiana na
sakata la ndugu yetu Absalom Kibanda.
Ukweli
sikukamatwa mahali popote, bali niliitwa na Kamishna ( Upelelezi)
Advocate Nyombi. Alhamisi nikiwa Iringa, tukakubaliana na kiungwana na
Kamishna Nyombi kuwa nifike Makao Makuu hayo ya polisi Jumamosi saa
tano. Ikawa hivyo.
Hapo
nilipokelewa na Kamishna Nyombi. Baada ya mazungumzo mafupi ndipo
akawaita maofisa wengine watano wa Upepelezi kufanya mahojiano nami.
Niliomba niwe na Mwanasheria, nikakubaliwa.
Nilimpigia
simu kaka yangu Nyaroonyo, naye, kwa vile ni Wakili pia wa Kibanda
akanisaidia kuhakikisha napata wakili mwingine. Pamoja na kuwa ilikuwa
ni Jumamosi, ndugu yangu Nyaroonyo Kichehere alifanya alivyoweza. Ndani
ya dakika 40 hivi alifika chumba nr 704 ghorofa ya saba akiwa na Wakili
Jacquiline Rweyongeza na Legal Officer Dickson Mbonde.
Nilimshukuru Kaka Nyaroonyo Kichehere. Na nilimuaga kwa kumwambia; “ Nenda ukaifahamishe jamii juu ya hiki kilichonitokea”.
Nachukua
fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati kabisa dada yangu Wakili Jacquiline
Rweyongeza na kaka Dickson Mbonde kwa kuacha yote ya Jumamosi na kuwa
tayari kuwa msaada kwangu. Jacquiline alimuacha nyumbani mtoto wake wa
miezi minne kwa ajili ya suala langu. Sina namna nyingine ya kumshukuru.
Na hakika, msaada wao niliuhitaji sana.
Nawashukuru
pia kwa dhati kabisa, ndugu zangu Saed Kubenea, Mbaraka Islam na
wengine wote waliokuwa na utayari wa kunisaidia pale msaada wao
ulipohitajika.
Kwa
ufupi, nimetoa maelezo yangu bila shuruti wala kutishwa. Na nimeweka
wazi kuwa yanaweza kutumika Mahakamani kama yatahitajika au hata kama
mimi nitahitajika, kwa namna yeyote ile.
Kesho saa mbili asubuhi nitaripoti Makao Makuu ya Polisi kupewa maelezo ya kitakachofuatia.
Kwa mara nyingine tena, nawashukuru sana kwa kuwa nami katika muda wote huu.
Maggid,
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment