Chanzo kilisema, Juni 3, mwaka huu Kuambiana alikunywa bia kwenye baa ya Fadhili, Sinza Mori, Dar na kushindwa kulipa, hivyo kulazimika kuacha ‘laptop’ yake ili aikomboe atakapolipa deni hilo.
“Tofauti na makubaliano, siku ya pili msanii huyo alimfuata Fadhili na kumtaka ampe laptop yake kwa nguvu bila kulipa deni hilo, alipokataa, alimshushia kipigo Fadhili mpaka alipopata msaada wa polisi,” kilieleza chanzo hicho.
Mapaparazi wetu walifika Kituo cha Polisi Kawe ambapo walikuta mlalamikaji amefungua jalada la kesi lenye namba KW/RB/5761/2012 SHAMBULIO. Kesi hiyo imehamishiwa Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa vile ndiyo kituo cha karibu na eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment