Na Hamida Hassan
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Baby Madaha hivi karibuni waliingia katika mzozo wa kugombea nyumba ya kupanga iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya wote kudai kulipia kodi ya nyumba hiyo.
“Baada ya kumlipa dalali, niliwatuma watu wakafanye usafi lakini wakashangaa kumkuta Wolper anahamishia vyombo vyake kwenye nyumba hiyo.
“Waliponipa taarifa nilichanganyikiwa sana kwani nilishalipa shilingi milioni tatu na laki sita ikiwa ni kodi ya miezi sita hivyo niliamua kukimbilia kwenye Kituo ha Polisi cha Magomeni kufungua kesi ili nisaidiwe kuipata nyumba hiyo au nirudishiwe fedha zangu,” alisema Baby Madaha.
“Hata hivyo, rafiki yangu Mariam Mndeme alijaribu kuongea na Wolper ili atupe ushirikiano wa kupata haki yangu lakini hakutaka kutusaidia,” alisema Baby.
Gazeti hili lilimtafuta Wolper na kumuuliza kuhusu ishu hiyo ambapo hakupenda kuongea mengi bali alimuunganisha mwandishi wetu na mwenye nyumba, Zulfa ambaye alisema kuwa mpangaji wake aliyeandikishana naye mkataba ni Wolper na kama kweli Baby alilipa fedha kwa dalali, basi ametapeliwa.
“Jamani hii ishu hainihusu kabisa, ukweli ni kwamba hao akina Baby wametapeliwa, umemsikia mwenye nyumba alichokisema kwa hiyo sitaki mnihusishe kabisa kuhusishwa na mambo hayo,” alisema Wolper.
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Baby Madaha hivi karibuni waliingia katika mzozo wa kugombea nyumba ya kupanga iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya wote kudai kulipia kodi ya nyumba hiyo.
Jacqueline Wolper.
Katika sakata hilo, ilielezwa kuwa wa kwanza kulipia kodi ya nyumba
hiyo alikuwa ni Baby Madaha ambaye alidai kufanya malipo kupitia kwa
dalali na kabla hajahamia, Wolper naye alilipa moja kwa moja kwa mama
mwenye nyumba aliyefahamika kwa jina moja la Zulfa na kusaini mkataba
maalum.“Baada ya kumlipa dalali, niliwatuma watu wakafanye usafi lakini wakashangaa kumkuta Wolper anahamishia vyombo vyake kwenye nyumba hiyo.
“Waliponipa taarifa nilichanganyikiwa sana kwani nilishalipa shilingi milioni tatu na laki sita ikiwa ni kodi ya miezi sita hivyo niliamua kukimbilia kwenye Kituo ha Polisi cha Magomeni kufungua kesi ili nisaidiwe kuipata nyumba hiyo au nirudishiwe fedha zangu,” alisema Baby Madaha.
Baby Madaha.
Baby Madaha aliongeza kuwa baada ya kufika kituo cha polisi,
alifungua jalada la mashtaka (RB) lenye namba MAG/RB/163/2013 Wizi kwa
ajili ya kumfuatilia mtuhumiwa.“Hata hivyo, rafiki yangu Mariam Mndeme alijaribu kuongea na Wolper ili atupe ushirikiano wa kupata haki yangu lakini hakutaka kutusaidia,” alisema Baby.
Gazeti hili lilimtafuta Wolper na kumuuliza kuhusu ishu hiyo ambapo hakupenda kuongea mengi bali alimuunganisha mwandishi wetu na mwenye nyumba, Zulfa ambaye alisema kuwa mpangaji wake aliyeandikishana naye mkataba ni Wolper na kama kweli Baby alilipa fedha kwa dalali, basi ametapeliwa.
“Jamani hii ishu hainihusu kabisa, ukweli ni kwamba hao akina Baby wametapeliwa, umemsikia mwenye nyumba alichokisema kwa hiyo sitaki mnihusishe kabisa kuhusishwa na mambo hayo,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment