Social Icons

Saturday, April 27, 2013

MAPYA YAIBUKA

Stori: Makongoro Going na Haruni Sanchawa
MAPYA yameibuka kufuatia utata wa kifo cha Mwalimu Elizabeth Mmbaga (22) kilichotokea kwa madai ya kunyongwa usiku wa kuamkia Jumatatu, Aprili 15, mwaka huu nyumbani kwake, Kimara -Baruti, Kinondoni, jijini Dar.
Hapa ndipo ulipo kutwa mwili wa marehemu Elizabeth
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini mambo mapya kiasi cha kukifanya kifo hicho kihusishwe na mauaji ya kikatili yanayodaiwa kufanywa na mpenzi wake ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliyejulikana kwa jina la Srinivas, mkazi wa Mikocheni, Dar.
Ndugu wakifungua chumba cha marehemu
Timu ya wachunguzi wetu ilimtafuta mjomba wa marehemu anayeishi Mabibo, Dar ambaye inadaiwa ndiye aliyekuwa akiwasuluhisha Eliza na mpenzi wake na kumuuliza kuhusu kifo hicho na mambo mapya yaliyopo.
Mmoja wa ndugu wa marehemu akimtambua muuaji kwenya picha
“Nakumbuka wiki moja kabla ya mauaji, Elizabeth alinieleza kwa njia ya simu kuwa alipata taarifa toka kwa rafiki yake ambaye ni jirani yake akimwambia kwamba jamaa yake huyo yupo katika baa iliyopo jirani na nyumba aliyokuwa akiishi.
“Ilinibidi nikutane na Eliza, tukafuatana naye hadi kwake kwa vile yule Mhindi alikuwa akimtishia kila mara kwamba atamuua kutokana na mgogoro wao wa kimapenzi.
Enzi za uhai wa marehemu
“Tulipokaribia yule Mhindi akawa anaondoka nyumbani hapo akifuatana na vijana wawili ambao hatujawahi kuwaona. Waliingia kwenye Bajaj, mimi niliwapigia winja, wakasimama, kijana mmoja alishuka na kunifuata.
“Nilimwomba na yule Mhindi ashuke. Nikajitambulisha kwake mimi ni mjomba wa Eliza na kwamba nimepata taarifa anataka kumfanyia fujo Eliza, nikamuuliza kuna tatizo gani?
“Alinijibu hawezi kufanya fujo. Hata hivyo, haikuchukua muda wakaanza kuzozana mbele yangu huku Mhindi  akimuuliza ni kwa nini anampigia simu hapokei!
“Ilibidi nimwombe Eliza aondoke mimi niongee na yule Mhindi ingawa Eliza hakuondoka. Nilimuuliza ana muda gani tangu aanze kufahamiana na Eliza, alijibu ni miezi saba.
“Nilimuuliza kama hawajawahi kukorofishana hata siku moja? Alinijibu wamekuwa wakikorofishana mara kwa mara, nikamshauri aachane naye, akasema anampenda sana hawezi kumwacha.
“Eliza aliingilia kati na kumwambia Mhindi kuwa yeye hampendi, Mhindi akasema yaishe naondoka lakini utaona.
“Wakati huo ilikuwa kama saa tano usiku. Mhindi aliingia kwenye Bajaj na kuondoka na wale vijana wawili. Nilimwambia Eliza asilale  kwake, alifanya hivyo ambapo alikwenda kwa mama’ke mdogo, Tabata - Barakuda.
“Siku ya tukio, saa kumi jioni mama’ke alinipigia simu akinitaka tukutane kwa Eliza. Tulipofika tulikuta walimu wenzake wakilia, tuliwauliza wanacholilia hawakutujibu.
“Mimi niliamua kuingia ndani kwa Eliza na kumkuta amelala, nilipomwangalia niligundua amefariki dunia. Alikuwa akitokwa damu mdomoni na puani. Ulimi ulikuwa nje huku akiwa na alama kama za kucha shingoni, nahisi alinyongwa kwa mkono.
“Nilikwenda Kituo Kidogo cha Polisi Rombo na kutoa taarifa, nikafuatana na  polisi wawili mpaka kwenye eneo la tukio.
“Inauma sana! Hakuna kitu chake chochote kilichochukuliwa, hakika Eliza angetoa taarifa mapema polisi kama alivyoshauriwa kufuatia vitisho vya yule jamaa asingeuawa,” alisema mjomba mtu huyo.
Mama mdogo wa marehemu, Anna Domisian naye alikuwa na haya ya kusema:
“Siku hiyo ya Jumatatu, saa tisa alasiri nilipigiwa simu na mwalimu mmoja akinitaka nifike Kimara kwa Eliza, hawakuniambia kilichotokea. Nilipofika nikakuta mwili wa Eliza ukiwa juu ya kitanda. Nilipatwa na mshtuko mkubwa kwani Jumapili jioni aliniaga anarudi kwake.
“Siku za nyuma aliwahi kunieleza juu ya fujo anazofanyiwa na mpenzi wake wa Kihindi na ndiyo maana nilimweleza mjomba wake aende akawasikilize.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

