Social Icons

Tuesday, May 14, 2013

SARA AMZAWADIA MWANAYE SIMU YA LAKI TANO

Sara akimpatia zawadi ya simu aina ya Ferrari mwanaye. Simu hiyo ina thamani ya shilingi laki tano.
Sara Mwakapala (kushoto) akiwa katika pozi na Faiza ambaye ni mzazi mwenzake Mheshimiwa Sugu (katikati) na kulia ni msanii wa filamu Khadija Kasogo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kikundi cha Sanaa cha Nderemo.
Keki aliyokata Vit Anthonio.
Mtoto Vit Anthonio akiwasha mishumaa kwa ajili ya kukata keki akisaidiwa na Faiza. Wengine pichani ni watoto wenzake, mama yake na mama zake wadogo.
...Wakizima mishumaa.
Picha ya zawadi ya simu aina ya Ferrari.
Faiza akimzawadia pesa mwanaye.
STAA wa filamu za kibongo, Sara Mwakapala hivi karibuni alimzawadia mtoto wake VitAnthonio,  Simu aina ya Ferary yenye thamani ya shilingi laki tano kwenye sherehe yake ya kuzaliwa alipokuwa akifikisha miaka mitatu.
Kwenye sherehe hiyo, walihudhuria mastaa mbalimbali akiwemo Faiza ambaye ni mzazi mwenzake Mbunge wa Mbeya, mheshimiwa Joseph Mbilinyi  ‘Sugu’, Baby Candy, Khadija Kasongo , Shetta na wengine wengi.
Wengine waliotinga kwenye shughuli hiyo ni watoto waalikwa na mashoga mbalimbali ambao walifika kwa ajili ya kusherehekea na Sara ambaye alikuwa na furaha ya mwanaye kutimiza miaka hiyo.
(PICHA NA HAMIDA HASSAN / GPL)
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."