Surprisingly, Producer huyu hutumia viboko kuirejesha
discipline studio kwa wasanii wanapungukiwa ama kukosa kabisa discipline wakiwa
wanarekodi.
Hahahah, hiki ndio kiboko anachotumia Tiddy awapo studio, it's funny right? |
Katika interview aliyofanya na MilazO 101 ya Radio One, Tidd
Hotter alipoulizwa alikiri kuwatandika
mboko a.k.a bakora wasanii akiwa studio, lakini alisema sio kwa ubaya ni kwa
uzuri na kwa urafiki tu.
“hahahaaa..yeah, unajua hiyo inatokana na baadhi ya wasanii
wanapokuwa hawako serious, unajua kuna kukosea kwa aina nyingi, mtu anaweza
kukosea kwamba kweli akili yake iko mbali na ukweli anaohitaji kuujua kwa muda
ule, na kuna mwingine unaona kabisa
anahitaji tu juhudi flani kuliko matani, kwa hiyo wengine wanaleta matani
kidogo na hiyo ni kazi yangu sa inabidi twende sawa kidogo ili kumfanya
a-concentrate, unajua kiboko ni kitu kizuri kinachomfanya mtu a-concentrate
kwenye kazi, sio kwa ubaya ni kwa urafiki tu kwa sababu baada ya hapo mnacheka
tu vizuri..yeah.”
Inawezekana ukajiuliza labda jamaa anaitumia adhabu hii kwa
wasanii wa aina gani, ambao wako chini yake ama yeyote, jamaa anafunguka.
“ni yeyote tu, kwa mfano kuna muda mwingine huwa na project
za kwaya, labda tunarekodi nyimbo nyingi halafu inafika usiku, unakuta kuna
wakina mama wenye umri mkubwa kabisa hata wanaweza kunizaa, wanakuwa wanalala
wakati wa vocal. Kwa hiyo kiboko ni kitu ambacho nakitumia kumuamsha mtu awe
kwenye ileee….”
Talking about umri wao, “Nawachapa wamama wakubwa sana,
miaka hata wanafika 40, 50..wapo ambao wanalala wakati wa vocal, so
napowapitishia viboko ..tah tah taaah…wanaendelea, kwa hiyo inasababisha mtu
anaconcentrate..siwachapi niwaumize, na hata napokuwa nachapa siwachapi kama
watoto wa shule niwachape niwaumize, yani ni kwa ajili tu ya kushtua, yan
kuwagugusa watu kwenye brain, basi kitu kama hicho.
Tiddy aliulizwa, Wapo wasanii wengi wakubwa ambao jamaa
ameshafanya nao kazi kama Belle9, Hardmad, Dark Master, Joslin, Dudu Baya na
wengine wengi ambao wanafanya nae kazi ,je kuna mmoja kati yao alishawahi
kukutana na adhabu hiyo(bakora).
“Yaani hao kwa sababu walishazoea na wanaijua game siku
nyingi na experience yao ni kubwa najikuta siwezi kutumia hiyo njia, lakini
natumia hiyo njia kwa sababu kuna wasanii wengine wanaichukulia kazi hii ya
muziki kama sijui wanafanya nini?! Kwa hiyo anajikuta anaingiza mawazo mengine kwenye
muziki. Kwa hiyo kakiboko kale ka mgongo kanasababisha mtu anakuwa sasa
ah..kumbe nafanya kitu flani. So badala ya kutumia bangi au pombe ama nini mtu
unamshtua brain yake na kuconcentrate kwenye kitu kwa kumuonesha kuwa kuna ka
kiboko hapa..hahahahaa.”
Tiddy Hotter alimaliza kwa kusema Discipline ya mtu
inamsababisha mtu kuwa mtu kwenye kile kitu anachokifanya.
msikilize Tiddy hotter
msikilize Ben Pol pia akiongelea Nidhamu katika kazi:
No comments:
Post a Comment