DENTI WA CHUO KIKUU ARUSHA ALIVYOUAWA

Stori:Joseph Ngilisho,Arusha
MWANAFUNZI wa mwaka wa pili  katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kilichopo Njiro jijini hapa, Henry Koga, ameuawa kikatili na hivi ndivyo alivyouawa.
 
Enzi za uhai wa mwanafunzi huyo
Kwa mujibu wa wanachuo wenzake ambao hawakutaka majina yao kuandikwa gazetini, Koga aliuawa kinyama kwa kuchomwa kisu shingoni na kundi la watu wasiofahamika wakati akitoka kujisomea nje ya chuo usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.
Imeelezwa kuwa tukio la kuuawa kwa mwanafunzi huyo lilitokea saa 4 usiku ambapo marehemu huyo akiwa na wenzake walivamiwa na kundi la wahuni wapatao wanne katika eneo la CDA, jirani na chuo hicho na Koga kuchomwa kisu shingoni na kifuani.
Wanachuo wenzake walisema marehemu hakuwa anatoka kwenye starehe kama watu wengine wanavyodai bali alikuwa na wenzake  wakitoka kujisomea nje kidogo ya chuo hicho kwa ajili ya kujiandaa na mitihani na walipofika eneo hilo, wakavamiwa na watu wasiojulikana.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya wanafunzi  walijikusanya asubuhi yake na kuanza kuandamana kushinikiza uongozi wa chuo hicho kutoa tamko juu ya vitendo vya uhalifu vinavyojirudia mara kwa mara chuoni hapo.
Kufuatia tukio hilo, wanachuo hao walifanya vurugu kubwa na kumlazimisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kwenda chuoni hapo, alipofika kulitokea hali ya kutoelewana ambapo walimzomea na kumpiga mawe, hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kuwafyatulia mabomu ya machozi.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema naye alijitahidi kuwatuliza bila mafanikio huku ikidaiwa yeye ndiyo chanzo cha vurugu hivyo kutakiwa kukamatwa. Mkuu wa mkoa alilazimika kuondoka eneo kuokoa maisha yake.
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Ibrahimu Kilongo akizungumzia tukio hilo, alisema wanachuo 10 wanashikiliwa na polisi kutokana na vurugu hizo na kwamba uchunguzi unaendelea.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

ISHA MASHAUZI MBARONI KWA WIZI

Stori;Richard Bukosi na Issa Mnally
MWIMBAJI ambaye pia ni bosi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan Makongo ‘Mashauzi’, Jumatano iliyopita alikumbwa na masaibu mazito kufuatia kudakwa na polisi wa Kituo cha Msimbazi, Dar akituhumiwa kukwapua mkoba wenye kitita cha shilingi laki saba, elfu hamsini na nane na mia mbili (758,200) mali ya Veronica Tarik.
Chanzo cha habari kituoni hapo kilidai kuwa Jumanne iliyopita, Isha Mashauzi na shosti wake aliyejulikana kwa jina la Halima Shaban waliingia duka moja Mtaa wa Mafia na Jangwani, Kariakoo, Dar kwa lengo la kufanya ‘shopping’ lakini walipochomoka, Veronica alishangaa kutouona mkoba wake.
ISHA AKIMBIZWA
Veronica aliwakimbiza wawili hao na kuwadaka mtaa wa pili na kuwasomea tuhuma zao kisha akawaomba awasachi kwenye mafurushi waliyobeba lakini Isha na mshirika wake waligoma, hali iliyosababisha kuzuka kwa timbwili wakidai mwanamke huyo alitaka kuwadhalilisha.
Baada ya Veronica aliyekuwa na wapambe ‘legelege’ kuzidiwa nguvu, waligeuka na kukimbilia Kituo cha Polisi Msimbazi ambako alifungua kesi ya wizi kwa Isha na shosti wake kwa jalada namba MS/RB/4023/2013.
MSAKO MTAA KWA MTAA WAANZA
Maafande wenye difenda waliingia mitaani kuwasaka watuhumiwa hao mtaa hadi mtaa wakitumia mbinu mpya za kikachero na kufanikiwa kuwatia mbaroni Jumatano iliyopita.
Isha akiwa selo, wapambe wake walimiminika kituoni hapo akiwemo Mtangazaji wa Kituo cha Redio Times FM cha jijini Dar, Hadija Shaibu ‘Dida’ kwa ajili ya kuhangaikia kuwachomoa wawili hao.
WAPAMBE WAMCHOMOA
Saa 5:14 usiku, wapambe hao walifanikiwa kuwawekea dhamana lakini kasheshe nzito ilikuwa wakati wa kutoka rumande kwani wapambe wa Isha waligundua kuwa mapaparazi walikuwa wamekizingira kituo hicho na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kunasa picha zao.
Isha alijaribu kujibanza ndani ya selo lakini wapambe walimpelekea taarifa kuwa mapaparazi nje walikuwa wakijipanga kukesha kituoni hapo mpaka siku itakayofuata.
Baada ya kupata ujumbe huo, Isha alichomoka mahabusu kwa kasi ya mnyama swala na kukimbilia kwenye gari aliloandaliwa kumchukua huku wapambe wake wakiwa wamezikamata kamera za mapaparazi eti ili wasimpige picha.
MSIKIE ISHA MASHAUZI
Kesho yake Alhamisi, paparazi alizungumza na Isha kwa njia ya simu ili aweze kuweka bayana juu ya sakata hilo lakini mwimbaji huyo alimjibu mbofumbofu.
“Wewe andika unachotaka si ulikuwepo kituoni na umenipiga picha, sasa unataka nini? Yaani hata wewe unanifanyia hivyo duh! Leo nimeamini mapaparazi hawana undugu,” alisema Isha na kukata simu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Friday, April 26, 2013

AIBU SANA!

Stori: Issa Mnally
NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.
Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).
BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.
Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.
ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.
BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.
MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE
Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo.
Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule.
Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.
MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?
Kwa upande wake OCD Mutafungwa alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.

INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.

NI MATOKEO YA GAZETI LA RISASI
Oparesheni hiyo ilikuja siku chache baada ya gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko, toleo namba 1000 la Jumatano ya Aprili 17-19 kuripoti ufuska unaofanyika katika ufukwe huo usiku wa saa 9 na kuendelea.
Uchunguzi wa gazeti hilo ulieleza kiundani vitendo vya ngono, usagaji, ubakaji, ushoga na ujambazi vilivyokuwa vikifanyika eneo hilo hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni wakaona kuna kila sababu ya kufumua uozo huo kwa kuwa ni wachapakazi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

WEMA, WEEEH ACHA TU!


Stori:Imelda Mtema
Kwa mara nyingine staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatengeneza kichwa cha habari baada ya kuacha historia jijini Arusha kufuatia ulinzi mkali aliokuwa nao, Ijumaa lina data zote.
Habari za uhakika zilieleza kuwa Wema na timu ya wafanyakazi katika kampuni yake ya Endless Fame Production, alikodisha ndege ya kifahari kutoka Dar kwenda Arusha kwa ajili ya mapumziko tangu Aprili 18 hadi 20, mwaka huu.
Ilifahamika kuwa ndani ya ndege hiyo ambayo kuikodisha ni mkwanja mrefu, aliongozana na kampani yake tu.
CHANZO CHA YOTE NI DIAMOND
Ilibumburuka kuwa timu yake hiyo ilikuwa takriban watu watano ambao walimsindikiza kwenda kwenye mapumziko kutokana na ‘stresi’ alizokuwa nazo.
Ilielezwa kuwa stresi alizokuwa nazo zilitokana na ile ishu ya kudaiwa kurekodiwa akibembeleza penzi kwa aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku mkali huku jamaa akiwa amelala na mpenziwe wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Baada ya kutokea kwa ishu hiyo ndipo Wema alipoamua kwenda kujichimbia Arusha kupoteza mawazo.
“Unajua ile ishu ilimchanganya sana bidada maana hakutegemea kama Diamond anaweza kufanya kitu kama kile so (kwa hiyo) alikwenda kutuliza akili na kweli sasa hivi walau yupo fresh (vizuri),” alisema sosi wa karibu wa Wema.
AINGIA ARUSHA KWA ULINZI MKALI
Walipoingia jijini Arusha, staa huyo wa Filamu ya The Super Star alipokelewa kwa ulinzi mkali hadi katika hoteli ya bei mbaya aliyokuwa ameweka oda kwa ajili yake na watu wake.
“Unaambiwa kuanzia Arusha Airport (uwanja wa ndege) hadi hotelini ilikuwa ni full ulinzi wa kufa mtu,” kilisema chanzo chetu,

APOKEA MWALIKO
Habari zilieleza kuwa akiwa hotelini hapo, habari zilienea kama moto wa kifuu kuwa yupo jijini Arusha hivyo akapokea mwaliko kutoka kwa mashabiki wake waliotaka japo kumuona tu kwenye Fashion Show iliyoandaliwa.

KASHESHE
‘Eventi’ ilifanyika kwenye Ukumbi wa Club D (World Garden) uliopo jijini humo na ndipo kasheshe lilipoibuka kwa watu kukanyagana wakitaka kumuona na kupiga naye picha.
“Aisee Wema wee acha tu! Kusema kweli watu wanampenda sana. Kuna wakati niliona kama ukumbi unakuwa mdogo na kwa taarifa yako ilikuwa haijatangazwa. Sijui kama ingekuwa imetangazwa kuwa Wema yupo A-town, ingekuwaje maana kila mtu alitaka japo amshike tu,” alisema sosi wetu huyo.

MENEJA
Kwa mujibu wa meneja wake, Martin Kadinda, ilibidi kuomba ulinzi maalum wa mabaunsa ambao walihakikisha hadhuriki.
“Tuliwaambia tupo na mtu mkubwa sana hivyo tukapatiwa ulinzi maalum wa kuhakikisha Wema hapati tatizo la mtu kumdhuru na ndicho tulichokifanya,” alisema Kadinda.
Ilifahamika kuwa kwa harakaharaka ulinzi wa Wema ulikuwa na takriban watu wasiopungua 10, yote ikiwa ni kuhakikisha usalama wake.

AFANANISHWA NA KIM KARDASHIAN
Kwa mujibu wa mashabiki wake ukumbini hapo, ulinzi wa Wema ulifananishwa na ule wa staa wa Marekani, Kim Kardashian ambaye hivi karibuni aliwekwa mtu kati na watu zaidi ya 32 wakiwemo askari na mabaunsa.
“Kweli Wema sasa amefikia levo za akina Kim, yaani naye ana ulinzi mkubwa hivi?” alihoji mmoja wa mashabiki wake.

TIMU NZIMA
Ukimwacha Wema na Kadinda, wengine walioambatana nao ni Kajala Masanja, Petit Man ‘Wakuache’, Tinny Daddy na Nurdin Bilal ‘Shetta’.
Baada ya mapumziko wote walirejea jijini Dar na kuendeleza libeneke wakiwa ‘wamerefreshi’ akili.

NI KUFURU NYINGINE
Hii ni kufuru nyingine ya Wema ambapo swali liliendelea kubaki palepale kuwa anapata wapi fedha anazotumia katika matukio yake ya gharama kubwa huku nyuma yake kukiwa na madai kuwa kuna ‘mkubwa’ mmoja anamuwezesha.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MR NICE ATANGAZA NDOA KENYA

Stori:Mwandishi Wetu
Mfalme wa miondoko ya TAKEU, Lucas Nice Mkenda ‘Mr Nice’ hivi karibuni ametangaza azma yake ya kuoa huku akieleza kuwa, mkewe mtarajiwa atakuwa ni Mkenya.
Akifanyiwa mahojiano na Kituo cha Televisheni cha  Kenya, Citzen TV, Mr Nice alisema miongoni mwa mambo yaliyomfanya aende nchini humo ni pamoja na hilo la kuoa.
“Suala la kuoa ni moja kati ya mambo yaliyonileta hapa, mke atapatikana na nitawaambia, kwa sasa hayo tumuachie Mungu,”  alisema Mr Nice
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

