Social Icons

Friday, June 8, 2012

HAWA NDO MAFREEMASON WALOTINGA CLOUDS FM......ahahahah

Pichani ni Dkt. Kemu Mzee (kushoto) na Alhaj Prof. Dkt. Salim Kungulila (kulia) wanaojiita Freemasons walio temebele kituo cha Clouds FM leo asubuhi kwenye kipindi cha Leo tena na kuelezea ufreemason wao

Wanadai wao wanafundisha dini zote na kudai kua kila mtu duniani ni Freemason na pia wafafanua maana halisi ya ufreemasons ila mwisho wasiku walishindwa kujibu kama wao ni mafreemasons au laaah! Wakaishia kusema wao ni WaashiHuru…

Walipo ulizwa kama freemason wanaabudu shetani wakashindwa kujibu.

Dkt. Kemu Mzee alisema ufreemason ni kitu ambacho hukioni na ni kama kuuza bidahaa haraka haraka kabla ya mwenzio so hapo wewe uliye uza haraka haraka ndo unatajirika haraka.

Walipo ulizwa juu ya masharti ya kujiunga waksema yanapatikana ofisini kwao na ni lazima mtu apate matibabu yao ambayo ni lazima na kuongezea ni sawa na kujiunga na chama fulani ukafuata masharti yao so kwa upande wao tiba yao ndo lazima.

Na Alhaj Prof. Dkt. Salim alisema watu wanapo ambiwa majini wanaogopa lakini watu wasihofu maana majini ni kama mashine. Mpaka sasa sielewi alimaanisha nini hahaha!!!

Kwa kumalizia waliulizwa kama freemason wanatakiwa kutoa sacrifice (kafara) ya ndugu wa karibu wakasema sacrifice (kafara) kila mtu anatoa wakristo au waislamu. Hiyo yakutoa watu ni uzushi pengine.

Hahaha hakuna siku nimecheka kama leo maana hawa jamaa nahisi walienda kuuza sura walikuwa wanapiga chenga maswali na kujibu yao tu.

Kwa hiyo kuconclude na kutokana na maelezo yao wao wamejiita WAASHIHURU tafsiri yake FREEMASON!
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."