Social Icons

Thursday, May 16, 2013

SHABIKI WA MARA CLARA HIZI NDIZO PICHA ZA SUZAN ZILIZOKUWA GUMZO KUPITIA MTANDAO WA EMINEYS ZICHEKI HAPA

















TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

WAREMBO WA MISS UTALII TANZANIA 2013 WAFANYA KUFURU NDANI YA CLUB HADI WAVUA VIATU ZICHEKI PICHA ZAO HAPA














TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

BABY CANDY AELEZA ISHU YA KUWEHUKA

Na Hamida Hassan
VIDEO Queen wa Bongo Fleva, Mimah Mohammed  ‘Baby Candy’ ameibuka na kueleza namna ambavyo aliugua malaria kali hadi kudaiwa kuwa amerogwa na shosti wake, Jacqueline Pentzel.
Mimah Mohammed ‘Baby Candy’.
Chanzo makini kililiambia Amani kuwa hivi karibuni nyota huyo alichanganyikiwa kwani majini huwa yanampanda kichwani mara kwa mara huku Jack  akidaiwa kuwa ndiyo chanzo cha matatizo hayo.
“Amewehuka kabisa, ukimuona utamuonea huruma na Jack ndiye anayedaiwa kumroga,” kilisema chanzo.
Baada ya habari hiyo kuvuja, paparazi wetu alimtafuta Baby Candy ambaye alikiri kuumwa pamoja kupata taarifa za uvumi kwamba Jack anahusika lakini yeye anamshukuru Mungu kwani ameshatibiwa hospitalini.
“Mimi na Jack bado tunaongea vizuri, niliamua kukaa mbali naye kwa sababu ya maneno mtaani, siwezi kusema alinifanyia kitu kibaya, nilikuwa nikisumbuliwa na malaria, nimetibiwa hospitali na sasa nimepona,” alisema.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MABAKI YA MWANAMKE YAKUTWA JIRANI NA MAGEREZA

Na Francis Godwin, Iringa
MABAKI ya mwili  wa mwanamke  anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ambaye jina lake halikufahamika, yamekutwa  eneo la Magereza, Kata  ya Miyomboni Kitanzini, Manispaa ya  Iringa.
Polisi wakikusanya mabaki ya mwanamke huyo.
Mabaki hayo  yalikutwa majira ya saa 6:00 mchana, juzikati yakiwa yamesambaratika kutokana na kuoza.
 Walioyakuta ni maofisa wa magereza ambao walikuwa katika  eneo hilo na wafungwa  wakikata miti kwa ajili ya  kuni.
Wakizungumza na Amani, baadhi ya  mashuhuda walidai kuwa mwanamke  huyo inaonekana siku ya kifo chake alikuwa amevaa suruali nyeusi, kilemba cha kitenge chenye madoa mekundu, njano, meusi na meupe pamoja na skafu ya rangi nyeupe na nyeusi.
Mashuhuda hao walidai kuwa  mwanamke huyo alipoteza maisha kwa zaidi ya wiki  mbili nyuma kutokana na mabaki hayo kuharibika kupita kiasi na kukauka.
Polisi akikusanya nguo za marehemu.
Mazingira ya kifo cha mwanamke huyo yalionesha utata  kwa kuwa hata polisi  waliofika eneo la tukio, walikiri kutokuwepo kwa taarifa yoyote ya mtu  kupotea na kwamba  inawezekana alivamiwa ama alikufa kwa matatizo yake au alikuwa akitoka hospitali ambayo ipo jirani na eneo hilo.
Mabaki ya  mwili  huo yalichukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika Chumba cha Maiti cha Nina Marwaha cha Hospitali ya Rufaa Mkoa  wa Iringa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MASOGANGE: SIKWENDA AFRIKA KUSINI KUJIUZA

Na Mwandishi Wetu
‘VIDEO Queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ ameibuka na kusema kuwa hakwenda Afrika ya Kusini ‘Sauz’ kujiuza kama baadhi ya watu walivyompakazia.
Agness Gerald ‘Masogange’.
Akipiga stori na Amani, Masogange ambaye iliwahi kuvuja video yake ya utupu mwaka jana, alifafanua kuwa picha mpya zinazodaiwa kuwa ni za nusu utupu zilizozagaa mtandaoni, zilisababishwa na ulevi na si kweli kwamba ni za kujiuza.
‘’Sijui hizo picha zilisambaa vipi kwa sababu zilikuwa kwenye kamera yangu na mimi siku hiyo nilikuwa nimelewa, sikuwa naelewa chochote na sikuwa utupu kiivyo kama wambeya walivyosema,” alisema Masogange.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

