Social Icons

Friday, May 3, 2013

GARDNER: NINGEKUWA SIJAOA NINGEMUOA VANESA MDEE

Na Mwandishi Wetu
MUME wa Legend wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jadee’, Gardner G Habash ‘Kapteini’ aliwaacha watu midomo wazi baada ya kusema kama angekuwa hajaoa, basi angemuoa msanii anayekuja kwa kasi kwenye gemu, Vanessa Mdee.
Vanessa Mdee.
Kapteini alitamka hayo juzi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Dar Indian Ocean 2013 kilichochukua nafasi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mume huyo wa Lady Jaydee alikuwa MC wa shughuli hiyo hivyo kutumia kipaza sauti kumnadi Vanesa.
Gardner G Habash ‘Kapteini’.
“Kiukweli Vanesa ni msanii mzuri, ana uwezo mkubwa wa kufanya muziki wa Hip Hop na kulitawala jukwaa. Ningekuwa sijaoa kwa kweli ningemuoa Vanesa Mdee,” alisema Gardner.
Mbali na Vanesa, wasanii wengine wanaounda familia ya B Heatz walipata nafasi ya kutumbuiza katika hafla hiyo akiwemo mkongwe, Ally Baucha.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."