игровые автоматы
skip to main
|
skip to sidebar
Social Icons
Pages
Home
NEWS
ENTERTAINMENT
VIDEOS
BIOGRAPHY
CONTACT ME
Wednesday, May 30, 2012
UMEAMUA KUINGIA KWENYE MAPENZI SASA?
UAMUZI wa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi si sawa na kufanya uchaguzi wa aina ya chakula unachopenda kula. Haufanani na uamuzi wa kuchagua muda wa kulala. Haufanani na kitu chochote kile.
Ni uamuzi makini, ambao unahitaji utulivu na uamuzi wa ndani. Si kukurupuka, maana mwisho wake unaweza kuwa machozi. Hebu jiulize, wewe ambaye unataka kuanzisha uhusiano wa kimapenzi upo tayari?
Suala la utayari halikuhusu wewe kama wewe kwa uamuzi binafsi na hisia zako za ndani pekee, lazima uwe na sifa muhimu ambazo zinakidhi wewe kuwa na mwenzi. Tupo pamoja marafiki?
Yapo mambo ya msingi ambayo lazima yawe yametimia kwako, ndipo uwe na hadhi ya kuwa mpenzi wa mtu. Wanasaikolojia ya Uhusiano, wameelekeza wazi vipengele muhimu ambavyo kijana anapaswa kuvizingatia kabla hajaamua kuingia katika uhusiano wa kimapenzi.
Hata hivyo, tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa vijana wengi wanaobalehe au kuelekea kubalehe huwa hawafahamu vipengele hivyo muhimu na hata hao wachache waliopata elimu hiyo elekezi bado hujikuta wakishindwa kufuata taratibu hizo kulingana na mazingira.
Vipo vitu vingi vya kuzingatia, lakini nitafafanua vile vya msingi zaidi, ambavyo vitakuongoza wewe kijana kabla ya kuamua kuingia kwenye uhusiano.
Ni mada nzuri zaidi kwa vijana ambao bado hawajaanza uhusiano, lakini hata kwa aliyeanza, itamsaidia kujua yupo katika kundi gani na nini cha kufanya. Lazima kuna kitu cha kujifunza katika mada hii. Twende darasani.
SUALA LA UMRI
Hili ni la kwanza kati ya yale muhimu zaidi ya kuzingatiwa, lazima uangalie una umri gani? Inawezekana ukawa na umri ambao unadhani una uwezo mkubwa wa kupanga na kuamua mambo yako lakini kumbe siyo!
Unaweza ukaingia katika uhusiano, ukadumu humo kwa muda mrefu sana, lakini wakati huo ukiendelea kukua kiakili, hapo sasa ndipo utakapogundua kuwa kuna makosa uliyofanya awali.
Inashauriwa kwamba vijana ambao wana umri chini ya miaka 18, wasijiingize kabisa katika uhusiano. Huu ni ushauri na mahali pengine siyo ushauri ni lazima! Kama unajijua upo chini ya umri huu, achana kabisa na mapenzi, huu ni muda wako wa kupanga maisha yako ya baadaye.
KWA WANAFUNZI...
Inawezekana ukawa na umri zaidi ya miaka 18, lakini ukawa masomoni, je unaruhusiwa kuwa na mpenzi? Jibu ni hapana...wewe uliye masomoni hususan Elimu ya Msingi na Sekondari hushauriwi kuwa katika uhusiano kwa kipindi hiki. Masomo ni magumu sana kwa ‘levo’ hii na inawezekana ukashindwa kufanya mitihani yako vizuri kutokana na kuwaza mambo mawili kwa wakati mmoja.
Kimsingi ni vitu viwili tofauti ambavyo havichanganyiki. Hii siyo amri, ni ushauri tu! Kama kweli unataka kufanikiwa katika maisha yako ya baadaye, soma kwanza achana na mambo ya mapenzi katika kipindi hiki.
Andaa maisha yako kwanza. Siku moja ukiwa mitaani baada ya kumaliza masomo, ikiwa utabahatika kusoma makala haya kwa mara nyingine gazetini, mtandaoni au hata kwenye kitabu, utajuta na inawezekana ukalia, wakati huo muda utakuwa umeshapita!
FEDHA INAHUSIKA?
Mapenzi na fedha ni vitu viwili tofauti rafiki zangu, lakini kuna wakati fedha inakuwa na nafasi yake katika mapenzi. Siyo kwa maana ya kuhonga au kununua penzi, lakini kwa ajili ya mahitaji ya hapa na pale.
Sasa jiulize, ikiwa wewe ni mwanafunzi, unayetegemea kupewa fedha za matumizi na wazazi wako, utawezaje kugharamia penzi lako?
Ikiwa umekwishamaliza masomo yako, na umri wako unaruhusu (zaidi ya 18), kipengele hiki hakikuhusu, maana penzi la dhati halizingatii fedha. Kama upo masomoni, basi yakupasa usome kwa bidii hadi utakapomaliza masomo yako, mapenzi yapo, utayakuta!
IPO DAWA!
Najua wengi watakuwa na maswali mengi, kwamba kwa sababu tu, mtu anasoma ndiyo asiwe na mpenzi? Au mwingine anawaza atawezeje kuishi bila kuwa na kampani ya jinsia tofauti? Hayo yote ni mawazo yenye maana kubwa katika mada hii. Wataalam wanawashauri wanafunzi kuwa mbali na mapenzi, kwa sababu mapenzi huteka hisia, muda mwingi huweza kuutumia kumuwaza mpenzi zaidi kuliko masomo, sasa kuna haja gani ya kuchanganya mambo wakati inawezekana kuacha?
Haikatazwi kuwa na rafiki wa jinsi tofauti na yako, lakini iwe kwa wema. Kuna mambo mengi unaweza kufanya na rafiki yako kuliko kuwa katika uhusiano wa kingono. Itapendeza kama mtasaidiana kimasomo au kuanzisha mijadala itakayowapa mwanga wa maisha yenu yajayo.
Pamoja na hayo, najua ni vigumu sana kuweza kudhibiti hisia, lakini hilo linawezekana kama utakuwa mtu wa mazoezi, msomaji wa vitabu mbalimbali vitakavyokujenga na mengineyo.
Mchukie kama rafiki yako wa kawaida, weka hisia za mapenzi pembeni, endelea na maisha yako na siku moja muda ukifika na ukiwa tayari utaingia katika uhusiano makini utakaokufurahisha siku zote za maisha yako.
MUHIMU
Katika vipengele vyote nilivyoanisha hapo juu, hasa katika kijisehemu cha kipato na masomo, haviwahusu wanafunzi wa vyuo! Hii inakuwaje? Kwa sababu wengi wao huwa ni watu wazima tayari, wenye ufahamu juu ya mambo mbalimbali ya maisha yao. Wanajua kupambanua mambo na wanajua wanachokifanya.
Wengine huwa tayari wapo katika ndoa au kuingia katika ndoa wakiwa vyuoni, hawa vipengele hivyo haviwahusu. Pamoja na hayo, angalia moyo wako unazungumza nini kabla ya kuingia katika uhusiano. Naamini nimeeleweka.
Tukutane hapa wiki ijayo kwa mada nyingine kali.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
pablo junior calter
About Me
Pablo Junior Calter
Tanzania Best Male Model 2011-2012 || Singer || Songwriter || Fashionist || Trend Setter || Money Maker.
View my complete profile
CONTACT ME
+255718953088
+255784953088
+255767679722
Like Us On Facebook
blog prepared by Pablo Junior Calter. Powered by
Blogger
.
Followers
Popular Posts
HEENA
HINA ni aina ya urembo ambao umekuwa ukitumiwa na watu wengi nchini hususan wa maeneo ya pwani kwa muda wa miaka mingi. Katika kipindi hi...
BREAKING NEWS LULU AKAMATWA AKIWA UCHI NI KIWEWE KIMEMSHIKA i
sasa Lulu(hot Lulu)yupo kituoni police na mahututi kwani anamaumivu na majeraha mengi sana usoni,lulu kapasuliwa pia na Kanumba,ha...
PICHA 20 ZA NYUMBA MPYA ANAYOISHI MWIGIZAJI WEMA SEPETU.
gonga hapa kea picha zaidi PICHA 20 ZA NYUMBA MPYA ANAYOISHI MWIG...
CHANZO CHA KIFO CHA STEPHEN CHARLES KANUMBA CHAFAAMIKA
KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU STEVE KANUMBA, ALISEMA KUWA ELIZABETH MICHAEL MAARUFU KAMA LULU ALIKUJA NYUMBANI KUKAWA NA KAUGOMVI A...
MORE PICS ZA HUKO MSIBANI KWA MAREHEMU STEVE KANUMBA
Ni alfajiri kabisa kama saa 12 hivi watu wengine wakiwa ndio wanaamka na wengine wakienda kulala na kupata mshtuko wa kuondokewa na kip...
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEPHEN CHARLES KANUMBA 'THE GREAT'
HISTORIA YAKE: Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mw...
Usafi wa nywele zako
IKIWA utaosha nywele zako kama kawaida na baadaye kutumia chanuo ama brash katika kuzibana, wakati mwingine unaweza kusababisha kukatika...
WEMA SEPETU AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA MWANAMUZIKI WA MACHOZI BAND.....
Mwinyi wa Machozi Band amvisha pete ya uchumba Wema Sepetu. Tukio hilo limetoke...
MFAHAMU JACKLINE WOLPER FEKI ANAEWATAPELI WATU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
kumekuwa na wimbi kubwa la matapeli kwenye mitandao ya kijamii hususan FACEBOOK, TWITTER, BBM na mingine mingi. Jana katika pita p...
Social Icons
My Blog List
MAJOY BLOG
Collaboration request
-
Hi there How would you like to earn a 35% commission for each sale for life by selling SEO services Every website owner requires the use of search engin...
9 months ago
M.P
How to Enjoy the December Holidays, on a budget.
-
*"There is no reason for you to miss out on the #VacayMood posts, just because your travel budget is limited!"* December is almost here and we ...
2 years ago
JESTINA GEORGE
Waziri Ndalichako azindua chuo kipya cha VETA Kagera
-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua chuo kipya cha VETA Ndolage kilichopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani Kagera k...
5 years ago
BongoClan™
PUNGUZO KUBWA LA BEI ZA HOMETHEATER KUTOKA BONGODECO,PIGA 0658184797 / 0752184797
-
Kama kawaida ya kujali wateja wetu BongoDeco tumetoa punguzo kubwa la bei za Hometheater na Sabufa Kumbuka bidhaa zetu zote tunazouza ni original kabisa n...
6 years ago
Somewhere Blog
-
Blog Archive
►
2017
(1)
►
September
(1)
►
2016
(2)
►
September
(2)
►
2013
(108)
►
October
(22)
►
September
(7)
►
May
(44)
►
April
(33)
►
February
(1)
►
January
(1)
▼
2012
(97)
►
November
(2)
►
July
(6)
►
June
(36)
▼
May
(19)
new hit: ze drinkie ft king charles-cheka kidogo
TABIA HII MPAKA LINI??????
WEMA SEPETU AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA MWANAMUZIKI...
Usafi wa nywele zako
MUACHENI MUNGU AITWE MUNGU
UMEAMUA KUINGIA KWENYE MAPENZI SASA?
USIFANYE SIMU IWE CHANZO CHA KUVUNJA NDO/MAHUSIANO
NEW HIT:ibrah rush feat kalapina - serikali
NEW HIT :marry me-rich mavoko
NEW HIT:nuru-supastaa
MJUKUU WA LUSIFA NAE KAJIUNGA NA FREE MASON?
IT'S ABOUT TIME! MISS DAR CITY CENTRE 2012 IS AROU...
FAIDA YA KUFANYA KAZI AU SHUGULI INAYODHARAULIWA.....
JE UNAZIJUA HIZI ''I LOVE YOU'' ''I MISS YOU'' ZA ...
UMRI, MAJINA YA LULU YAZUA UTATA MAHAKAMANI
RIHANNA REVEALS SKETCHES FOR HER 2ND EMPORIO ARMAN...
ALBINO MODEL DIANDRA FORREST ROCKS CAKE MAGAZINE I...
MSANII SAJUKI KUELEKEA NCHINI INDIA JUMAPILI HII &...
new track released kutoka *B~ONE~RECORDS* chini ya...
►
April
(5)
►
March
(29)
TAZAMA ENTERTAINMENT
advertise
advert info
Total Pageviews
MONTANA
CURRENT TIME
Feedjit
Feedjit Live Blog Stats
GEO COUNTER
widgeo.net
Search This Blog
for more information call us
+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS
My Facebook Profile
Pablo Junior Calter I
Create Your Badge
quote of the day
"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."
No comments:
Post a Comment