Social Icons

Tuesday, May 14, 2013

BWANA HARUSI AMUUA BABA YAKE KWA RISASI HUKO KIBAHA


Mwanaume mmoja wa miaka 47 aliyejulikana kwa jina la Shirima mkazi wa Kibaha, amemuua baba yake mzazi anayekadiriwa kuwa na miaka 70 kwa kumpiga risasi iliyotoka kwenye bunduki yake (short gun -"SMG")

Inasemekana baba huyo alikuwa amelala nyumbani kwa mwanae akitokea Moshi kwa mwaliko wa harusi ya bwana Shirima ambayo ilikwisha fanyikana .Siku hiyo Shirima na mkewe walikua honeymoon hapo nyumbani kwao.


Usiku wa jana baba yake alipatwa na haja ndogo akaenda chooni wakati anarudi akakosea mlango wa chumba chake na kuingia chumbani kwa mwanae....


Mke wa Shirima aliposikia mlango unafunguliwa na mtu yupo ndani, alianza kupiga kelele za mwizi....mwiziiii!!!...,

Hapo ndo mumewe akachukua short gun yake na kumlenga babake na kumuua akidhani ni mwizi.

Inavyosemekana ni kwamba, mtaani kwao nyumba zipo mbalimbali na ndo maana akachukua uamuzi wa kumimina risasa bila kuuliza hata swali moja kwa mvamizi huyo wa chumbani kwake.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."