Spika wa Bunge Anne Makinda amewaasa Wabunge kutumia Lugha ya Staha ambayo ni ya Kibunge wakati wa kuchangia mijadala Bungeni. 
Mhe.
 Makinda amesema, kuendelea kutumia lugha ya matusi, kejeli na maudhi 
kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ni kuendelea kuliondolea hadhi 
Bunge.Pamoja na hilo, wabunge wanatakiwa kujikita katika kuchangia hoja 
zenye kutataua matatizo ya wananchi ili kutimiza wajibu wa kila mbunge 
wa kuwa wakilisha wananchi. 
Mhe.
 Makinda , amesema, fursa ya kila Mbunge kuchangia lazima ilenge kutatua
 matatizo ya wananchi na sio kutukanana na kusahahu jukumu lilomblele ya
 kila Mbunge. Katika Picha ni baadhi ya waheshimiwa Wabunge waliochangia
 mjadala wa kupitisha Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na 
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2013/14 Mjini 
Dodoma.






No comments:
Post a Comment