CHAZ BABA AMVISHA PETE MCHUMBA’KE JUKWAANI


Na Musa Mateja
PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ juzikati aliendeleza harakati za maandalizi ya ndoa kwa mashabiki wake baada ya kumvisha pete jukwaani mchumba’ke, Rehema Sospeter.
Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ akimvisha pete mchumba’ke, Rehema Sospeter.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Amani lilijiri Mei 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama, Dar, wakati bendi yake ilipokuwa ikitambulisha albam mpya, Risasi Kidole.
Akizungumza na paparazi wetu mapema wiki hii, Chaz Baba alisema ameamua kuonesha uamuzi wake huo kuanzia kwa mashabiki wake waliofika ukumbini na kwa wale wasiofika kwa sababu wengi wao walikuwa hawamuamini.
“Nilifanya vile kukata vilimilimi ‘coz’ tangu nimegawa kadi za mchango wa harusi, kumekuwa na maswali mengi ambayo yanaashiria wengi hawaamini uamuzi wangu,” alisema Chaz.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

AUNT EZEKIEL APOZWA MACHUNGU YA MAREHEMU MAMA’KE NA MTOTO WA KAKA’KE


Na Imelda Mtema
ALHAMISI nyingine imewadia msomaji wangu, tunakutana tena na mastaa ambao Mungu amewajilia kupata mtoto na kujua staili wanayoishi nyumbani kwao.
Aunt Ezekiel 'Mrs Demonte' akiwa na 'mwanaye' Nicole.
Leo tunaye staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel 'Mrs Demonte' ambaye anaishi maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar na mtoto wa miaka 2 anaiyetwa Nicole kama mwanaye wa kumzaa.
Hivyo basi, kutokana na kumlea mtoto huyo tangu akiwa mdogo, moja kwa moja amepata nafasi ya kukaa kwenye safu hii, ungana nami katika mahojiano niliyofanya naye;
Amani: Mambo vipi, mtoto huyo kila siku uko naye ni wa nani?
Aunt: (kicheko cha kiana) Ni wangu, watu wanafikiri mimi sina mtoto?
Amani: Hata mimi ndiyo najua leo, ulimzaa kwa siri?
Nicole akimlisha keki 'mama'ke'.
Aunt: Hapana bwana nilikuwa nakutania tu, huyu ni mtoto wa kaka yangu.
Amani: Mh! Mbona kila nikikutembelea hapa kwako nakuona uko naye, wazazi wake wapo wapi sasa?
Aunt: Wazazi wake wote wapo lakini mtoto huyu ni zaidi ya kila kitu kwangu.
Amani:  Kivipi?
Aunt: Yaani tangu anazaliwa yuko mikononi mwangu na nikaamua kumlea mimi kama mtoto wangu na hata yeye anajua mimi ni mama yake mzazi.
Amani: Kwani ndugu zako si wana watoto wengi, kwa nini huyu tu?
Aunt: Huyu ni mtoto wa kaka yangu ambaye kwa mama yetu tulizaliwa wawili tu hivyo nikimuona huwa ananipoza machungu kwani ni kama marehemu mama yangu.
Nicole katika pozi.
Amani: Sasa unavyosafiri kwenda Dubai kwa mumeo huwa inakuwaje?
Aunt: Yaani huwa ninamkumbuka sana na nikimuona mtoto amekatiza mbele yangu huwa naumia na machozi kunilengalenga kabisa.
Amani: Sasa kwa nini usiondoke naye?
Aunt: Ndiyo nimeanza kufanya taratibu hizo maana hata shule nimemtafutia kule Dubai.
Amani: Sasa vipi Mungu akikujalia mtoto wako, upendo utazidi kuendelea kwa huyu au vipi?
Aunt: Nitawapenda wote, sidhani kama kutakuwa na tofauti kati ya mwanangu na huyu kwa sababu nampenda sana Nicole.
Amani: Nashukuru sana Aunt.
Aunt: Asante, karibu tena.
Upendo wa mama na mwana.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Wednesday, May 15, 2013

BARUA NZITO : USTAA ULIONAO LEO UKUTENGENEZEE UZEE MZURI!

KWENU,
Wasanii mnaong’aa katika sanaa mbalimbali nchini. Ninafurahi kuwasiliana nanyi tena kwa wakati mmoja baada ya kuachana muda mrefu uliopita. Naamini mpo sawa na michakato ya kusaka mkate wa kila siku inaendelea vyema kabisa.
Kama ndivyo, ndiyo furaha kwangu. Nazungumza nanyi mastaa katika fani mbalimbali Bongo. Inawezekana wewe ni mwanamuziki, mwanasoka, mtangazaji, mchoraji, mchongaji, mwanamitindo au msanii wa filamu.
Nyota yako kwa sasa inang’aa na kila unapopita unakubalika. Ni jambo la kujivunia sana. Heshima yako ni kubwa kupitia sanaa yako. Inawezekana wewe ni mtunzi wa vitabu na unakubalika sana kwa kazi yako ambayo inakuingizia fedha nyingi.
Hongereni wote kwa pamoja. Pamoja na yote hayo, yapo mambo ya msingi ambayo nataka kuwashauri ili muweze kubaki kileleni siku zote na  mwisho wa siku muwe na uzee mzuri usiosababisha kero kwa wengine. Mmenipata ndugu zangu?
TAFUTA KUWA NAMBA MOJA
Ukiwa kama staa, usijisahau katika nafasi uliyonayo na kudhani labda utaendelea kuwa hapo siku zote. Dunia inabadilika na ushindani kwenye sanaa yoyote ni mkubwa. Usibweteke kwa unachopata leo ukaona kinatosha.
Umiza kichwa zaidi ili uwe/uendelee kuwa namba moja. Kuwa mbunifu zaidi na endelea kujifunza ili uwe staa mkubwa nchini. Chipukizi wengi wanakuja nyuma yako, ukilegeza kidogo tu unaachwa!
KIMATAIFA ZAIDI
Baada ya kujihakikishia kwamba umeshika nafasi ya juu Bongo, unatakiwa kupanua zaidi ubongo wako na kujifunza ili uwe wa kimataifa. Huwezi kubaki hapohapo na ukaendelea kujiona wewe ni staa.
Thubutu! Marehemu Steven Kanumba alionesha mwanzo mzuri. Wengine wanaofuata nyayo zake ni Lucy Komba, Hashim Kambi, Wema Sepetu na baadhi ya wanamitindo na wacheza soka ambao wanajaribu kutafuta soko la kimataifa.
ANZISHA MIRADI
Pamoja na mafanikio makubwa ya kimataifa, huwezi kujiita staa na kujivunia kama hutawekeza katika miradi. Kama nilivyosema awali, chipukizi wengi wanakuja nyuma yako na wanaweza kukushusha wakati wowote.
Ili kuepuka hilo ni vyema kutazama kesho yako – siku ukishuka na kushindwa kufurukuta kwenye sanaa. Anzisha miradi ambayo itakusaidia. Fungua biashara au kampuni mbalimbali kwa kutumia lebo ya jina lako ambalo tayari lipo juu.
Siku zijazo ukishastaafu, hutakuwa na dhiki wala kuomba misaada. Mifano ipo mingi tu. Wapo mastaa wengi wa zamani, sasa hivi wanateseka. Juzi tu, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla alijibu hoja bungeni, Dodoma akisema kwamba, serikali haina utaratibu wa kuwasaidia wanasoka pindi wanapostaafu.
Umeona kazi hiyo?
MIFANO IKO WAZI
Pongezi kwa mastaa ambao wameshtuka mapema na kujiwekea misingi ya baadaye. Wapo ambao wamejenga nyumba, wamefungua kampuni na mambo mengine mazuri ambayo yataendelea kubaki hata kama ustaa utatoweka.
Wapo wengi lakini hapa nakutajia wachache kama Jide, AY, Profesa Jay, Izzo Business, Jafarai, Juma Nature, H – Baba, Dully Sykes, Mike T na Chegge (Bongo Fleva), JB, Ray, Pastor Myamba, Wema Sepetu, King Majuto, Aunt Ezekiel (Bongo Movies), Aboubakar Sadiq, B12, Harris Kapiga, Dida (watangazaji) na Kaseja na Ngassa (soka).
Hawa wawe mfano kwako na wakupe nguvu ya kuandaa maisha yako baada ya ustaa wako kushuka. Kumbuka unaweza kuendelea kuishi kistaa hata baada ya kuwa nje ya gemu. Uamuzi upo mikononi mwako.
Yuleyule,
Mkweli daima,
.................
Joseph Shaluwa
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

BABY MADAHA: NAMFUATA MWISHO NAMIBIA

Na Gladness Mallya
LICHA ya Mwisho Mwampamba kuwa mume wa ndoa wa Meryl Shikwambane, msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha amesema anajiandaa kwenda nchini Namibia wanapoishi wanandoa hao kwa lengo la kujumuika na Mwisho na kula bata.
Baby Madaha.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko jijini Dar es Salaam, Baby alisema bado ana uhusiano wa kimapenzi na Mwisho na kwamba yeye ndiye alimwalika aende Namibia wakafurahie penzi lao.
“Nakwenda Namibia kwa Mwisho wangu. Simwogopi huyo Meryl, kwanza yeye ndiye aliyeingilia penzi langu. Mimi ndiye wa kwanza kuwa na Mwisho, hivyo ni halali yangu.
“Mwisho mwenyewe ndiye aliyeniambia niende na amesema nitafikia hotelini, nitafurahi naye kwa muda wote nitakaokuwa huko, mambo mengine mwenyewe ameshayapanga na atajua cha kufanya.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MASHOGA WAFURIKA PATI YA MSANII


