Social Icons

Friday, October 11, 2013

NJAIDI AOMBA MSAADA AKATIBIWE NJE

Hamida Hassan
MSANII anayeuvaa uhusika wa mama katika filamu nyingi, Hidaya Njaidi aliyepata ajali mwanzoni mwa mwaka huu na kuumia vibaya mkono anaomba msaada wa matibabu kwani mkono wake umesagika kwa ndani na anahitaji kupatiwa matibabu zaidi nje ya nchi.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Hidaya alisema kuwa kwa sasa mkono wake unamuuma sana na anachosubiri ni kujua kiasi cha pesa anachotakiwa kutoa na hospitali atakayokwenda kutibiwa kati ya India au Afrika Kusini.
“Wiki ijayo ndiyo nitajua baada ya kurudi Muhimbili lakini ukweli ni kwamba mkono unanisumbua. Hata hivyo, sina pesa za kutosha hivyo naomba watu wanisaidie,” alisema Hidaya.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."