Mmoja wa wanafunzi aliyepandisha mashetani akiwa amelala baada ya kuanguka.
Mmoja wa wanafunzi aliyepandisha mashetani akiombewa.
Baadhi ya wanafunzi walioanguka.
Umati wa wazazi waliofika kushuhudia tukio hilo na kuwachukua watoto wao.
Baadhi ya viongozi wa eneo hilo pamoja na diwani wao wakielezwa na mwalimu jinsi tukio hilo lilivyoanza.
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini
Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku
wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu
kutanda maeneo hayo.Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.
(Picha/Stori: Gladness Mallya/ GPL)
No comments:
Post a Comment