Na Hamida Hassan
PATI ya Miss Utalii 2004 ambaye ni mwigizaji wa filamu za Kibongo, Sara Mwakapala aliyomuandalia mwanaye Anthonio kumpongeza kwa kutimiza umri wa miaka mitatu, nusu itibuke baada ya jamaa waliodaiwa ni mashoga kufurika.
Mmoja wa vijana waliodaiwa kuwa mashoga akikata mauno.
Katika pati hiyo iliyofanyika maeneo ya Leaders, Kinondoni, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, mbali na mashoga hao waliokuwa wakiserebuka taarab, pati hiyo pia ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali ambao walimtuza Anthonio fedha na zawadi kibao.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Sara alifunguka kuwa alifurahishwa na tukio hilo la mwanaye kutimiza umri huo kwani malezi si mchezo, yanahitaji kujipanga.
...Vijana hao walitokelezea kama mnavyomuona mmojawapo kulia.
Sarah alimzawadia mwanaye simu aina ya Ferrari yenye thamani ya Sh. laki tano huku maandalizi yote ya shughuli hiyo yakigharimu Sh. milioni 3.
Wageni waliomtuza mtoto huyo ni pamoja na Faiza ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Mimah Mohamed ‘Baby Candy’.   
Baadhi ya warembo waliohudhuria sherehe hiyo wakiwa na Sara Mwakapala (wa kwanza kushoto).
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

LADY JAYDEE YAMEMKUTA

MWANAMUZIKI Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, juzi Jumatatu hatimaye yalimkuta baada ya kuibua simanzi nzito katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar, alipofikishwa baada ya kufunguliwa kesi ya madai namba 29/2013 na mabosi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga.
Lady Jaydee na mumewe Gadner G Habash wakiwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar.
KAMA JAY-Z NA BEYONCE
Hali katika mahakama hiyo iligubikwa na huzuni baada ya watu kumuona Lady Jaydee akiwasili eneo hilo sambamba na mumewe Gadner G Habash ambapo walifananishwa na wanandoa mastaa wa Marekani, Shawn Carter ‘Jay Z’ na Beyonce Giselle Knowles, walipotimba mishale ya saa 6:00 mchana.
Risasi Mchanganyiko liliwashuhudia mastaa hao wakiingia eneo hilo huku wakiwekewa ulinzi mkali kama ilivyo kawaida mahakamani kuhakikisha usalama wa watu.
Wawili hao waliongozana hadi chumba cha makarani ambapo walielezwa kesi inayomkabili mwanamuziki huyo na kupangiwa siku ya kesi ambayo ni Mei 27, mwaka huu.
Pia walitajiwa hakimu atakayeendesha kesi yao kuwa ni Athumani Nyamrani wa chumba namba 2 cha mahakama hiyo.
Baada ya kupewa utaratibu wa kesi hiyo walichomoka mahakamani na ndipo wakakutana na paparazi wetu aliyewasimamisha na kutaka kujua madai yaliyofunguliwa.
...Wakielekea chumba cha makarani mahakamni hapo.
JAYDEE AAHIDI KUPAMBANA
Akizungumza na paparazi wetu, Lady Jaydee alisema: “Kesi inahusiana na masuala ya kimtandao, eti Ruge na Kusaga wanadai nimewachafua.
“Kwa leo sitaki kusema mengi, baada ya kupata fomu hizi sasa hivi tunampelekea mwanasheria wetu lakini kila kitu kitawekwa bayana Mei 27, kesi itakapotajwa mbele ya hakimu.
“Kama wameamua kupambana na mimi nitapambana kwa msaada wa Mungu.”
HOFU YA KUFILISIWA
Baadhi ya watu waliokuwa mahakamani hapo walionekana kumuonea huruma mwanamuziki huyo kwa jinsi alivyokuwa akihenya kwenye viunga vya mahakama hiyo huku akipishana na askari wenye silaha nzito.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisikika akisema kesi hiyo inaweza kumpotezea muda mwingi na kumuathiri kisaikolojia kwani haijulikani hatima yake ni nini.
...Wakiwa eneo la mahakama.
WAKILI WA AKINA RUGE APIGWA ‘STOP’ KURONGA
Paparazi wetu alikutana na wakili wa upande wa akina Ruge mahakamani hapo lakini alikataa kutoa ushirikiano na kusema anaogopa kuizungumzia kesi hiyo kwa kuwa bosi wake hakumuagiza kufanya hivyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

11 KORTINI KWA KUZINI NA MBWA

WANAWAKE 11 raia wa Kenya pamoja na Mzungu raia wa Sweden, hivi karibuni wamefikishwa katika mahakama moja iliyopo Mombasa kwa kudaiwa kunaswa wakirekodi mkanda wa ngono na mbwa.
Wanawake hao waliotajwa kwa majina ya Beatrice Mueni Mwosa, Waithera Karanja, Marry Nyambura Kimani, Magdaline Wairimu, Celestine Nekesa, Dorcus Melisa, Ludia Nyaboke, Phidelia Mawia, Anne Wanjiku, Cecilia Nzambi na wengineo wanadaiwa kunaswa na polisi katika eneo la Nyali wakifanya uchafu huo.
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa katika eneo hilo, ilikutwa kamera na kompyuta mpakato ‘laptop’ mali ya Mzungu huyo anayedaiwa kuratibu mpango mzima, vitu ambavyo vilichukuliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Katika hatua nyingine, imedaiwa kuwa mwanaume huyo Msweden aliingia nchini humo kama mtalii na akawa karibu sana na mwanamke Mkenya ambaye inadaiwa ndiye aliyewakusanya wanawake wengine kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.
Hata hivyo, upande wa mashitaka utakuwa na kazi kubwa ya kuthibitisha kama kweli wanawake hao wamehusika kwani inadaiwa wakati wanakamatwa, mmoja tu ndiye aliyekuwa amesharekodi ‘scene’ yake.
SERIKALI YA KENYA YACHARUKA
Wakati kesi ikiendelea mahakamani, makamu wa rais wa nchi hiyo, William Ruto ameeleza kusikitishwa na tukio hilo, akasema amewaagiza watu wa usalama kuhakikisha raia wa kigeni wenye tabia chafu kama hizo wanatimuliwa mara moja.
“Nimewaambia watu wa Internal Security (Usalama wa Ndani) kwamba watu kama hawa hawafai kuwa katika taifa letu la Kenya, wapandishwe ndege waende kwao,” alisema Ruto.
WABONGO WAONYWA
Kufuatia tukio hilo, mademu Bongo wenye uhusiano wa kimapenzi na Wazungu wametakiwa kuwa makini kwani baadhi si watu wema.
Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko baada ya kesi hiyo kuwa gumzo, baadhi ya watu wamesema kilichotokea Kenya ni fundisho kwa wasichana wa Kibongo wanaoshobokea Wazungu.
“Hilo limetokea Kenya lakini ni fundisho kwa mabinti wetu hapa nchini ambao wanakimbilia kuanzisha uhusiano na Wazungu.
“Kuna uwezakano wapo wanaofanyiwa vitendo hivyo kwa kuahidiwa pesa nyingi au kuwekewa mitego na hatimaye kurekodiwa picha chafu wakiwa wanajua au hawajui,” alisema mama Salma wa Magomeni jijini Dar aliyedai kwamba amekuwa akifuatilia kesi hiyo tangu ilipoanza kusikilizwa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