DIAMOND: NAENDA LONDON KUMLETEA MAMA MCHUMBA

Stori:Sifael Paul
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaendelea kutunisha akaunti yake baada ya kulamba shavu la shoo za kutosha nchini Uingereza ambapo ameahidi kurejea Bongo na mchumba rasmi atakayemtambulisha kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’.
Mkali huyo wa ngoma ya Kesho alifunguka hayo juzikati kupitia website yake alipokuwa akizinadi shoo hizo atakazofanya kwenye majiji ya London na Reading, Uingereza ambapo aliwataka warembo hasa Wabongo waishio humo kupendeza ili achague mmoja atakayekuwa mchumba’ke.
Bila kujali mjadala utakaoibuka kwa kuwa tayari ana mchumba ambaye ni Penniel Mungilwa ‘Penny’, Diamond alifunguka: “Mashabiki wangu wa London na Reading kijana wenu nakuja kuweka historia kwa mara nyingine. Warembo mpendeze nakuja kuchagua mchumba mmoja wa kuja kumtambulisha kwa mama Diamond.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

USHOSTI WA LULU, PENNY WAZUA MINONG’ONO

Stori:Hamida Hassan
Ushosti unaoonekana kuwepo sasa kati ya msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha DTV ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Penniel Mungilwa ‘Penny’ umeibua minong’ono huku baadhi wakidai eti Lulu ana lengo la kumrusha roho Wema.
Hilo limeibuka kutokana na ukweli kwamba, sasa hivi Wema na Penny haziivi baada ya Diamond kuhamishia penzi kwa mtangazaji huyo na kwamba kitendo cha Lulu kuonekana ‘close’ sana na Penny ni lazima kitamuuma Wema.
“Ni ukweli ulio wazi kuwa Wema hawezi kumpenda Penny, lakini pia kitendo cha Lulu kuwa karibu na Penny ni lazima kitamuuma Wema na atahisi lao ni moja, inawezekana Lulu kafanya makusudi ili kumrusha roho Wema,” alisema msanii mmoja wa filamu aliyeomba hifadhi ya jina lake kukwepa bifu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Listen n download wakali kwanza new song

Listen n download wakali kwanza new song

http://www.hulkshare.com/dl/5e90vu1n99ts/Artists_Maka%20mua%20ft%20Joslin%20&%20Edina_Track_Nitarudi.mp3?d=1

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

JIACHIE BEACH PARTY

JIACHIE BEACH part berinda 27/4 juma mosi, karibu na whtsend kwa kiingilio cha buku tano tu *music*na kutakuwa na models pale na michezo kibao na suprize kibao huku KINGKAPITA akifanya yake na mdogo wake ambaye ndio mtamuona kwa mara ya kwanza SABAU njoo ujionee mwenyewe kuna msanii mkubwa atapanda ila njoo utamjua hapo,*music* *wine* huku ukifahamiana na marafik zako wa mtandaon toka FB,BBM,TWEETR,na nyingine kibao,zawad kama kawa  kuanzia saa saba mpaka majogooo,mwambie na jiran na rafik yako.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Thursday, April 25, 2013

Wanaume wanavyoibiwa kwa ‘I love U, I miss U baby!’

