MAZINGIRA
ndani ya Gereza la Segerea jijini Dar yamemlazisha msanii wa sinema za
Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kubadili tabia bila ya kupenda, Amani
linakuhabarisha.
Lulu ambaye ni mshukiwa namba moja katika kifo cha msanii wa filamu nchini, Steven Kanumba, hivi sasa analazimika kuvaa nguo ndefu na kutinga hijabu tofauti na alivyokuwa uraiani.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo katika makabrasha yetu, msanii huyo kabla ya kukumbwa na tuhuma hizo, akiwa uraiani aliwahi kufanya mahojiano na waandishi wa Global Publishers na kudai kuwa hawezi kuvaa nguo ndefu kwa kuwa zinamuwasha mwilini.
Hata hivyo, imebainika kuwa hayo yalikuwa ni maneno ya rejareja ya Lulu kwa lengo la kujitetea kwa mapaparazi.
Haya yote yamekuja kufuatia msomaji mmoja kupiga simu ofisi za Global akihoji kuhusu habari ya staa huyo kudai nguo ndefu zinamuwasha.
“Jamani mimi naitwa mama Diana, naishi huku Tabata. Kuna wakati mliandika madai ya Lulu kwamba anasema akivaa nguo ndefu anawashwa mwilini, siku hizi kila nikiangalia picha zake za mahakamani namwona amevaa nguo ndefu. Je, hawashwi?
“Nauliza kwa sababu hivi karibuni mliandika Lulu apata gonjwa baya gerezani, nikafikiri lilitokana na kuwashwa,” alisema msomaji huyo.
Hata hivyo, alifahamishwa kuwa ugonjwa uliompata msanii huyo gerezani hautokani na kuvaa nguo ndefu.
“Kwa sasa Lulu anatinga nguo ndefu za kila aina na wala halalamiki kuwashwa,” paparazi wetu alimjibu mwanamke huyo.
Kesi inayomkabili msanii huyo itaendelea tena katika Mahakama Kuu Juni 11, mwaka huu na anatarajiwa kutinga akiwa na nguo ndefu nyingine.

No comments:
Post a Comment