Social Icons

Thursday, May 16, 2013

CHAZ BABA AMVISHA PETE MCHUMBA’KE JUKWAANI


Na Musa Mateja
PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ juzikati aliendeleza harakati za maandalizi ya ndoa kwa mashabiki wake baada ya kumvisha pete jukwaani mchumba’ke, Rehema Sospeter.
Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ akimvisha pete mchumba’ke, Rehema Sospeter.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Amani lilijiri Mei 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama, Dar, wakati bendi yake ilipokuwa ikitambulisha albam mpya, Risasi Kidole.
Akizungumza na paparazi wetu mapema wiki hii, Chaz Baba alisema ameamua kuonesha uamuzi wake huo kuanzia kwa mashabiki wake waliofika ukumbini na kwa wale wasiofika kwa sababu wengi wao walikuwa hawamuamini.
“Nilifanya vile kukata vilimilimi ‘coz’ tangu nimegawa kadi za mchango wa harusi, kumekuwa na maswali mengi ambayo yanaashiria wengi hawaamini uamuzi wangu,” alisema Chaz.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."