Social Icons

Wednesday, May 8, 2013

SKENDO MTEGO WA KUJIUZA... AUNTY LULU ABADILIKA

Na Gladness Mallya
AMINI usiamini Global Publishers ni mtambo wa kurekebisha tabia! Siku chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kunaswa kwenye mtego wa kujiuza, sasa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha aliyokuwa akiishi zamani na kuwa na mwingine mpya.
Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Katika ‘exclusive interview’ na paparazi wetu jijini Dar, juzikati, Aunty Lulu alifunguka kuwa kwa sasa ameamua kubadilika kwani kama ni starehe amefanya sana pamoja na uchafu mwingi ila kutokana na mtego wa kujiuza kumnasa na ushauri aliopewa na familia yake, amebadilika na sasa amegeukia kwenye ujasiriamali.
Alisema kuwa anawashukuru waandishi wa habari wa magazeti ya Global Publishers kwani wamebadilisha maisha yake, kama siyo wao angefikia hatua mbaya lakini kwa sasa ametulia na anafanya mambo ya maendeleo tofauti na zamani ambapo alikuwa hajielewi anafanya nini.
“Yaani kutokana na mtego wa kujiuza nimeamua kubadilika kwa sababu jamii ilinichukulia tofauti sana hivyo nikaamua kufanyia kazi ushauri wa familia yangu niliokuwa nikipewa kila siku lakini nikawa naukataa.
Kwa sasa nafanya ujasiriamali na ninafurahia maisha haya kuliko yale niliyokuwa nikiishi zamani.
Aunty Lulu kwa sasa anamiliki duka la vipodozi na ni wakala wa kutoa na kuweka fedha kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi maeneo ya Kinondoni Kanisani, Dar ambapo ndipo anashinda kwa sasa na kwa mujibu wake  ameachana kabisa na kujiachia kwenye sehemu za starehe na kufanya mambo yasiyotakiwa katika jamii.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."