POLISI 7 KIZIMBANI KWA KUTESA, KUUA, NA KUWAINGIZIA MITI SEHEMU ZA SIRI WATUHUMIWA

POLISI saba kutoka wilayani Kasulu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, iliyoanza kikao chake mjini Kigoma leo na kusomewa mashitaka ya kuua kwa kukusudia. Mbele ya Jaji Sam Rumanyika, askari Polisi hao walidaiwa kuwa Agosti 6, 2011 walimpiga na kumuua kwa makusudi Festo Stephano, mkulima na mkazi wa Kijiji cha Rungwe mpya wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Waliopandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yao ni pamoja na Baraka Hongdi, Koplo Mawazo, Koplo Swahib, Koplo Charles, Koplo Shamsi, Koplo Jerry na Koplo Amrani ambao kwa pamoja walikana mashitaka.
Baada ya kukana mashitaka, kesi hiyo ilianza kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao, ambapo shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Masumbuko Stephano, aliieleza Mahakama kwamba askari hao walikusudia kufanya mauaji hayo.
Masumbuko aliieleza Mahakama kwamba siku ya tukio, alikamatwa pamoja na marehemu na mgambo wa kijiji, na kuwekwa katika mahabusu ndogo katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata.
Alidai baada ya kufika, askari hao walianza kuwapiga kwa kutumia vitako vya bunduki, fimbo na chupa za bia, hali iliyosababisha wapatwe na maumivu makali.
Shahidi huyo alidai kuwa baada ya kupigwa na kukaribia kupoteza fahamu, polisi hao waliwavua nguo, wakawafunika na turubai ndani ya gari ambapo baadaye walinunua magunia ya mkaa na kuwakandamiza na magunia hayo.
Shahidi wa pili katika kesi hiyo, Andrea Sama, alidai kwamba askari hao walikusudia kufanya mauaji siku hiyo, kwani licha ya kutoa kipigo pia waliwavua nguo na kuwaingiza miti kwenye sehemu zao za haja kubwa.
“Mheshimiwa Jaji kwa kweli nilishuhudia vitendo vya askari hao kwa macho yangu, na nilishindwa kuamini kama jambo hilo linafanyika kwenye ardhi ya Tanzania au tuko nchi nyingine, maana unyama uliofanywa na askari polisi hao huwezi kudhani kama ni walinzi wa amani katika nchi hii,” alidai Sama.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa mfululizo hadi kutolewa hukumu, ambapo mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Juvelin Rugaihuruza, alidai kuwa upande wa Jamhuri ambao ndiyo mlalamikaji, unatarajia kuwa na mashahidi 12 na vielelezo viwili.
Washitakiwa hao wanatetewa na Mwanasheria, Method Kabuguzi, kutoka Kampuni ya Uwakili ya Kigoma Law Chamber and Advocate ya mjini Kigoma.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

WEMA AZUNGUMZIA PICHA YAKE ILIYOSAMBAA MITANDAONI AKIWA KATIKA POZI ZA KIMAHABA NA RAHEEM....SOMA ALICHOKISEMA

HATA kama ukimkwepa vipi, lazima utakutana na stori yake tu! Staa wa Bongo, Wema Sepetu anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine, safari hii ametokelezea na mwanaume mwingine katika pozi tata lililozua minong’ono kwa mashabiki wake.


Wema akiwa katika pozi la kimahaba na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Raheem.
Wema ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006, huku akifurukuta kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, ametokelezea na mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Raheem katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
GUMZO MITANDAONI
Picha hiyo ambayo pozi lake ni ‘very romantic’ imezua gumzo katika mitandao mbalimbali ilipotundikwa na wadau wengi walionekana kuamini kuwa Wema alikuwa akimnadi mpenzi wake mpya.
Mtoa maoni mmoja aliandika: “Naona Wema ameamua kutuonesha shem wetu mpya, sasa hapo kazi kwa wenye vijicho.”
Mwingine aliandika: “Mmh! Mbona (Raheem) haonekani uso? Kama lengo lake lilikuwa kumwanika angemuacha tu aonekane ila dah! Ana kifua kizuri sana. Huyu jamaa anaonekana anafanya sana mazoezi.”
DIAMOND ATAJWA
Katika gumzo hilo, wengine walikwenda mbali zaidi, wakisema kwamba inawezekana Wema alikuwa na Raheem kwa siri muda mrefu lakini sasa ameamua kuvunja ukimya ili kumringishia x - boyfriend wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Siku zote alikuwa wapi? Atakuwa anamwoneshea Diamond tu huyu,” mtoa maoni mwingine aliandika.
INTERVIEW NA RAHEEM
Ni jadi ya magazeti ya Global Publishers likiwemo hili la Risasi Mchanganyiko kutafuta mzani wa habari kabla ya kwenda hewani hivyo lilimtafuta Raheem ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha.
Raheem alikiri kuitambua picha yake na Wema lakini alisema imemshtua na kumcha-nganya maana hakutegemea kama ingefika mitandaoni na hatimaye kwenye vyombo vya habari.
Wema Sepetu.
Alisema: “Ni kweli nilipiga hiyo picha na Wema lakini ni ya kawaida tu, haina maana nyingine tofauti. Wema ni rafiki yangu na dada yangu. Tunaheshimiana, hakuna cha zaidi.
“Wema ni maarufu na watu wanaweza kujaji wanavyotaka, hilo litanisababishia matatizo kwa sababu mimi nina mpenzi wangu na Wema si mtu wangu kabisa...she is just my sister (ni dada yangu tu).”
Risasi: Hiyo picha mlipiga lini, wapi na kwa matumizi gani?
Raheem: Ilikuwa kwenye function (tukio) fulani ambayo siwezi kuizungumzia. Kama wiki sita au miezi miwili hivi iliyopita na tulipiga kama marafiki tu, hakuna cha zaidi.
Risasi: Kwa hiyo Wema akithibitisha wewe ni mpenzi wake itakuwaje?
Raheem: Nitamshangaa sana! Wema ni dada yangu tu.
Risasi: Inasemekana Wema ameamua kuianika hiyo picha kwa lengo la kumrusha roho Diamond, unasemaje hapo?
Raheem: Sijui na kwa kweli siwezi kuzungumzia mambo ya mtu binafsi. Sijui chochote.
GONGA HAPA KUMSIKIA WEMA
Wema alipatikana na kusomewa mashitaka yake ambapo alikiri kupiga picha na Raheem, akafafanua kuwa aliipiga muda mfupi baada ya kutoka kufanya interview na kituo kimoja cha redio (jina kapuni) lakini akasema haina uhusiano wowote na suala la mapenzi.
“Ni kweli nilipiga hiyo picha, yeye aliniomba tu kama fan (shabiki) wangu, akataka ku-show love (kuonesha upendo), sikuona sababu ya kumkatalia. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Martin (Kadinda – meneja wake) na baada ya siku hiyo sijawahi kuonana naye tena mahali popote...sioni tatizo kabisa, ni kawaida kwa sisi mastaa,” alisema Wema.
Risasi: Lakini Wema wadau wanasema eti ni mpenzi wako na umefanya hivyo kwa lengo la kumrusha roho Diamond.
Wema: Umeshasema wadau, waache na mambo yao lakini maelezo yangu ni hayo na naamini yamejitosheleza.
Risasi: Kuna kitu nahitaji ufafanue zaidi...lile pozi lipo romantic sana, hufikiri kuwa inaweza kuwa sababu ya watu kuwa na hisia kwamba ni mpenzi wako?
Wema: Ni kweli picha ni romantic lakini yule kijana (Raheem) si mpenzi wangu. Naomba nieleweke hivyo. Ahsante.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Tuesday, May 14, 2013

BWANA HARUSI AMUUA BABA YAKE KWA RISASI HUKO KIBAHA


Mwanaume mmoja wa miaka 47 aliyejulikana kwa jina la Shirima mkazi wa Kibaha, amemuua baba yake mzazi anayekadiriwa kuwa na miaka 70 kwa kumpiga risasi iliyotoka kwenye bunduki yake (short gun -"SMG")

Inasemekana baba huyo alikuwa amelala nyumbani kwa mwanae akitokea Moshi kwa mwaliko wa harusi ya bwana Shirima ambayo ilikwisha fanyikana .Siku hiyo Shirima na mkewe walikua honeymoon hapo nyumbani kwao.


Usiku wa jana baba yake alipatwa na haja ndogo akaenda chooni wakati anarudi akakosea mlango wa chumba chake na kuingia chumbani kwa mwanae....


Mke wa Shirima aliposikia mlango unafunguliwa na mtu yupo ndani, alianza kupiga kelele za mwizi....mwiziiii!!!...,

Hapo ndo mumewe akachukua short gun yake na kumlenga babake na kumuua akidhani ni mwizi.

Inavyosemekana ni kwamba, mtaani kwao nyumba zipo mbalimbali na ndo maana akachukua uamuzi wa kumimina risasa bila kuuliza hata swali moja kwa mvamizi huyo wa chumbani kwake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

MWANAUME ALIYELAZWA WADI YA WANAWAKE DAR; MAAJABU SABA


Na Makongoro Oging'
MAAJABU zaidi yamebainika kuhusu kijana wa kiume, Karina Mohamed ‘Natalia’, 20, aliyelazwa wodi ya wanawake akidhaniwa ni mwanamke.
Karina Mohamed 'Natalia' akiwa katika hospitali ya Amana.
Karina, alilazwa wodi ya wanawake akidhaniwa ni mwanamke kwenye Hospitali ya Amana ambayo ina hadhi ya mkoa kitabibu, Ilala, Dar es Salaam, kabla ya kugundulika akiwa chumba cha maiti baada ya kufariki dunia.
Pamoja na habari hiyo ya Karina kuandikwa kwenye gazeti ndugu na hili la Risasi Jumamosi, toleo namba 1005 la Mei 4, mwaka huu, Uwazi limebaini maajabu yaliyofanya alazwe wodi ya wanawake kwa siku mbili bila kugundulika.

MAAJABU YA KWANZA; SURA
Timu ya gazeti hili imebaini kuwa sura ya Karina, haina tofauti yoyote na ya mwanamke.
Uwazi limepata ushahidi wa picha za Karina, enzi za uhai wake na kujiridhisha kwamba sura ya kijana huyo ilikuwa na sifa nyingi za kike kuliko za kiume.
Karina Mohamed 'Natalia' enzi za uhai wake.
MAAJABU YA PILI; UMBO
Kupitia picha ambazo alipiga akiwa amevaa nguo za kubana, imebainika kuwa Karina ambaye ana asili ya Kiarabu, alikuwa ameumbika kwa sifa nyingi za kike.
Consolata Temu, 26, aliyemfahamu Karina enzi za uhai wake, alisema: “Niwe mkweli, yule jamaa aliumbika kike kuliko wanawake wengi sana. Mimi mwenyewe niliwahi kumwambia kwamba ningeumbika kama yeye ningeringa sana.”
Akaongeza: “Hipsi za Karina ni za kike zaidi. Nimewahi kukaribiana naye na kufanikiwa kumshika, yule jamaa alikuwa na mwili laini mpaka unaweza kujiuliza alikuwa anakula nini. Maana ni mwanamke kabisa.”