Ndugu zangu, wiki hii nataka kuzungumzia suala moja ambalo nahisi wanaume wengi hawalifahamu. Kwa kifupi ulimwengu wa mapenzi wa sasa umetawaliwa na usanii wa hali ya juu.
Wanawake wengi wameyageuza mapenzi kama kitega uchumi. Wapo ambao hawataki kusikia suala la kuwa na wapenzi wala kuolewa wakiwa na dhamira ya kutaka kuwa na uhuru wa kuwabadili wanaume kadiri wanavyotaka.
Unaweza kukutana na msichana mzuri sana, ukampenda na kudhani anaweza kuwa mkeo. Yeye akishabaini umemzimikia, anakuwekea mapozi ya kimtindo kwa muda kisha anakukubalia.
Kwa kuwa na wewe umeoza kwake, utakuwa tayari kumfanyia chochote ili uweze kumshikilia. Akilini mwako unajipa matumaini kuwa uko peke yako na huyo atakuwa mkeo siku zijazo kumbe mwenzako ana lengo la kukuchuna tu.
Atatumia maneno matamu kukulainisha lakini mizinga itakuwa sehemu ya maisha yake. Kwa kuwa na wewe unampenda na hauko tayari kumkosa, utakuwa ukimpa pesa na huduma nyingine.
Unajua kitakachotokea? Huenda hujui lakini wengi wanafanya hivi; anakupiga mizinga sana hadi inafikia hatua unamchukia na kuhisi hakufai.
Kuhisi kwako hakufai ndiyo furaha kwake kwani na yeye hakuweka akilini mwake kuwa anataka kuolewa na wewe. Matokeoa yake unabaki ukiumia kumkosa na pia itakuuma zaidi kwa kuwa ametumia pesa zako nyingi bila kufanikisha kile ulichodhamiria.
Hivyo ndivyo ilivyo sasa na kwa mfano kuna hii mitandao ya kijamii kama vile Facebook. Huku wanaume wengi wanalizwa na hawa mabinti wajanja wa mjini.
Msichana anaweza kukuomba urafiki ukamkubalia, baada ya muda anajitongozesha kwako kwa kudai amekuzimikia. Kama na wewe utakuwa limbukeni na ukadata na mtu ambaye wala humjui lakini maneno yake yakakuvutia, tarajia kulizwa.
Nasema hivyo kwa kuwa, ni lazima ataonesha kukupenda sana na atakuwa akikuandikia maneno matamu kama vile I love you, I miss you na mengineyo ya aina hiyo na ukishakolea si ajabu akaanza kukuambia anataka kuonana na wewe ila kwa kuwa yuko mbali anataka umtumie nauli.
Lakini hata kabla ya kukuambia umtumie nauli, anaweza kuwa ameshakuomba pesa nyingi, vocha za kutosha na wewe ukawa unamtumia ili kulilinda penzi lenu.
Sasa mwisho wa mawasiliano yenu utakuwa pale ambapo atakuomba umtumie nauli ili aje muonane, ukishamtumia tu anaingia mitini na huwezi kuamini msichana huyo anaweza kuwa na wanaume wengi anaowafanyia hivyo.
Wengine hawatumii mtandao wa Facebook bali hutumia simu zao kuwaingiza mjini wanaume. Kwa kifupi huo ni mchezo ambao upo na wanaume wengi wameshalizwa.
Kikubwa ni watu kuwa makini na hawa wasichana warembo wanaojirahisi kwa wanaume. I love you, I miss you ni maneno tu ambayo anayeyatamka anaweza akawa hamaanishi hivyo bali anataka kukupumbaza tu na ukiingia kwenye laini akuchune weee mpaka mwenyewe uachie ngazi kisha yeye anahamia kwa mwingine.

Ni hayo tu kwa leo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

IRENE UWOYA: UKINIPASUA ROHONI UTAMUONA KRISH

Stori:Imelda Mtema
MAMBO vipi msomaji wangu wa safu hii maridhawa ya Staa na Mwana, kama ilivyo ada hapa tunapata kuwajua watoto wa mastaa.
Big up kwenu ambao mnaendelea kutuma maoni yenu, nawashukuru sana. Kutokana na maombi ya wengi, leo tunaye mwigizaji, Irene Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja, Krish Ndikumana.
Birthday Boy Krish akiwa katika pose siku ya bethidei yake mwaka jana
Krishi ana umri wa miaka miwili, ili kujua mengi ungana nami katika mahojiano niliyofanya naye hapa chini:
Krish na mama yake wakizima mishumaa wakati wa bethidei yake mwaka jana
KRISH NDIYO NUSU  YA MAISHA YAKE
“Ki ukweli nafikiri kabisa mtoto wangu ndiyo nusu ya maisha yangu, ukinipasua roho yangu utamkuta yeye na ninaweza kutembea lakini nikimkumbuka tu, akili yangu inafikiria kumuona wakati huohuo.”
NINI MAANA YA JINA LA KRISH
“Kuna filamu ya Kihindi nilikuwa nikiipenda sana kuitazama ilikuwa ikiitwa Krish, kwa kweli nilijiwekea nadhiri kuwa kama nikibahatika kujifungua mtoto wa kiume nitampa jina la Krish na Mungu aliponibariki nikafanya hivyo.”
UPENDO KWA MTOTO UPOJE?
“Kiukweli nahisi Krish ndiyo mtu wa kwanza ninayempenda katika uso wa dunia na wengine wanafuata kwa sababu kuna wakati nahisi ni kama nyama yangu imekatwa halafu akatokea Krish.”
ANAISHI NAYE?
“Krish tangu nijifungue anaishi kwa bibi yake na amezoea sana huko, hata bibi na babu yake wanapenda sana kukaa naye kwa vile ni mjuu wao wa kwanza hivyo kwao ndiyo kila kitu.”
HAMKUMBUKI MWANAYE?
“Daah! Unajua kuna wakati najishangaa iwe usiku kiasi gani, nikimkumbuka mwanangu nawasha gari hadi Mbezi fasta nakwenda kumuona na nyumbani huwa wanashangaa sana.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

