WATU wengi tunapokuwa kwenye mikwamo huwa tunatamani
sana kuona wenzetu wanatusaidia. Yawezekana hata unaposoma makala haya
kuna mambo unahisi unahitaji msaada kutoka kwa binadamu wenzako lakini
hao unaotaraji wakusaidie inaonekana kama wamekupa kisogo.
Katika kazi yangu ya ushauri wa masuala ya Elimu ya Ufahamu na Nafsi nimekuwa nikikutana na watu wengi wenye matatizo makubwa ambayo kusema kweli yanahitaji msaada wa wasamaria na wakati mwingine hata kutoka kwa bosi kazini au ndugu waliofanikiwa.
“Huu ni mwaka wa tatu sijapata kazi nahangaika na mwanangu, ndugu zangu wana uwezo lakini hawataki kunisaidia.”Aliniambia dada mmoja hivi karibuni ambaye naamini maelezo yake yalinipa mwanga wa kuandika makala haya kwa sababu niliamini ndugu na jamaa wanaoweza kumsaidia dada yule wapo lakini hajui namna ya kuwavutia.
Katika hali ya kawaida matokeo yoyote tunayoyaona kwenye ulimwengu huu yawe ya kisayansi au kijamii yamevutwa kupitia matendo, fikra na vichocheo vingine. Nyumba hazioti kama uyonga zinajengwa, magari yanategenezwa na watu na hata tabia nazo kuna vitu vya kufanya mpaka kumfanya mwanadamu awe na akili, apendwe au atajirike.
Kwenye maisha kuna kitu kingine muhimu ambacho kinaendana na falsafa ya kuvuta vitu nacho ni kutengeneza mkondo wa maisha. Huwezi kupata fedha mpaka utengeneze mkondo ambao fedha hizo zitapita, inaweza kuwa mkondo wa kuuza bidhaa, kufanya kazi nakadhalika.
Lakini pia ukitaka umeme lazima uweke mkondo wa nyaya, kwenye maji utatakiwa kutandaza bomba ili kipite kile unachotaka kipite kupitia mtandao huo.
Swali langu kwa yule dada aliyenisimulia matatizo yake lilikuwa ni “umetengeza mkondo wa kusaidiwa, unajua namna ya kumvuta mtu akusaidie?” Kusema kweli alishangaa nilipomuuliza swali hilo, yawezekana hata wewe msomaji wangu unashangaa, unawezaje kumvutia mtu akusaidie?
Jibu la swali hili ni rahisi na bila shaka hii ndiyo mbinu pekee ya kumfanya mtu akusaidie haraka nayo ni kumsaidia yeye kwanza kabla hajakusaidia.
Umsaidie nini wakati wewe huna kitu? Ni vema kutambua kuwa kila mwanadamu anahitaji msaada wa wengine, kuna watu wenye fedha nyingi lakini wanahitaji msaada wa heshima, akitokea mtu akiwapa heshima hufurahi na kutoa walivyonavyo kama asante ya heshima.
Mbali na hao wanaotaka msaada wa heshima wapo ambao wanapenda sana mtu wa kuwapelekea watoto shule, kusimamia miradi vizuri, kufagia nyumba zao, kufuliwa nguo, kuzinyoosha, kutumwa hiki na kile kwa uaminifu mambo ambayo anayehitaji msaada anaweza kusaidia bure lakini baadaye akalipwa anachotaka.
Kama hilo halitoshi mtu anaweza kutoa muda wake kazini kwa kufanya kazi za ziada bila malipo, lengo likiwa ni lilelile la kumfanya bosi wake ahisi uwepo wake kwenye ajira ni msaada na hivyo kuwa tayari yeye pia kusaidia kupitia mkopo, nyongeza ya mshahara, safari na semina ambazo zitasaidia kuongeza kipato.
Kwa somo hili, naamini tunaohitaji kusaidiwa tutakuwa tumefahamu namna ya kuvuta misaada na hivyo kutumia mbinu hii kujipatia mahitaji yetu.
Nashukuru kwa kuwa pamoja nami!

No comments:
Post a Comment