Social Icons

Friday, May 3, 2013

LINEX AKATAA KUFUNGA NDOA KWA FASHENI

Na Gladness Mallya
KUTOKANA na ndoa za mastaa wengi kuvunjika, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Sunday Mangu ‘Linex’ amefunguka kuwa japokuwa ana mchumba hayupo tayari kuoa kwa fasheni kwa kumuiga mtu f’lani kwani anaogopa kuharibu dira nzima ya maisha yake.
Sunday Mangu ‘Linex’ akiwa na mchumba wake Suvi Rikka.
Akichezesha taya na paparazi wetu juzikati, Linex alisema kwa sasa yeye na mchumba wake Mzungu aitwaye Suvi Rikka bado wanasomana na kila mmoja akisharidhika na tabia ya mwenzake ndipo suala la ndoa litafuata.
“Mimi sitaki kuoa kwa fasheni eti kwa kumfuata mtu f’lani na sitaki kufunga ndoa leo halafu kesho imevunjika, nataka mimi na mke wangu tuishi milele,” alisema Linex.
...Wapenzi hao wakiwa katika pozi.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."