RECHO, SAGUDA WAPEANA MALOVEE HADHARANI

Stori:Mwandishi Wetu
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rechael Haule ‘Recho’ amenaswa akipeana malovee hadharani na jamaa’ke anayejulikana kwa jina la Saguda George.
Tukio hilo lililoibua minong’ono lilitokea juzikati katika Viwanja vya Leaders jijini Dar wakati staa huyo na wenzake walipokwenda kula raha zao ambapo ilidaiwa kuwa kilevi kilipofika mahali pake, ndipo wawili hao walipoanza kubusiana hadharani.
“Mh! Hawa nao ifike wakati waoane kama wenzao kina Kupa, wamedumu katika uhusiano kwa muda mrefu sasa, kwa nini waendelee kujiibaiba hivi?” alihoji msanii mkubwa wa filamu aliyeomba hifadhi ya jina lake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MZEE KANKAA AGONGWA NA GARI

Stori:Denis Mtima ma Chande Abdallah
MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amegongwa na gari wakati akifanya mazoezi ya kutembea kufuatia ugonjwa wake wa kiharusi.
Tukio hilo lilitokea Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Kariakoo, Dar ambapo gari hilo aina ya Toyota Voxy lilitokea ghafla na kumgonga kidogo na kumsababishia michubuko kwenye miguuni na kichwani.
Dereva wa gari hilo alifanya uungwana kwa kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo ndugu zake walitaarifiwa na kwenda kumchukua.
“Mzee Kankaa alitoka nyumbani na kutuaga kuwa anakwenda kufanya matembezi. Tulijua ni karibu, lakini baadaye tukasikia taarifa kuwa amepata ajali na yupo Kituo cha Polisi Msimbazi,” alisema Abdul ambaye ni mtoto wa Kankaa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

NATASHA: NDOA YANGU ITAKUWA BEI CHEE


Stori:Gladness Mallya
MKONGWE wa filamu Bongo ambaye pia ni mtangazaji, Suzan Lewis ‘Natasha’ amefunguka kuwa ndoa yake itakuwa simpo kwani hataki mbwembwe nyingi kama ilivyo kwa wengine.
Akizungumza hivi karibuni katika kituo kimoja cha runinga, Natasha alisema ndoa yake itakuwa ya kawaida ‘simpo’ na zaidi atahakikisha waalikwa wanapata msosi na  kunywa vizuri na asiwepo mtu wa kulalamika.
Msanii huyo alizidi kutiririka kuwa, alikuwa akitamani kuolewa sana kwani hakuwahi kupitia hatua hiyo hivyo muda umefika wa kutimiza ahadi ya Mungu kwa binadamu kuzaliana na kuongezeka japokuwa watu wamekuwa wakisema mengi  na amewaomba msamaha wote waliokwazwa na uamuzi wake wa kuolewa.
“Nilikaa na familia yangu ikakubali, mjukuu wangu Junior nilipomwambia kuhusu ishu hiyo hakuwa na kipingamizi hivyo siku si nyingi nitaolewa,” alisema Natasha.
a ndoa alikubali na nikaamua kuolewa lakini angekataa, nisingeolewa kwa sababu huyu ndiyo kila kitu kwangu,” alisema Natasha.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

VANESSA MDEE AGOMBEWA KUOMBWA KOLABO

Stori: Centre Spread
STAA wa Songi la Closer, Vanessa Mdee amefunguka kuwa mara baada ya kuachia wimbo huo ambao unafanya vizuri kwa sasa, wasanii wengi wamekuwa wakimuomba kumshirikisha katika nyimbo zao.
Centre Spred imetonywa kuwa, mwanamuziki huyo ambaye anasimamiwa na Kampuni ya B Heatz amekuwa akipokea maombi mengi lakini anauachia uongozi wake ufanyie kazi maombi hayo kwa umakini.
“Uongozi wa B-Hitz chini yake Hermy B ndiyo wanaoelewa muziki wangu na kujua ubora wa muziki hivyo wao ndiyo wananipa mwongozo lakini kiukweli nashukuru Mungu maombi ninayopata ni mengi,” alisema Vanessa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

KIDUMU AMMWAGA MZAZI MWENZIYE

Stori: Sophia Marcel
MWANAMUZIKI kiwango wa Burundi anayepiga mzigo pande za Kenya, Nimbona Jean Pierre ‘Kidumu’ amemwagana na mzazi mwenzake aliyezaa naye watoto wawili.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Kidumu ameamua kuachana na mwanamke huyo aliyekuwa akiishi naye awali baada ya kupata kifaa kipya kinachosoma Chuo Kikuu cha Nairobi ambacho anatarajia kufunga nacho pingu za maisha Julai, mwaka huu.
Alipoulizwa na waandishi kuhusiana na ishu hiyo, Kidumu alikiri kumpata mpenzi huyo mpya toka kabila la Wakikuyu na kubainisha kuwa ndiye anayemlelea watoto wake ambao alizaa na mwanamke wake wa awali ambaye hakumtaja jina.
“Ni mapema kumjua kwa jina mpenzi wangu mpya, mashabiki wajue kwamba ninaye na nitawatambulisha mambo yatakapokuwa sawa huko mbeleni,” alisema Kidumu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

CHUZ AMSAJILI BATULI

Direkta wa Kampuni ya Tuesday Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ ameamua kumsajili mwigizaji anayekuja kwa kasi, Batuli ili kuimarisha kampuni yake.
Akizungumza na Centre Spred, Chuz alisema amefikia uamuzi wa kumchukua nyota huyo baada ya kuona uwezo wake katika kazi ambazo amezifanya na zimefanya vizuri sokoni.
“Natarajia kumchezesha katika filamu yangu mpya ya Makaburi ya Kinondoni, uwezo wake ni mkubwa nina imani atafanya vizuri,” alisema Mr Chuz.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Wednesday, April 24, 2013

MREMBO ABAMBWA KWA WIZI

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
MREMBO mmoja, Rukia Omari mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar amebambwa akidaiwa kuiba fedha kwa njia za miujiza eneo la
Bunju Mwanjenje kwenye duka la Wapemba.
Akiojiwa na mwandishi baada ya kukamatwa
Imeelezwa kuwa katika tukio hilo, Rukia alichukua fedha kimiujiza dukani na kutokomea, hali iliyosababisha wenye duka kutangaza dau la shilingi 500,000 kwa atakayewezesha kukamatwa kwake.
Mrembo akiwa chini ya ulinzi
Arobaini zake zilipowadia, Rukia alikamatwa akiwa mafichoni, Boko Mtambani na kushushiwa kichapo na wananchi wenye hasira
wakimtaka amtaje aliyemtuma.
Baada ya kupokea kichapo, mrembo huyo aliwataja baadhi ya watu akiwemo mganga mmoja anayetokea Sumbawanga (jina tunalo)
na kudai kuwa ndiye aliyekuwa akimpa dawa (chuma ulete).
“Dawa hiyo huwa naiweka kwenye pesa zangu nyumbani ili ziongezeke na nyingine huwa natembea nayo kwa ajili ya kujipatia
pesa,” alisema mrembo huyo. 
Mrembo huyo alikiri kufanikiwa kuiba mamilioni ya shilingi kwa kutumia dawa hiyo na kuomba asamehewe. Rukia aliokolewa na
ndugu zake pamoja na wasamaria wema waliompeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo alikofunguliwa mashtaka ya wizi.
Tukio hilo ni la pili kwa Rukia kwani mara ya kwanza alikamatwa Tabata jijini Dar es Salaam miezi michache iliyopita kwa tuhuma

kama hizo lakini akaachiliwa baada ya kuomba msamaha.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."