Social Icons

Thursday, May 10, 2012

USIFANYE SIMU IWE CHANZO CHA KUVUNJA NDO/MAHUSIANO

KAMA kawaida tumekutana kwenye kona yetu ili kujuzana mawili matatu kuhusiana na mahaba.
Nina imani mada yangu ya wiki iliyopita imezua maswali mengi kwa wapenzi juu ya upendo wa kweli ndani ya simu, wengine walifikia hatua ya kuyasema mengine juu ya matatizo ya simu katika uhusiano wao ambao ameingia shetani mvunja amani ndani ya nyumba.

Dada mmoja baada ya kusoma mada ya wiki iliyopita alisema simu ya mumewe imekuwa kama ngozi kwa laazizi wake huyo, kwani kila anapokwenda, hata iwe msalani. Anapobahatika kuipata anakuta ina ‘password’, kitu ambacho anaamini mume wake si muaminifu.

Aliniuliza kuwa mume wake kufanya vile inaashiria nini? Jibu lilikuwa jepesi, si mwanaume hata mwanamke ukiona simu yake ina password au anaichunga sana hata akiwa nyumbani, ujue pale hakuna uaminifu.
Kama nilivyoizungumzia simu wiki jana kuwa makusudia ya mtu aliyeitengeneza kusudio lake kubwa lilikuwa kurahisisha mawasiliano si kingine. Lakini wanadamu wenye mioyo dhaifu tumeitumia kama kichaka cha kuficha maovu yetu.

Sasa hivi ndani ya nyumba simu imekuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani, asiye muaminifu uilinda simu yake kama ikulu ya Barack Obama.
Sasa hivi ndani ya nyumba zetu inaonyesha jinsi gani zimepoteza unaminifu kila mmoja analinda simu yake kuliko hata wivu kwa mwenzake.

Imekuwa kila mmoja anamwinda mwenzake alale ili aipekue simu, kwa vile ni mzoefu hata ukibahatika kuipata utakuta uchafu wake amefuta ili kupoteza ushahidi.
Ukiona hivyo mnakuwa mnaishi kwa mazoea lakini fahamu hakuna upendo ndani ya nyumba yenu na kuvunja ile ahadi ya kuishi kwa upendo na uaminifu katika ndoa.

Unaweka password unamuonyesha nini mwenzako? kama mwanaume unamuonyesha kabisa mkeo kwamba una wengine zaidi yake hapo unamfundisha nini mkeo, akilipa kisasi umlaumu nani?
Hebu turudie somo letu ambalo nimekuwa nikilitoa kila siku ili ambao hawakubahatika kusoma nilipolitoa ili tuangalie unachokifanya ni sahihi na ndiyo mapenzi?

Nilielezea mapenzi ni kupendana kuheshimiana kuoneana huruma kujaliana na uvumilivu.
Nilielezea mapenzi ni kupendana, kuheshimiana, kuoneana huruma, kujaliana na kuvumiliana. Ukiwa na mapenzi lazima utakuwa na vitu hivi kwa mwenzako, pia utakuwa muwazi kwake na mkweli ili kufanya muweze kuishi bila mmoja kuwa na mashaka na mwenzake.

Wapendanao siku zote hulinda heshima yao kwa kila mmoja kuilinda ya mwenzake, pia kuwa wawazi ili chochote kitakachokwenda kinyume, kiulizwe na kupatiwa majibu sahihi bila kujiumauma. Pia huwa hawana mipaka kuanzia katika miili yao na vitu vyote kwa vile huamini wao ni kitu kimoja, hivyo hawafichani kitu.
Watu kama hawa simu si chanzo cha matatizo, bali ni chombo cha mawasiliano, hakuna mtu wa kuificha simu yake wala kuweka password na kila mmoja ana uhuru wa kuishika au kuopokea ya mwenzake.

Nina imani somo langu limesomeka vizuri, sasa tunarudi kwenye mada ya leo kwa kuuliza swali, sifa nilizozieleza kuhusu mapenzi, je, wewe unazo au mwenzako anazo? Je, simu katika nyumba yenu inatumikaje? Ni chanzo cha migogoro au ni chombo cha mawasiliano ambacho kinaachwa popote bila masharti yoyote?

Tutumie simu kama chombo cha mawasiliano, hata kama si muaminifu katika uhusiano, si lazima mwenzako ajue jinsi gani unavyomdharau kupitia simu.

Simu isiwe chanzo cha migogoro na kuvunja nyumba zetu ambazo sasa hivi zimeingia mdudu ambaye ameonyesha jinsi gani tusivyo waaminifu, kitu ambacho kimeongeza ukosefu wa amani katika ndoa zetu.

Tuwe wawazi na wakweli kwa wenzetu, tuone aibu kuonyesha kwa vitendo sisi si waaminifu. Kama ulijua wazuri kuliko mwenzako wapo wengi, ulikaa naye kwa sababu gani?

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."