MSANII
wa filamu nchini Sadiki Juma Kilowoko (Sajuki) anatarajiwa kusafirishwa
kuelekea nchini India mapema wiki ijayo au Jumapili hii kwa ajili ya
matibabu.
Akizungumza na mtandao huu mke wa Sajuki - Wastara Juma amesema kwamba baada ya kukamilika kwa asilimia kubwa ya michango ambapo wameweza kupata jumla ya Sh milion 16 pamoja na ticketi tatau za ndege zilizotolewa na wasanii na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi walio guswa na ugonjwa wa msanii huyo, yeye pamoja na mtu mwingine mmoja wataondoka na Sajuki kuelekea nchini India ambako Sajuki ataenda kuanza matibabu.

Rais wa Shirikishio la Wasanii nchini Ndugu Simon Mwakifamba amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kwa kuanzia maana jumla ya fedha iliyo kuwa inahitajika ni Sh milioni 25 na kuongeza kuwa michango mingine inazidi kuchangishwa na pesa hizo zitatumwa kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.
Sajuki anasumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni. Tuendelee kumuombea Sajuki pamoja na familia yake.
No comments:
Post a Comment