MAAJABU YA TATU; SAUTI
Imeelezwa kuwa Karina alikuwa na sauti nyembamba kiasi kwamba kila aliyezungumza naye, aliamini ni mwanamke mpaka yeye mwenyewe alipoamua kueleza.
“Akinyamaza utaondoka na imani kwamba umekutana na mwanamke. Wanaume wengi walimtongoza kwa kuamini ni mwanamke. Ukizingatia ni mzuri sana.”

MAAJABU YA NNE; KIFUA
Imebainika kuwa wauguzi kwenye Hospitali ya Amana, walishindwa kubaini kuwa Karina ni mwanaume kwa sababu kifua chake, japo hakina matiti lakini kimekaa kama cha mwanamke.
  Muuguzi mmoja (jina tunalo), alisema: “Sisi tulijua maziwa yake ni madogo, maana alivyo ni mwanamke mtupu. Tulishangaa sana kujua ni mwanaume, maana ni mzuri kuliko hata sisi wengine hapa.”

MAAJABU YA TANO; TUMBO
Muunguzi huyo alisema: “Kuna kipindi wakati wa kumhudumia, tulipandisha nguo na kumpima tumbo. Sijawahi kuona tumbo la mwanaume likiwa laini vile. Lile ni tumbo la kike. Huo ndiyo ukweli, kwa kweli hilo lilikuwa tukio la kwanza kuliona.
“Mtu mwenye sifa zote za kike, baadaye kugundulika ni mwanaume, nilishangaa sana.”

MAAJABU YA SITA; NYWELE
Kwa mujibu wa muuguzi, Karina alifika hospitalini hapo akiwa na nywele ndefu ambazo ziliwekewa dawa, kufanana kabisa na za mwanamke.
“Hakuna anayeweza kutulaumu kabisa katika jambo hili. Hata angekuwa nani, asingekubali kama yule ni mwanaume. Hata aliyegundua baadaye ni baada ya kumuona jinsia yake wakati alipovuliwa nguo,” alisema.
Ukweli kuhusu nywele, vilevile unajidhihirisha katika picha zake enzi za uhai wake, zinazomwonesha akiwa ametengeneza nywele katika mitindo mbalimbali ya kike.

MAAJABU YA SABA; NYETI
Rafiki wa Karina, aliyeomba hifadhi ya jina lake gazeti, alisema: “Yule jamaa alikuwa na ‘umbile’ dogo sana ambalo hakulifurahia. Kitendo cha kuwa na ‘umbile’ hilo, aliona mkosi, ndiyo maana alikata tamaa, moja kwa moja akaamua kujishughulisha na mapenzi ya kinyume na maumbile.
“Alijishughulisha na vitendo vya ushoga na hili linafahamika kwetu sisi tuliokuwa watu wake wa karibu na ndiyo maana alikuwa na vitendo vingi vya kike na alichukia kuitwa mwanaume.”

KUZIKWA NA JIJI
Habari zinasema kuwa Karina ni raia wa Kenya, mwenye asili ya Jiji la Mombasa, Uwazi limebaini kuwa mpaka sasa hakuna ndugu aliyejitokeza kumtambua.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala, Dar es Salaam, Marietha Minangi, alisema: “Hakuna ndugu aliyejitokeza, endapo zitapita siku saba kabla ya ndugu kujitokeza, basi atazikwa na jiji. Siku saba zinahesabiwa kuanzia pale alipofariki dunia.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

WANAFUNZI WAVAMIWA NA MASHETANI, WAANGUKA HOVYO

Mmoja wa wanafunzi aliyepandisha mashetani akiwa amelala baada ya kuanguka.
Mmoja wa wanafunzi aliyepandisha mashetani akiombewa.
Baadhi ya wanafunzi walioanguka.
Umati wa wazazi waliofika kushuhudia tukio hilo na kuwachukua watoto wao.
Baadhi ya viongozi wa eneo hilo pamoja na diwani wao wakielezwa na mwalimu jinsi tukio hilo lilivyoanza.
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda maeneo hayo.
Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.
(Picha/Stori: Gladness Mallya/ GPL)
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."