Social Icons

Friday, May 3, 2013

MCHUMBA WA MTU ATUPWA JELA KWA KUJIUZA!

Na Richard Bukos
MREMBO Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda jela miezi 6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.
Brandina Barthon akiwa chini ya ulinzi.
Brandina alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika, mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa wengine.
Brandina Barthon akipelekwa kwenye karandinga.
Hukumu hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio lakini mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa macho.
Wakati mwanamke huyo akiangua kilio, afande wa Jeshi la Magereza alimfikia na kumchukua  kwa ajili ya kumpeleka kwenye Karandinga kuelekea Gereza la Segerea kuanza maisha ya jela.
Brandina Barthon akipandishwa kwenye karandinga.
Mbali na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya kutolewa hukumu hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

 

for more information call us

+255718953088
-------or-------
+255784953088
*email*
innocentfabian@gmail.com
THANKS

quote of the day

"Don't criticize me simply because I am different. Understand me, and you will most likely appreciate my difference and criticize your variance."