Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa ‘ile
inayoitwa’ movie ya Diamond na Wema Sepetu iliyopewa jina na Diamond,
‘Temptations’ haipo na kama unaingoja, utaingoja hadi miguu iingie
tumboni. Hakuna movie.
Diamond na Wema Sepetu walikuwa
wakila bata na kufurahia kama wapenzi wengine wanaopendana kwa dhati.
Kwa kuangalia picha tu, ni rahisi mno kujua penzi zito kati ya wawili
hawa. Picha hizo ni ishara kuwa, Diamond na Wema hawajawahi kuachana na
Diamond amekuwa akimcheat mpenzi wake Penny.
Wazungu wanasema, kama hujafanya
utafiti hauna haki ya kuzungumza, hivyo ili kuonesha kuwa hizi si brabra
tu, tumefanya utafiti kwanza.
Wema, Diamond na binamu yake Romeo wakiwa Hong Kong
Ukweli wa kwanza tulioubaini ni kuwa,
Diamond na Wema Sepetu walikutana Hong Kong na sio Malaysia. Wema
alienda huko takriban wiki tatu zilizopita na hivyo Diamond alimfuata
baada ya kumaliza show yake ya Malaysia. Kwa mujibu wa msichana aitwaye
Alice aliyeiambia Bongo5, Diamond alisafiri kutoka Kuala Lumpur,
Malaysia kwenda Hong Kong kumfuata Wema kwa ndege ya kampuni ya Air
Asia.
“Nilipanda na Diamond flight moja
from KUL to HKG tena ilikua ni Air Asia X flight number 567 alipandia
KUL-LCC Terminal nilimuona kwenye lounge direct nikashangaa anafanya
nini huku na baada kufika HKG sijui hata alipotelea wapi kumbe haya yote
ndo alikua akiyafuata hongera zao,” alisema Alice.
Huko, Diamond na Wema wamekaa wote
kwenye hoteli moja na mpenzi wake Penny hakuwa anajua kuhusu hili hadi
picha hizi zilipoanza kuenea na yeye ameshtuka kama walivyoshtuka
wengine.
Haijajulikana picha hizo zimesambazwa
na nani lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kuna uwezekano kuwa
picha hizo zimesambazwa na Wema wenyewe kwa kusudi la kumuumiza Penny.
Kuna taarifa zimeifikia Bongo5 kuwa, Penny ameumizwa mno na picha hizo
na amekuwa akilia siku nzima. Hata hivyo binafsi hatujaweza kuthibitisha
taarifa hizo.
Jitihada za kumtafuta Penny azungumzie suala hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokelewi.
Penny
Hivi karibu kwenye birthday ya
Diamond, Penny alielezea kuwa uhusiano wake na Diamond ndio mgumu zaidi
katika mahusiano yote aliyowahi kuwa nayo.
“Not the easiest relationship I’ve
ever had..but its the most intresting! When I’m down, he would make me
feel on top of the world, my bestfriend, my brother, my soulmate, my
baby, my man. My strength, my joy, my love, Ohhh!!! What else do I gotta
say? I love u, and its been a blessing to have met you, u taught me
that love is just Me&You the rest shouldnt matter or make me loose
my sleep, today I ask God to bless u a million more times, the sweetest
boyfriend ever!!! Crazie too..unpredictable mind, through the ups and
downs Im gona hold you down til God says so..you have taught me that
love conquers all, that Love is pain, but the pain is worth the while..I
love you baby,” aliandika Penny.
Miaka ya nyuma, Wema na Penny
walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa mujibu wao wenyewe, urafiki wao
uliharibika hata kabla ya wote kufahamiana na Diamond.
“Urafiki hatuna,” Penny aliliambia
jarida la Mzuka kwenye makala ambayo haikuwa kutoka. “Mimi sidhani kama
nina uadui naye personally, sijui yeye na urafiki hatuna. Let me just
say kwamba sio kwasababu ya Diamond. Nadhani mimi na yeye tulikuwa tuna
issue zetu nyuma ambazo hazikuwa resolved so tulikuwa tuna distance mimi
na yeye. Tulikuwa hatuongei maybe kwa mwaka labda kama sio miezi nane,
we had our own issues kwahiyo hatukuwa marafiki vile tena kama
tulivyokuwa zamani. So mimi kuwa na uadui naye sidhani kama nina uadui.
Mimi am happy unajua, mimi ndo hivyo mimi naishi maisha yangu am happy
na nilichonacho am happy with my man, am happy na watu wangu so am good
mimi sina tatizo naye kabisa.”
Naye Wema kwenye interview na Mzuka aliwahi kuzungumzia alivyojiskia Diamond kuwa na uhusiano na Penny, rafiki yake wa zamani.
“It’s a free world, kila mmoja ana
uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye. They met, they fall in love
wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall in love na mtu yeyote asiwe
questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi kwanini, because alikuwa
rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish them all the best. Mimi
na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii issue, tuna drama zetu tu
za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo tu,” alisema.
Ikumbukwe kuwa, Wema na Diamond
waliwahi kuingia kwenye ‘kile kilichoonekana’ kama ugomvi mzito, baada
ya Diamond kumrekodi mpenzi wake huyo wa zamani alipompigia na
kuisambaza sauti kwenye vyombo vya habari.
“Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni
mtu wa aina hiyo kufanya kitu alichokifanya. Though nimesema kwamba
nitaacha kama ilivyo na nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very
disappointed, very very disappointed,” Wema aliliambia Mzuka.
Tunasubiria kushuhudia muendelezo wa drama hii kutoka kwa Malkia na Mfalme wa drama Tanzania.
SOURCE:BONGO5.COM
No comments:
Post a Comment