Na Francis Godwin, Iringa
MABAKI ya mwili wa mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ambaye jina lake halikufahamika, yamekutwa eneo la Magereza, Kata ya Miyomboni Kitanzini, Manispaa ya Iringa.
Walioyakuta ni maofisa wa magereza ambao walikuwa katika eneo hilo na wafungwa wakikata miti kwa ajili ya kuni.
Wakizungumza na Amani, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa mwanamke huyo inaonekana siku ya kifo chake alikuwa amevaa suruali nyeusi, kilemba cha kitenge chenye madoa mekundu, njano, meusi na meupe pamoja na skafu ya rangi nyeupe na nyeusi.
Mashuhuda hao walidai kuwa mwanamke huyo alipoteza maisha kwa zaidi ya wiki mbili nyuma kutokana na mabaki hayo kuharibika kupita kiasi na kukauka.
Mabaki ya mwili huo yalichukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika Chumba cha Maiti cha Nina Marwaha cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa.
MABAKI ya mwili wa mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ambaye jina lake halikufahamika, yamekutwa eneo la Magereza, Kata ya Miyomboni Kitanzini, Manispaa ya Iringa.
Polisi wakikusanya mabaki ya mwanamke huyo.
Mabaki hayo yalikutwa majira ya saa 6:00 mchana, juzikati yakiwa yamesambaratika kutokana na kuoza.Walioyakuta ni maofisa wa magereza ambao walikuwa katika eneo hilo na wafungwa wakikata miti kwa ajili ya kuni.
Wakizungumza na Amani, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa mwanamke huyo inaonekana siku ya kifo chake alikuwa amevaa suruali nyeusi, kilemba cha kitenge chenye madoa mekundu, njano, meusi na meupe pamoja na skafu ya rangi nyeupe na nyeusi.
Mashuhuda hao walidai kuwa mwanamke huyo alipoteza maisha kwa zaidi ya wiki mbili nyuma kutokana na mabaki hayo kuharibika kupita kiasi na kukauka.
Polisi akikusanya nguo za marehemu.
Mazingira ya kifo cha mwanamke huyo yalionesha utata kwa kuwa hata
polisi waliofika eneo la tukio, walikiri kutokuwepo kwa taarifa yoyote
ya mtu kupotea na kwamba inawezekana alivamiwa ama alikufa kwa
matatizo yake au alikuwa akitoka hospitali ambayo ipo jirani na eneo
hilo. Mabaki ya mwili huo yalichukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika Chumba cha Maiti cha Nina Marwaha cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment