IKIWA utaosha nywele zako kama kawaida na baadaye kutumia chanuo ama
brash katika kuzibana, wakati mwingine unaweza kusababisha kukatika au
hata kuathiri ukuaji wa nywele zako.
Hata hivyo, kwa kufuata ushauri unaweza kuepukana na tatizo hilo na
hivyo kusababisha nywele zako kujaa na kukua vyema. Fuata hizi dondoo
rahisi ambazo ili kuhakikisha unasaidia sio kuua nywele zako bali
kuzikuza na kuzifanya zinawiri. Ikiwa unatumia mafuta ya jeli, umakini
unahitajika katika kuziosha nywele zako. Kama unatumia jeli ya nywele
katika mtindo wako, hakikisha unaosha vizuri na kuondoa jeli yote kabla
ya kulala. Unapolala na jeli au urembo mwingine unaofanana nayo,
unasababisha kuziba kwa tundu za nywele katika ngozi ya kichwa.
Kitendo hicho mbali na kuzuia kupumua kwa ngozi ya kichwa pia huchangia
kuzuia nywele chipukizi kuota katika ngozi ya kichwa. Kuwa makini na
shampoo za madukani Mara nyingi baadhi ya watengenezaji wa vipodozi
huweka maslahi mbele bila kuangalia athari zinazoweza kuwapata watumiaji
wa bidhaa zao. Kwani kuna baadhi ya shampoo huwa na kemikali hatari kwa
ngozi. Hivyo ni vyema zaidi ikiwa utakuwa na uelewa wa kutosha
kuhusiana na aina hiyo ya kipodozi. Pendelea zaidi kutumia herbal
shampoo.
Si hivyo tu wakati mwingine vipodozi vya bei rahisi huwa na kasoro,
hivyo ni vyema kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa nywele kujua ni
aina gani ya shampoo ni sahihi kwa nywele zako. Kinyume cha hapo unaweza
kuishia kuathiri nywele na ngozi yako bila ya mwenyewe kufahamu. Epuka
kubana nywele mara kwa mara Ubanaji wa nywele hasa kuelekea mgongoni
mara nyingi huhatarisha maisha ya nywele zako hasa za usoni. Kwani
kiteno cha kuzibana husababisha kuvutwa kwa nywele na hivyo kusabisha
kukatika hasa kwa zile zilizo hafifu.
Usichane nywele zikiwa mbichi Zinapokuwa mbichi nywele huwa na
uwezekano mkubwa wa kukatika hasa pale zinapochanwa au kufutwa kwa taulo
gumu. Ni vyema ukaacha zikauke kwa upepo na baada ya hapo unaweza
kuzichana. Katika hili kama utakuwa unatumia ‘conditioner’hakikisha
husugui katika nywele na badala yake tumia kwa kupaka. Ikiwa kama nywele
zako zimekatika na hazilingani, ni vyema ukakata ncha ili
kuzisawazisha. Hii husaidia kuzifanya zikue vizuri na pia kuondoa
uwezekano wa kukatika mara zinapoingia maji.
Hasa kwa zile zenye ‘relaxer’. Chochea ukuaji wa nywele zako kwa
kuzichana Unapochana nywele zako hakikisha unatumia shanuo la mbao au
kitana chenye meno yaliyoachana. Hakikisha nywele zako zinakuwa kavu.
Usizivute sana kwani pamoja kusababisha maumivu pia huleta uwezekano wa
kukatika.
Jambo la muhimu katika uchanaji wa nywele, husaidia kuchochea mzunguko
wa damu katika ngozi ya kichwa na pia husaidia kukua kwa nywele.
Imarisha umaridadi wa nywele zako IKIWA utaosha nywele zako kama kawaida
na baadaye kutumia chanuo ama brash katika kuzibana, wakati mwingine
unaweza kusababisha kukatika au hata kuathiri ukuaji wa nywele zako
. Hata hivyo, kwa kufuata ushauri unaweza kuepukana na tatizo hilo na
hivyo kusababisha nywele zako kujaa na kukua vyema. Fuata hizi dondoo
rahisi ambazo ili kuhakikisha unasaidia sio kuua nywele zako bali
kuzikuza na kuzifanya zinawiri. Ikiwa unatumia mafuta ya jeli, umakini
unahitajika katika kuziosha nywele zako. Kama unatumia jeli ya nywele
katika mtindo wako, hakikisha unaosha vizuri na kuondoa jeli yote kabla
ya kulala. Unapolala na jeli au urembo mwingine unaofanana nayo,
unasababisha kuziba kwa tundu za nywele katika ngozi ya kichwa.
Kitendo hicho mbali na kuzuia kupumua kwa ngozi ya kichwa pia huchangia
kuzuia nywele chipukizi kuota katika ngozi ya kichwa. Kuwa makini na
shampoo za madukani Mara nyingi baadhi ya watengenezaji wa vipodozi
huweka maslahi mbele bila kuangalia athari zinazoweza kuwapata watumiaji
wa bidhaa zao. Kwani kuna baadhi ya shampoo huwa na kemikali hatari kwa
ngozi. Hivyo ni vyema zaidi ikiwa utakuwa na uelewa wa kutosha
kuhusiana na aina hiyo ya kipodozi. Pendelea zaidi kutumia herbal
shampoo. Si hivyo tu wakati mwingine vipodozi vya bei rahisi huwa na
kasoro, hivyo ni vyema kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa nywele
kujua ni aina gani ya shampoo ni sahihi kwa nywele zako. Kinyume cha
hapo unaweza kuishia kuathiri nywele na ngozi yako bila ya mwenyewe
kufahamu. Epuka kubana nywele mara kwa mara Ubanaji wa nywele hasa
kuelekea mgongoni mara nyingi huhatarisha maisha ya nywele zako hasa za
usoni.
Kwani kiteno cha kuzibana husababisha kuvutwa kwa nywele na hivyo
kusabisha kukatika hasa kwa zile zilizo hafifu. Usichane nywele zikiwa
mbichi Zinapokuwa mbichi nywele huwa na uwezekano mkubwa wa kukatika
hasa pale zinapochanwa au kufutwa kwa taulo gumu. Ni vyema ukaacha
zikauke kwa upepo na baada ya hapo unaweza kuzichana. Katika hili kama
utakuwa unatumia ‘conditioner’hakikisha husugui katika nywele na badala
yake tumia kwa kupaka. Ikiwa kama nywele zako zimekatika na hazilingani,
ni vyema ukakata ncha ili kuzisawazisha. Hii husaidia kuzifanya zikue
vizuri na pia kuondoa uwezekano wa kukatika mara zinapoingia maji. Hasa
kwa zile zenye ‘relaxer’. Chochea ukuaji wa nywele zako kwa kuzichana
Unapochana nywele zako hakikisha unatumia shanuo la mbao au kitana
chenye meno yaliyoachana.
Hakikisha nywele zako zinakuwa kavu. Usizivute sana kwani pamoja
kusababisha maumivu pia huleta uwezekano wa kukatika. Jambo la muhimu
katika uchanaji wa nywele, husaidia kuchochea mzunguko wa damu katika
ngozi ya kichwa na pia husaidia kukua kwa nywele
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI