MTOTO
wa siku moja mnamo Mei 24, mwaka huu ameokotwa katika makaburi ya
Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya mfuko wa
rambo.
Taarifa
zilizopatikana katika eneo la tukio zilidai kuwa, mtoto huyo alisikika
akilia na wasamaria ambao siku hiyo usiku walienda na kumkuta akiwa
katika mfuko mweusi huku mbwa wakimnyemelea.
Mtoto
huyo wa kike baada ya kuokolewa na wasamaria wema alipelekwa kwenye
kituo cha afya kiitwacho Afya Bora ambapo wafanyakazi wake, Catherine
Shayo na Magreth Masanja walimpa huduma ya kwanza kisha wakatoa taarifa
Kituo cha Polisi Buguruni na kupewa kumbukumbu namba BUG /RB/6238/2012.
Baadaye mtoto huyo mchanga alipelekwa katika Hospitali ya Amana na PC Nel.
Uchunguzi
unaonesha kwamba, maeneo ya Buguruni na Vingunguti yanaongoza kwa
utupaji watoto ambapo Aprili 27 na Mei 4, mwaka huu watoto wawili
waliokotwa mmoja akiwa amefariki.
Na Makongoro Oging'
Global Publisher
Note: Jamani wadada mpaka lini tabia hii, mbona tunakua wanyama hivi? yani inasikitisha kwa kweli.
Kwa
nini mnafanya ngono zembe halafu hamtaki kukubali matokeo? Walaaniwe
wote wanaotoa mimba au kutupa vichanga kama hivi,karne hii si ya kupata
mimba za bahati mbaya, kuna njia za kila aina za uzazi wa mpango ili
kuzuia mimba zisizotarajiwa zinazoleta maafa kama haya. Kuna watu
wanalia usiku na mchana kuomba Mungu wapate watoto wakati wengine
mwawatupa.
Ole wenu wenye tabia hizo damu za hawa watoto zitawaandama siku zote za maisha yenu.
Nimeumia sana.
No comments:
Post a Comment